Itafika wakati nami nitampata anipendaye kweli?

Itafika wakati nami nitampata anipendaye kweli?

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,377
Reaction score
4,847
Miaka inakimbia kama Tuisila Kisinda/Tk Masta hainisubiri sababu mimi sio special hata ningekua special isingeweza nisubiri.

Ukija kwenye sekta ya mahusiano nako ni afadhali ya jana kuliko leo sijui ndio kusema mtu kadandia mtumbwi wa... kila sehemu nakula za kichwa, nikienda kwa yule ananiambia yupo kwenye mahusiano yake na mwezi ujao anaolewa, nikienda kwa X wa zamani ananiambia sorry ulichezea bahati for now i have 3 kids na tunapendana na baba watoto wangu sana tena futa namba yangu.

Nafikiria sana je, niachane na mambo ya beb mamas na nijikite kwenye kutafuta mapene aka shekeri kidogo natembea navutiwa na binti mrembo wa mitaa ya mbele napewa namba za simu charting ya kwanza hello hello, za kwako nzuri, tunaendelea ehee unajua flani ninakupenda naomba uwe rafiki yangu, message inayorudi unajua pale ninapoishi kodi inaisha mwezi huu kati ya laki 6 nina laki moja niongezee laki 5 dia ndipo naitwa dia kwa mara ya kwanza.

Jibu langu sina pesa kwa hiyo afta natuma sms kimya naenda dukani kwa masawe naweka vocha ya mia 5 napiga hakuna salamu majibu yake achana na mimi bahili wewe.

Nataka kulia ila nakumbuka kauli ile inasema wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika natulia navuta pumzi najipa moyo.

Nakuja Jf kwa watu wenye IQ kubwa kubwa naandika mada yenye kichwa cha habari “Natafuta mchumbwa wa Kike sina vigezo vingi,“ nako sipati mtu.

Sasa hapa najiuliza kwani kosa langu nini mbona mapenzi hayanitaki japo mimi nayataka.

Hebu nanyi wana Jf mnishauri nikimbilie wapi mimi au kisa mimi mshamba au niache ushamba, nzuri mbaya nafikiria hapa.
 
Miaka inakimbia kama Tuisila Kisinda/Tk Masta hainisubiri sababu mimi sio special hata ningekua special isingeweza nisubiri.

Ukija kwenye sekta ya mahusiano nako ni afadhali ya jana kuliko leo sijui ndio kusema mtu kadandia mtumbwi wa... kila sehemu nakula za kichwa, nikienda kwa yule ananiambia yupo kwenye mahusiano yake na mwezi ujao anaolewa, nikienda
Endelea kutafuta mapene mbona watajileta wenyewe tu
 
Utakataa ila deep down 👇
HUJIAMINI!!
 
Mmew unakupenda, mmea utakuweka huru !

images - 2022-06-06T173602.357.jpeg
 
Unaweza ukawa bado unaishi naye ila machalii wenye mpunga watakusaidia kumtunza (kumgharamia mahitaji yake)

Hapo sasa itabidi nitafute mamilo mmoja akubaliane na kipato changu ili asiende kwa machalii manake hawa na huruma
 
Wanaume mna uwanja mpana sana na muda wa kutosha kupata mwenza. Utapata mtakayependana,tuliza akili na usikurupuke usije kupata atakayekufanya uyachukie mapenzi
 
Back
Top Bottom