Israel: Waziri Mkuu Netanyahu afikishwa Mahakamani huku akiwa bado madarakani

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefikishwa mahakamani katika kesi iliyokuwa ikisubiriwa kwa shauku kubwa dhidi ya ufisadi kwa muda wa miaka mitatu, kesi hiyo iliahirishwa mwezi Machi kutokana na janga la corona.

Netanyahu amekuwa Waziri Mkuu wa kwanza aliyeko madarakani kufikishwa mahakamani tangu kuundwa kwa taifa la Israel zaidi ya miaka 70 iliyopita.

Tanzania pia inahitaji katiba inayo ondoa watu kuwa juu ya sheria.

#katiba mpya
FB_IMG_1590405688804.jpeg
 
Huyo jamaa si ndio wanasema mtu mwenye IQ IQ kubwa sana apa duniani, Achan na kitu madaraka siasa ni ulevi mkubwa sana
 
Wazungu wanajua wazi kua kwenye jamii yoyote wenye akili ni wachache ila wajinga ndio wengi ila wakakubaliana mambo ya msingi, sheria, katiba na mambo ya kitaalamu waachiwe wataalamu na wenye akili kuyatungia sera na kuyasimamia ila mambo yasiyo na msingi kama siasa na mambo mengine tuwaachir watu wote, wajinga na wenye akili ila hakuna atakaeruhusiwa kuvuruga sera na misingi yote iliyotengenezwa na wenye akili ila labda kuboresha.

Wao walikubaliana kua wataongozwa na sheria na kanuni zilizotungwa na wenye akili.

Huku Afrika, tukakubaliana kua sheria, katiba, sera na mambo ya msingi tuwaachie wajinga ndio waamue wanalolitaka na yoyote atakaetaka kuboresha au kupiga kilichoandikwa na wajinga auwawe, afungwe au apotezwe. Kwamba wajinga ndio watoe muongozo wa maisha ya watu wote, wenye akili na wajinga wenzio.

Hivyo basi sisi tutaendelea kuwapigia magoti wazungu na kuwalamba makalio maisha yetu yote labda hadi hapo mungu atakaporudi kama yupo.
 
Yaani Kuna viongozi hawajui kutumia madaraka yao vizuri. How come wewe NI kiongozi wa nchi unababaishwa? Waje Africa tuwape mwongozo Kama walivyofanya Putin na Kim jong II
 
Wazungu wanajua wazi kua kwenye jamii yoyote wenye akili ni wachache ila wajinga ndio wengi ila wakakubaliana mambo ya msingi, sheria, katiba na mambo ya kitaalamu waachiwe wataalamu na wenye akili kuyatungia sera na kuyasimamia ila mambo yasiyo na msingi kama siasa na mambo mengine tuwaachir watu wote, wajinga na wenye akili ila hakuna atakaeruhusiwa kuvuruga sera na misingi yote iliyotengenezwa na wenye akili ila labda kuboresha.

Wao walikubaliana kua wataongozwa na sheria na kanuni zilizotungwa na wenye akili.

Huku Afrika, tukakubaliana kua sheria, katiba, sera na mambo ya msingi tuwaachie wajinga ndio waamue wanalolitaka na yoyote atakaetaka kuboresha au kupiga kilichoandikwa na wajinga auwawe, afungwe au apotezwe. Kwamba wajinga ndio watoe muongozo wa maisha ya watu wote, wenye akili na wajinga wenzio.

Hivyo basi sisi tutaendelea kuwapigia magoti wazungu na kuwalamba makalio maisha yetu yote labda hadi hapo mungu atakaporudi kama yupo.
Bonge la andiko kwa mwezi huu mzima ISIPOKUWA huo mstari wa mwisho.
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amevishambulia vikali vyombo vya sheria vya nchi yake, akivituhumu kula njama ya kumuondoa madarakani, na kujitaja kuwa kiongozi imara wa sera za mrengo wa kulia. Netanyahu alisema hayo jana alipofikishwa mahakamani, katika kesi iliyokuwa ikisubiriwa kwa shauku kubwa.

Amekuwa akiandamwa na shutuma za ufisadi kwa muda wa miaka mitatu, na kesi hiyo iliahirishwa mwezi Machi kutokana na janga la corona.

Netanyahu amekuwa Waziri Mkuu wa kwanza aliyeko madarakani kufikishwa mahakamani tangu kuundwa kwa taifa la Israel zaidi ya miaka 70 iliyopita. Kiongozi huyo ameishutumu polisi, waendesha mashtaka, vyombo vya habari na mfumo mzima wa sheria, kufanya hila ya kumpindua kinyume na matakwa ya wananchi.

Wakosoaji wake wamesema kauli yake ya kuvikosoa vyombo vya sheria inaweza kuathiri imani ya wananchi juu ya vyombo hivyo.
 
Back
Top Bottom