Israel:Wanajeshi wetu hawaendi ICC

Israel:Wanajeshi wetu hawaendi ICC

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,230
Reaction score
3,333
150103174852_israel_640x360_ap_nocredit.jpg

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa hatakubali wanajeshi wake kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC.

Alikuwa akizungumza katika kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri tangu Palestina ilipotuma ombi la kujiunga na mahakama ya ICC ambayo wana imani itaifungulia mashtaka Israel kwa madai ya uhalifu wa kivita katika maeneo inayokalia.


141224141821_israel_soldier_640x360_reuters_nocredit.jpg

Bwana Netanyahu ameishtumu Palestina kwa kutumia njia ya mapambano.

Israel imezuia kitita cha dola millioni 125 ufadhili wa fedha za kila mwezi kwa Palestina kama kodi inayochukua kwa niaba yake kama makubaliano ya mkataba wa amani.

Hatahivyo Palestina imepinga hatua hiyo ikitaja kama adhabu dhidi yake.



Source: Israel:Wanajeshi wetu hawaendi ICC - BBC Swahili
 
Safi sana Netanyau Gaidi hawezi kukufanya ukashitakiwe pale unapomtandika sana
 
Back
Top Bottom