ISRAEL v/s IRAN.

Status
Not open for further replies.
We umesahau kua Mh Kikwete na Obama wametulete Umeme mpaka vijijini?!
Njoo upande FISI bhana!
Umeme umeletwa na Obama bhana sio Iran!
Teh, teh, teh teh! Ngoja nisubiri majibu ya mstari wangu huo wa mwisho kutoka kwako!
Kumbuka USA hatoi msada bila lengo, hakuna cha bure lazima damu za wa Tanzania zitalipa tu.
 
waajemi walitolewa palestine mwaka 634 mda huo yesu alishaga kufa,kumbuka wakati yesu yupo eneo hilo lilikua chini ya Roman empire ,eneo zima likijulikana kama palestine,zilipita himaya nyingi kama waasyria na pia nebukedneza wa himaya ya babylon na ndie alievunja hekalu la solomon,kabla hawajafuata persia empire,ottoman empire kisha british empire kisha ndo baadhi ya nchi zikaanza kupata uhuru hapo.

Nitaenda zaidi in deep kwa kuweka miaka baadae .
 
Hi mada haikuwa ya kidni wala nini, tatizo linakuja pale wengi wenu nyie wakristo mikisikia tu Israel mnakuja dai eti ni taifa la Mungu, vipi liwe taifa la Mungu wakati hakuna hata ujumbe mmoja wa Mungu waliufata.

Mnao anzisha dini ni nyie na tukisema ukweli mnanza kuleta za kuleta.

Turudi kwenye swali lako.

Mataifa yote yanajulikna yalipo toka isipokuwa taifa la Israel hawajulikani walitoka wapi ndo mana wanachukua nchi sio zao.

We umeona wapi taifa duniani lemekalia sehemu si zake isipokuwa taifa la Israel.

Hivi hawa wangekuwa taifa la Mungu wange hangaika kuiba ardhi sio zao, hivi inakuja akilini kweli.

Kuhusu vita Israel kapigana vita vyote kwa kupewa msada na USA na Western countries hakuna vita aliye pigana hakupewa msada na USA, sema western media wanajidai tu kusema kuna vita kaenda bila USA wakati si kwlei hata siku moja.

Iran kapigana vita na Iraq miaka 8 na wakati Iraq ilikuwa ikijulikna kama ni strong kuliko Israel, na Iraq ilikuwa ikisaidiwa na nchi zote za kiarabu na USA na Western na Iram hakushindwa vita, ni uwongo kabisa kusema Iraq iliwashinda sababu walio omba vita ismamishwe ni Iraq sio Iran.

Iran imewekewa vikwanza tokea 1979 na USA na Iran ndo kwanza inaendelea na Jana tu the supreme leader wa Iran, Ayatollah Ali Khamen ana muambia Rais wa Iran anapoteza time tu kuongea na USA, mana USA ni shetan na shetan hawezi kuaminiwa hata siku moja, yani inaonyesha vipi Iran hana hata haja ya kuongea na USA au awe rafiki yake.
http://www.nytimes.com/2013/10/06/w...-questions-aspects-of-rouhanis-trip.html?_r=0
 
kabla sijaenda ndani zaidi yapasa ujue kuwa wakati waisrael wanatoka utumwani misri na kuja caanan nchi ambayo maandiko yao wanadai ilikua ya ahadi,walikuta wenyeji maeneo hayo na ilibidi wapigane ili kupata maeneo.wakiongozwa na joshua ndo waliteka baadhi ya maeneo ambayo ndo walianzisha utawala wao.lakini waligawanyika makundi mawili yaani ilikuwepo israel kingdom ambayo kama sikosei ikiwa na mji mkuu uitwao samaria,pia ikawepo Judea kingdom ikiwa na jerusalem kama mji wake lakini jerusalem ikijulikana kwa jina lingine limenitoka.

Baada ya mapigano kati ya ufalme wa israel na ule wa yuda.alifuata mtawala wa yuda aitwaye DAUD .Na ndiye aliunganisha hizo falme mbili ikawa moja Israel kingdom.baada ya king david kufa alifata mfalme solomon ,lakini baada ya solomön falme hizi mbili ziligawanyika tena.
Na ni kipindi hicho ndo eneo hilo likavamiwa na nadhani waasyria na ndo ukawa mwisho wa israel kingdom na judea kingdom.wakasambaratika wengine ndo wakakimbilia nchi za europe,kumbuka hapo ni kabla ya yesu hajazaliwa.
Bado walibaki wayahudi hapo mpaka wanakuja waroma.
Na ni kipindi cha waroma ndipo yesu alizaliwa.
Nikipitia reference ntakuja niweke na miaka ili story ikae sawa kwani naongea kwa kutumia kumbukumbu zilizo kichwani,ila mwenye maelezo zaidi anaweza kuchangia.
 



Hizbolah Hana uwezo wa kuipiga Israel na tena ni kikundi ambacho kinafanya propaganda tu kwenye vyombo vya habari Kama yalivo makundi mengine!

Unapoingia vitani athari nyingi Hua zinatokea za kiuchumi Na kuaribika miundo mbinu na watu kupoteza maisha na ata raia wa kawaida!

Vita nyingi Hua na sababu mbalimbali na zingine hazina faida ata kwa wananchi! Mfano Ile vita ya 2006 dhidi ya Hizbolah. Waisrael hasa raia wa kawaida wengi hawakupenda taifa Lao kuingia vitani na ndio Maana ukaona makelele mengi yalitokea lakin hiyo haimaanishi kua Waisrael waoga Kama unavooamini! Tumeona ata Hapa kwetu watu wakilazimishwa kua wazalendo baada ya ule mzozo wa Rwanda

Ninachotaka kusema Ni kwamba waisrael wakiwa pamoja wakiungana na kua wamoja na kua na sababu ya msingi kuingia vitani basi hakuna taifa ata moja ata Iran itachapwa asubui tu!

Alafu tusilinganishe Israel na kikundi Kama Hizbolah au Hamasi Maana hizo ni vurugu tu!
Wewe mwenzio anapita na Kifaru cha kisasa kinachotegua mabomu uliyoyatega ardhini kwa ukubwa wa eneo la mita200 mraba alafu wewe unataka kumshambulia kwa Manati au kombeo! Si ni vichekesho! Hayo ndio yanayojiri kwa Hamasi Na Hizbolah.
 
mimi nachojua katika vita, hamna mshindi. Baada ya vita kwisha wote mnakuwa mmepoteza, ama raia, mali,na hata uchumi lazima uyumbe. Vita haina mshindi bhana! Embu wekeni hapa ni nchi ipi ilishinda kwenye vita dhidi ya nchi nyingine!

marekani dhidi ya iraq
 
Tafuta sababu ya vita ya Israel na Hizbullah ya mwaka 2006 ilianza sababu gani?

Israel alingia kwa lengo la kuwakomboa matekwa wake mawili, mwisho wa vita hakupata alicho kitaka ikabidi aombe wa German wawasaidie kuwarudisha hao, ikabidi Israel awafungulie matekwa wote wa Lebanon na wa kiarabu ndo apewe hao wanajeshi wawili.

Ukweli ni Hizbullah won the war because they've got what they wanted.
 

Unaenda vizuri ila kuna vitu unachanganya kidogo Kama Nebkandineza na kuvunja hekalu la Solomon
Na kwa mtazamo huo kunaonekana kua taifa la Israel lilikuwepo
Sio ndio lilianzishwa1948
 
Hivi we mzima kweli? Unadhani kuwa katika Jamii forum mda mrefu ndo unanizidi akili au unanizidi kitu.


Hivi we mwanajeshi msatafu, katika akli zako unadhani wote walio kuja join kwenye jeshi bada yako uliwazidi cheo, na ujuzi wa kijeshi.

......Experience matters !
 

Ayatollah Ali Khamen huyu ni Kiongozi wa kidini bila Shaka!
Na kwa mujibu wa unabii atakua anaelewa vizuri kile anachokisema!
Na atakua anafahamu nini kitakujatokea Hapo baada Kati ya Us Na Israel na Ulaya na Roma kwa ujumla!
Sio Kama Iran hana shida ya kuongea na Us ila ni kwamba ata Iran ifanyeje Us na washirika wake hawawezi kubadilika! Ni udhalimu kwa kwnda mbali! Na bila Shaka Ayatollah Ali Khamen anafaham wazi kua Us na washirika wake wataitawala Dunia kabla ya Kiama na kwa maanahiyo cola zote zitakazokwenda kinyume nao zitaangushwa!

Tumeona Iraq, Libya, Syria Iko njian na mataifa mengine ya kiarabu yamekua vibaraka yameupokea huo ufedhuli wa western!
Wakimaliza Syria wanaingia Iran na ndio Maana Hapo nyuma nilisema Iran lazima itapigwa tu kwa namna yeyote!

Hapa naongea kiimani na kwa mujibu wa Unabii unavonielez!
 

Kumbe Israel Ile ni nchi Yao ya ahadi kwa mujibu wa Maandiko Yao na hili taifa lilikuwepo kabla ya Palestine!

Umetlilika vizuri katika history ingawa kuna vita vichache unavichangaya lakini mengi unaweka Sawa na ndio Maana Mimi nikaona Vema kurudi katika history ya zamani kabisa kulikoni kubishana tu na Hapa tumeamza Kufahamu mwanza Israel ulikuwapo tangu zamani Na tawala zizopita!

Ninaswali jingine ni kwanini Hawa waisrael walikua wanagawanyika Na kupigwa na kuchukuliwa utumwani?
Sababu inaweza kua walikua wakimkosea Mungu wao?
Na kukaliwa kutawaliwa au kuchukuliwa utumwani kilikua kunawaondolea uhalali wa nchi Yao?
Maana kuna watu wanasema Israel pale sio kwake ni wavamizi tu!
 
Unaenda vizuri ila kuna vitu unachanganya kidogo Kama Nebkandineza na kuvunja hekalu la Solomon
Na kwa mtazamo huo kunaonekana kua taifa la Israel lilikuwepo
Sio ndio lilianzishwa1948
mkuu ujue wakati wa saul,david na solomon kulikuwepo na united kingdom of israel,baada ya seleman kufa alifuata mtoto wake Rehobam ndo akawa mtawala wa israel,lakini mfalume huyu alikua katiri akiwatesa watu wake hadi wakamwasi,wakapigana wao kwa wao mpaka wakajitenga kati ya israel na judea.

Wameendelea hivyo kwa kama miaka 200,wakaja waasyra wakaiteka israel,wakawatawanya waislaeri sehemu mbalimbali za himaya yao.katika israel iliundwa na makabila kumi ya wana wa israel,hayo makabila ndo wakati wa yesu yalijulikana kama makabila ya israel yaliyopotea.
Judea nayo baada ya miaka 300,ilitekwa na wababeli chini ya mfalume nebukedneza wa babeli(irag ya leo).na ni huyo mfalme aliteka jerusalem ya yuda na kubomoa hekalu la solomon,akawaondoa wayahudi jerusalem mpaka walipokuja watawala wapya wa persia ndo wakaruhusu wayahudi kurudi,lakini tayari hizo falme mbili za waisrael zikawa zimeishia hapo.
Hadi warumi wanakuja kutawala ndo eneo hilo likajulikana kama palestine.
Ndo kipindi hicho yesu alizaliwa,kuanzia yesu anazaliwa hapakuwa na israel kwani eneo hilo lilikua chini ya roman empire...ndo wafuate egypt empire,ottomani empire ,british empire.
Baada ya vita ya pili,ndo waingereza walifanya mkataba wa bailfoul na wayahudi waliokua ulaya baada yao kuwasaidia kipesa waingereza kumshinda adolf hitler ndo uingereza ikawalipa kwa kuruhusu wayahudi kurudi pale palestine.
Lakini wale walikua ni wayahudi wazungu waliozaliwa nje ya eneo hilo na wengi walikua wa ukoo wa ashekenaz
 
ukweli ni kuwa sio falme ya israel pekee ndo walipigana.kulikua na falme nyingi ambazo zilikuwepo enzi hizo leo hazipo,falme kama mesopotamia,rumi,persia british,mongolia.etc.

Kwahapa africa kuna mali,timbuktu etc.dunia inabadilika hata tanganyika enzi za yesu haikua inaitwa tanganyika.
Walichofanya watu wenye asili ya kiyahudi huko ulaya ni kutumia fursa ya vita vya pili vya dunia kuwashinikiza wazungu kuunda upya kwa taifa la israel.
Ni sawa na leo mngoni wa Tanzania arudi africa kusini na kuchukua maeneo ya o yaliyokua chini ya zwangedaba.
Tofauti hapa ni kuwa kwa asili kabisa ile eneo lilijulikana kama caanan kabla hata ibrahimu babu yake jacob hajahamia hapo akitokea Ur.
 

Kilichokua kinapita ni zile Tawala na kuja zingine lakini taifa la Israel lilikua halifutiki katika USO wa Dunia!

Hawa waisrael maisha Yao tangu Hapo zama hizo ni vita kutawaliwa kuchukuliwa utumwani na kutulia taifa Lao kwa nyakati kazaa! Na katika yote haya Mungu alikua hawaachi!

Unaweza ukaniambia ni kwanini hawa watu wamekua ni wa maswaibu sana?
 
mimi nachojua katika vita, hamna mshindi. Baada ya vita kwisha wote mnakuwa mmepoteza, ama raia, mali,na hata uchumi lazima uyumbe. Vita haina mshindi bhana! Embu wekeni hapa ni nchi ipi ilishinda kwenye vita dhidi ya nchi nyingine!

Tulijitia viherehere tukamchakaza Amini ( uganda) lakini nadhara ya vita yalitutesa zaidi ya miaka 20
 

Kwanini Ayatolla amwambie Rais wake kua anapoteza muda kijadili na Us na kwamba kua Us ni Sheitwan na Sheitwan Hua haaminiki?

Naomba tuojadili hii kauli ata Kama kwa Imani zetu!
Huyu Ayatollah anavigezo gani vya kumfanya aseme hivo na anaona niñi mbele na Huu Usheitwan wa Us kautoa wapi na utakua na mpango gani Na Dunia?
Naomba majibu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…