Israel siyo taifa teule

Acha porojo. Biblia nimesoma kuliko unavyodhani. Israel wanachofanya ni upuuzi
 
Ushasagiwa chupa uchanganye na juice unywe habari zimeandikwa hizo... unadhani vita zilianza miaka hii?
 
Haukuwa na haja ya kutumia reference ya Biblia , kama huamini kuwa Israel Ni taifa teule. Maana Biblia ndo inaonyesha kuwa Israel Ni taifa teule, Asilimia kubwa kuanzia Mwanzo Hadi cha mwisho inaelezea taifa la Israeli Inaonyesha Mungu ndiye aliamua na aliyelichagua liwe taifa teule.
Mukusudi na njia za Mungu huwezi kuzielewa kisiasa na kidini,
Matendo yao hayaondoi uteule wao, Ni sawa mtoto wako akivuta bangi au akikukosoe anabaki kuwa mtoto wako ila hukumu na adhabu ndo utaamua umpe ya namna gani,
 


Mkuu, unachanganya sana historia.

Wafilisti ndio hao Wapelestina, wapalestina ni Waarabu wa kale sana miongoni mwa Waarabu na walikuwepo kabla hata ya ujio wa waarabu wa Saudia, waarabu wa Saudia ndio uzao wa Ismail Mwana wa Ibrahimu kwa maneno Mengine Sio Waarabu wote ni uzao wa Nabii Ibrahimu au unaweza kusema kwamba kabla ya Nabii Ibrahimu "Bara arabu" tayari kulikuwepo na Makabila ya Waarabu miongoni mwao ndio hao Wafilisti (Wapalestina).

Nabii Musa (as) aliamrishwa na Mungu awaokoe Wana Wa Israeli kutoka Misri na awaingize hapo Palestine ambamo alitakiwa awapige hao Wafilisti ili achukue udhibiti wa hiyo nchi kwani wao Waisreali kuingia hapo isingekuwa jambo rahisi bila kupigana na utawala wa Wafilisti katika zama zile ingawa Musa as alishindwa kuwashawishi Waisraeli kupigana lakini baadaye baada ya miaka 40 kizazi kipya cha Waisraeli chini ya (Joshua??) Waliweza kuingia na kuwapiga Wafilisti (Wapalestina) na kuchukua mamlaka ya nchi hiyo, katika zama hizo kukawa na Makabila matatu makuu yaliyokuwa yakiishi katika eneo hilo; Wafilisti (Wapalestina walionyanganywa mamlaka), Waisraeli na Makabila mengine ya Waarabu kama Mabedui (Bedouins) hawa Wapalestina ndio waliokuwa wakiitwa Wasamaria (Samaritans) katika Biblia.

Zama Yesu alipotokea hapo Palestine kulikuwepo na Makabila mawili tu kati ya Makabila 12 ya Waisreali makabila hayo ni Judea na Benjamin makabila 10 yalikuwa yametawanyika sehemu.mbalimbali duniani mfano Ulaya, India, Afghanistan, Bara Arabu yote, Iran nk, na haya makabila yalikuwa yamechukuliwa utumwani na mfalme Nebuchadnezzar wa Babylon na alipowaacha huru kutoka utumwani ndipo hawakurudi Palestine wakaamua kutawanyika katika sehemu mbalimbali za dunia.

Yale makabila mawili yaliyobaki ya Waisraeli yaliyobaki Palestina yakamezwa na Makabila ya Waarabu yaliyokuwepo wakati huo na identification yao ikafutika baada ya miaka 2000 na ushee kupita ndiyo maana mwaka 1948 umoja wa mataifa kwa kuwaonea huruma Waisreali baada ya kuuwa sana na Wazungu wa ulaya na hasa Nazi ya Hitler ikaona ili kuwafariji itabidi watafutiwe nchi ya kuishi, option zilikuwa; Argentina , Uganda, Canada, Marekani na Palestine kipindi hicho Palestine ilikuwa inatawaliwa na Waingereza na James Balfour Muingereza ndiye aliyepeleka UNO azimio la kuanzishwa taifa la Israel --- Wakafanya ujanja kutokuipa Uhuru nchi ya Palestine na hapo hapo kumega kipande cha nchi hiyo na kuanzisha taifa la Israeli ili hapo baadaye Israeli iimeze Palestine yote kitu ambacho Israeli leo ndicho anachofanya.
 
MUNGU WA ISAKA, MUNGU WA IBRAHIM, MUNGU WA YAKOBO. MUNGU WA ISRAELI.

MUNGU WA BABA YENU (waisraeli) NILIYEKUTOENI KATIKA NCHI YA UTUMWA.

Kwanini hatajwi kama MUNGU MUUMBA ULIMWENGU? Kwanini aliongea na kuingia mikataba(maagano) na hao jamaa tu?!


Hawa jamaa huyu ni Mungu wao sie wengine tumemshobokea tu lazma tuwe kama watoto wa kambo.


Misri walikua na miungu yao, Ugiriki walikua na miungu yao, Ulaya Kaskazini walikua na miungu yao, kila sehem walikua na imani zao na walidili na miungu yao kwa namna tofauti tofauti. (Tusome sana historia na maandiko tusikariri Biblia tu na Qurani).

Wana wa Israel Mungu wao alikua anawaacha kama wakimsahau, hata sehem zingine ilikua ni hivo hivo tu.
Sasa swala la kila taifa kumkubali mungu wa Israeli maana yake ni kwamba Miungu yetu tumeikataa na mkataa kwao ni mtumwa.

Nisiwachoshe sana ila dunia ilijichanganya sana kumgeuza Mungu wa Israeli kuwa Mungu wa ulimwengu mzima, na kwa MUNGU WA ISRAELI, HILI NI TAIFA LAKE TEULE.
 
Uchambuzi mzuri.
 
Mi sijasoma ulichoandika,ila nakwambia hivi we kusema sio Taifa teule haiondoi ukweli kuwa ni Taifa teule!
 
Ilikuwa kipindi cha kale. Lakini agano jipya kuua ilikuwa dhambi, hatukuona kabisaa kuna Vita za kuuana zaidi ya wale wasioamini wakiwaua walioamini.

So kwako kupigwa kwa Palestina unaona sawa?
Hivi Israel asingekua na iron dome Yale makombora 1000 ya hamas ambayo yamesharushwa so far ni maafa kiasi gani yangeleta tusipende kuongelea upande mmoja
 
Ilikuwa kipindi cha kale. Lakini agano jipya kuua ilikuwa dhambi, hatukuona kabisaa kuna Vita za kuuana zaidi ya wale wasioamini wakiwaua walioamini.

So kwako kupigwa kwa Palestina unaona sawa?
Sio sawa, ila kuna watu wanawatumja wapalestina kutaka kutimiza malengo yao binafsi.
 
Hivi mnazungumzia Taifa hili la mwaka 1948 au ?

Kama ni hili ushahidi ni upi ?

Je ni upi uhusiano kati ya Uyahudi na Israeli ?
 
"Mimi siamini kama kuna Mungu" hii sentensi itaku-cost
Na ninarudia tena 'siamini kama kuna Mungu' na nimeandika Mungu nikianza na capital later ujue ninammaanisha huyo Mungu wenu mliyekaririshwa na Wazungu na Waarabu lakini pia hata muingu ya asili siiamini pia.
Nasubiri hiyo kuni-cost yako kwa mikono miwili.
 
Hivi mnazungumzia Taifa hili la mwaka 1948 au ?
Hutuaangalii taifa la Israel ambalo lilirudishwa kwenye nchi yake 1948, ila tunangalia chimbuko la taifa hili , Miaka maelfu iliyopita, Ni taifa lilikuwa na utambulisho wa kipekee ndo maana watesi wao waliweza kuwatambua kwa haraka na kuwaangamiza kwenye nchi zao walipokuwa uhamishoni

Uyahudi inatakona na jina la Yuda mtoto mmojawapo wa Israel, linatumika zaidi maana ndo kabila lilikuwa na ukoo wa royal family,Pia ndio walikuwa wamiliki wa mji mkuu wa Israel
 
Ninachojua ndio walio muua yesu.
Wana dini yao ambayo sio kristo.
Wanasujudu kama waislam.
 
Wewe umeongea ukweli mtupu. Na hii comment yako nimeipitisha kama msimamo wa huu uzi kuhusiana na Israel. Case closed.
 
Wapalestina ni Ukoo wa Ismael lakini baba yao mmoja ni Ibrahim
 
Israeli ambae alikuwa ndio Yakobo,alipewa jina la Israeli kwasababu katika magumu yake yote alimtegemea Mungu,Israeli alikuwa na watoto wa kiume 12 ambao ndio makabila yenyewe ya Israeli,ilifikia wakati kuna mgawanyiko ulitokea baada ya mfalme kuwakandamiza raia,makabila ya Yuda na Benjamin yaliendelea kumtii mfalme,makabila haya mawili ndio yalitambulika kama wayahudi,na yale makabila 10 mengine ndio yalitambulika kama wasamaria,ikumbukwe wasamaria walianza kuabudu miungu ya kipagan na hili lilifanya wawe na chuki na wayahudi(Yuda na Benjamin). Lakini walipokuwa wakipewa nchi ya kanaani kuitawala waliambiwa wauwe mataifa flan waliyoyakuta wakiwepo wafilisti ambao ndio wapalestina,kinyume chake waisraeli hawakuwaangamiza wafilisti wote kama walivyoagizwa,na Mungu alikuwa amewaonya mapema kuwa endapo watawaacha hai watakuja kuwasumbua vizazi na vizazi,nafikiri hii vita yao ndio matokeo ya ukaidi wa Israeli kwa Mungu juu ya kuwaacha hai wafilisti.Mwisho kabisa ISRAELI YA SASA SIO TAIFA TEULE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…