Israel inataka kupigana vita na Russia, Russia inaogopa

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,534
Russia ni taifa kubwa hapa Duniani, ina jeshi imara na silaha Kali,kiuchumi Russia haiko vizuri sana,tofauti na Marekani yenye uchumi bora na jeshi zuri.
China imekuja juu sana kiuchumi, imejitahidi sana kuwa na jeshi kubwa na lenye vifaa vya kisasa,tatizo la China ni uzoefu mdogo ktk uwanja wa vita.
Israel ni taifa dogo mno kieneo,ina uchumi wa wastani tu,(neither rich nor poor) ila kijeshi na kijasusi ni hatari mno.
Ili uweze kushinda vita,silaha Kali na jeshi bora havitoshi,bali uwe vizuri pia kijasusi ili uweze kupata taarifa za siri za adui yako ili uweze kumkabili.
Israel ina sifa hizo.
Mwaka 1976,mataifa makubwa kama US,Russia,UK,France, Japan yalikili kuwa "Operation thunder 90 minutes at Entebbe" haikuwa operesheni ya kawaida ,Dunia ilisisimka na kutulia kwa masaa kadhaa,hakuna mtu yoyote aliyefikiri kuwa Israel ingeweza kutuma kikosi cha makomando hatari kwenda kuwakomboa mateka 90 kwa dakika 90.
Wenye chuki na Israel poleni sana,mkubali mkatae Israel si taifa la kispot hata kidogo.
Urusi kila siku inachokozwa na Israel ili iingie vitani lakini Russia inaogopa mno,majeshi ya Russia yapo Syria ili kuilinda Syria lakini kila siku Israel inaipiga Syria.
Unajua kinachotafutwa? Israel inataka Syria ichukie na kisha ishambulie ardhi ya Israel ndipo Israel ipate Sababu ya kuingia vitani kamili.
Ili ipigane indirect na Russia siyo direct.
Si kwamba Russia haina nguvu,la hasha,ila kila Russia akiwaza uwezo wa MOSSAD Duniani, ujasiri wa askari wa Israel na ubora wao,support ya US, inabidi Russia akunje mkia.
Karibuni Pro-Russia na anti-Israel mnipopoe mawe,ila siishi kwenye nyumba ya vioo.
 
Uchambuzi wako bado sana......isreal haiwezi kuingia vitani kwa wakati hu na superpower kama Russia hata marikani haiwezi kuishauri isreal kitendo kama hicho ni "military ignorance" wakati Iran iko standby ku destroye isreal opportunity ikipatikana.......my friend Russia sio Tz au Syria ku declare war kijinga kijinga hivo dunia yote inakua affected.
 
Mkuu huyu kalewa sandwich za Marekani hebu rejea wale Hezbolla 2006 walivyomsumbua muyahudi na hawana silaha za kutosha iweje Russia akisema atupe lile kombora la Satan pale telavivsi mchezo unaishia hapo
 
israel kiboko yake ni hizbollah,,kumbuka mwaka 2006 vifaru vya israel jinsi vilivyochakazwa na makombora ya hizbollah mpaka walikimbilia UN kuomba kusaidiwa kuwatuliza hizbollah,,ile vita iliwagarimu sana israel ..walipoteza wanajeshi wengi sana
 
Kwanza ww unaonyeshea wazi kuwa ni mdogo ktk kufuatilia mambo ya kivita duniani kutokana na hio mada yako ulioitoa, JIULIZE KWA NN MAREKANI HANA MPANGO WA KUIVAMIA SYRIA KIJESHI, USIFANANISHE URUSI NA MAMBO YA KIPUUZI MKUU, MAREKANI MWENYEWE NA ULAYA NZIMA WANAWAJUA WALE WATU, HAO WAYAHUDI WALICHAKAZWA NA WAVAA NDALA TU WAKILEBANONI NA WAZIRI MKUU WA IZRAIL ALIJIUDHULU KUTOKANA NA KICHAPO 2006, MPAKA LEO UNAJUA KUWA KUNA MKATABA WA ILE VITA ILIOTOKEA PALE MWAKA 2006??? ALAF UNAKUJA KUFANANIZA URUSI NA MAMBO YA KIPUUZI
 
Unaipenda mno Israel.

Ila amin nakuambia..ni Russia ndio ilowaokoa Israeli toka mikonon mwa Hitler.

Hata ivo Israeli haiwezi kupigana na Urusi kijeshi maana Urusi ni kitu kinginr kabisa.

ISRAELI INATUMIWA NA DEEP STATE WA US + NATO KWAAJILI YA KUIPROVOKE RUSSIA,ILI WAIDUNDE RUSSIA KWA KUICHANGIA .

kwa ufupi, wanachokitafuta ni kuimaliza Russia +China ili Dunia itawale na wamagharibi.

Hao israeli bila US sio kitu. ,,ndomaana unaona baada ya russia kumpa syria S-300...israeli imekimbilia US kwaajili ya kuomba msaada.
 
Ngoja niweke kiti nijifunze kitu hapa cha wababe wa duniann but kwa utoto wangu wa vita.. Urusi na Israel jamani itakuwa vita ya dunia mjue.. mrusi sio wa spoti spoti hataki kuleta vita ya dunia.. tuacheni haya mambo kutaka wagombane...navyojua mrusi akimgusa muisrael mmarekani ataingilia bi vita tayar ya dunia hiyoo.. tutapata shida wote tu... tusifananishe movie na real war.
 
Sisimizi anaweza muangusha tembo tulia wewe.
Mimi ni kawaida kabisa hiyo siwezi kushangaa Russia akipigwa na Israeli.
We kama huamini mataifa matano ya arabuni yakiongozwa na Misri yaliapa kuifuta Israeli kwenye uso wa dunia mwaka 1967 ila kilichotokea unajua.

Waarabu wakajipanga mwake 1973 "Yom Kippur war" wakarudi tena kulipiza kisasi kipindi hichi wakiwa na silaha bora kabisa toka usovieti lakini wapi mwisho wa siku hostility ikaishia hapo saivi full kuheshimaiana.

Funzo: Ukubwa sio ishu bali mbinu za kivita ndio mpango mzima.
 
Sisimizi anaweza muangusha tembo tulia wewe.
Mimi ni kawaida kabisa hiyo siwezi kushangaa Russia akipigwa na Israeli.
We kama huamini mataifa matano ya arabuni yakiongozwa na Misri yaliapa kuifuta Israeli kwenye uso wa dunia mwaka 1967 ila kilichotokea unajua.

Waarabu wakajipanga mwake 1973 "Yom Kippur war" wakarudi tena kulipiza kisasi kipindi hichi wakiwa na silaha bora kabisa toka usovieti lakini wapi mwisho wa siku hostility ikaishia hapo saivi full kuheshimaiana.

Funzo: Ukubwa sio ishu bali mbiniu za kivita ndio mpango mzima.
Hebu utueleze na ile vita vya mwaka 2006 kati ya Israel na Hezbollah ilikuwaje mkuu....
 
israel kiboko yake ni hizbollah,,kumbuka mwaka 2006 vifaru vya israel jinsi vilivyochakazwa na makombora ya hizbollah mpaka walikimbilia UN kuomba kusaidiwa kuwatuliza hizbollah,,ile vita iliwagarimu sana israel ..walipoteza wanajeshi wengi sana
Hahahahahaha mkuu vifaru vyake vya merkava Ali maarufu kitanda cha Mungu hezbollah walivichakaza balaa muyahudi hana hamu nao
 
Hebu utueleze na ile vita vya mwaka 2006 kati ya Israel na Hezbollah ilikuwaje mkuu....
Mkuu hiyo vita ilikua kavu though naweza kusenga ngoma ni dro ila sasa tukianza kupiga hesabu tutaangaalia watu wangapi wa pande zote walifariki halafu tulinganishe, tuangalie nani kapoteza ardhi na nani kachukua ardhi, tuje kwenye tanks, ndege na silaha zote zilizotumia, uharibifu wa majengo, raia, mali za watu, miundombinu hapo ndipo tutapata majibu nani hasa alipoteza na nani hasa alishinda.

Kwa mfano world war two USSR kashinda ila mimi ninaweza kukubishia kwani hakuna mtu atakaekubali kupoteza watu wake zadi ya million 20 halafu ajisifu hapo napinga mkuu. Unaambiwa kila familia ilipoteza mtu mkuu hapo kuna ushindi hapo?
 
Hahahahahaha mkuu kwa nini usikubali tu ile vita muyahudi alichemka matokeo yake akawa anashambulia mpaka raia wasiokuwa na hatia
 
Back
Top Bottom