CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,304
- 12,999
NIMEICOPY MAHALI
Kijana Joseph ambaye sasa ni marehemu,enzi za uhai wake alibahatika kuwa na kazi nzuri kabla ya kuoa.
Baada ya kuoa miaka mitano ya kwanza akabahatika kuwa na watoto mapacha wa kike na wa kiume na mke wake aliishi kwa furaha akifurahia baraka ambazo Mungu aliwapa familia ile.
Mke hakuwa na kazi na mme akaona ni vyema amsaidie kwa kumsajilia kampuni na mama yule akawa na
kampuni ya mitindo na ikafana sana na kupata umaarufu katika eneo lile.
Miaka michache baadae baadae mme akapatwa na matatizo kazini na kusimamishwa kazi na kwa kuwa
alikuwa daktari basi na leseni yake ya udaktari ikafungiwa na hakutakiwa kufanya kazi yoyote.
Mpango huo ulisukwa na wenzake pale kazini kwa kuwa alisifiwa sana kwa utendaji wa kazi zake na
kupinga vitendo vya rushwa.
Maisha yakazidi kuwa mabaya pale nyumbani kwani miaka ilivyosogea hakupata tena wala kuliona lile
penzi la mkewe, kwani mke akawa ni mtu wa kumchukia mmewe mara mme akihitaji fedha apewe kwa
masimango na mbaya zaidi hata watoto wakaanza kufundishwa na mama yao kumchukia baba yao.
Hali ile ilimpa mzee yule wakati mgumu na ikafikia kipindi akaanza kudhohofika mwili kwa mawazo
ingawa akajitahidi sana kutoyaonesha hayo machoni pa watu na majirani.
Baada ya muda akapatwa na homa na akawa akijiuguza lakini baada ya muda akashauriwa aende akapimwe
na kugundulika kuwa alikuwa na tatizo katika moyo wake lililosababishwa na msongamano wa mawazo.
Akamfuata mkewe ofisini kwake na kumwambia anatatizo la moyo na ilihitajika apate msaada wa fedha
kiasi cha laki tano (500,000) ili afanyiwe upasuaji wa haraka na kujiokoa katika hali hiyo hatarishi kwa maisha yake.
Mke alimjibu, " Sidhani kama nina hela ya kuchezea kwa kukupa mwanaume usiye na faida kwafamilia yako... yaani mpaka chupi
nikununulie mimi?Wanaume wenzako wanafanya kazi na sio kama wewe ulivyo sasa"
Baba alinyanyuka na kuufuata mlango bila ya kusema neno machozi yakimtoka na akikumbuka jinsi
alivyoijenga familia yake kwa upendo na amani akiwapa mahitaji yote na jinsi alivyotumia mpaka tone lake la
mwisho la fedha, muda na hata jasho kuinyanyua biashara ya mkewe ambayo ni kwa ajili ya familia.
Akawasha gari na kuondoka kuelekea nyumbani akiwa na mawazo huku akiona jinsi mtu umpendaye
anayoweza kubadilika kiasi cha kukuombea ufe kwa kuwa ni kero kisa huna kazi na kumfananisha na wale wote.
Huku nyuma mke akaingiwa na roho ya ubinadamu na na kujilaumu kwa kauli ile na kuanza kuumia kisha
akajaribu kumpigia simu mzee ikawa haipokelewi na kumka kuliwasha gari na kuanza kumfuata mzee
Kilomita chache mbele akaona kuna mkusanyiko mkubwa wa watu akapaki gari na kuuliza kuna nini?
wakamwambia kuna ajali ya gari kuna mzee alikuwa anataka kuingia upande wa kushoto bila kuona kama
kuna gari.
Kusogea pale hakuamini kuona mwili wa mme wake ukiwa umefunikwa alianza kutokwa na machozi kabla
ya kuingia kwenye gari na kuona kuna kadi nzuri ikiwa kwenye bahasha akaifungua na kuisoma.
Kilio kikubwa kilimtoka baada ya kugundua kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku za kuzaliwa ya baba huyo na
hakuna aliyekumbuka zaidi ya yeye mzee kununua kadi iliyoandkiwa "
NAKUSHUKURU MUNGU KWA KUNIFIKISHA MWAKA HUU MPYA PAMOJA NA CHANGAMOTO
NINAZOZIPITIA NAAMINI KUNA SOMO WATAKA KUIPA JAMII KUPITIA MIMI. UHIMIDIWE BWANA.. HAPPY BIRTH
DAY TO ME"
Mama yule aliomboleza na mpaka sasa anazidi kuomboleza na hana amani tena hata faida ya ile
biashara haioni tena na hajui nani atamsamehe.
Je, unapitia mapito gani sasa katika mahusiano yako?
Je, unayamudu vipi matatizo ya mahusiano yako?
Je, unafikiria nini kama siku ukiamka na kuona wewe ndio chanzo cha kifo, kilema au chanzo msongamano
wa mawazo kwa mwenza wako kutokana na tabia zako za ubinafsi?
Ndugu una kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kukupa mwenza huyo na kuamini kuwa
katika kila mnalolipitia ni jaribu la kuwafanya muwe na sababu ya kuonyeshana upendo vyema zaidi ya
ule wa mwanzo;
Nimeumia sana mpaka nimefikiria sana mahusiano yangu na watu wanaonizunguka,
kupitia stori hii nimepata somo la upendo na uvumilivu na kuzishinda
stress za dunia.