Isiwe furaha ya muda tuu

Isiwe furaha ya muda tuu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,096
Reaction score
828,932
Niwapongeze mawakili walioenda South Africa kupambana hadi kufanikiwa kuirudisha ndege aina ya airbus mali ya serikali ya Jamhuri? Ya Tanzania.. Nawapongeza sana kwakuwa ni nadra sana kutokea mawakili wetu kushinda kesi za nchi hasa nje ya nchi

Angalizo muhimu kwao:
Wasibweteke wakalewa sifa... Hii fungate ya ushindi isiwe ndefu... Wajipange... Hii ngoma bado mbichi sana... Ndege imerudi lakini deni bado liko pale pale na linazidi kuongezeka kutokana na riba
Bwana stein kadhamiria... Hata kama hatakata rufaa south Africa bado kuna mahakama ya Africa anaweza kukimbilia huko na bado kuna mahakama ya haki za binadamu anaweza kukimbilia huko na kusajili upya kesi yake
Ameshalipwa za kutosha na pengine ameshaona hakuna dalili za kulipwa tena hivyo atakachofanya sasa ni kusumbua na kuharibu taswira ya nchi kimataifa...
Hii inaitwa NIGUSE UNUKE.. unamwaga mboga namwaga ugali...
Kipindi hiki cha fungate zitafutwe mbinu za kumalizana na mzungu kiroho safi ILI maisha yaendelee bila hofu... Hapa Tanzania vinapokamatwa vitu kwenye misako ya polisi watu hutangaziwa kwenda kuvitambua vitu vyao
Akikamatwa jambazi sugu wananchi hutangaziwa kwenda kumtambua...

Nina hofu wadeni wetu wanatafutana na kutengeza group za mawasiliano ILI siku mali yetu ikikamatwa popote watoke kila kona.... Tuna nafasi bado ya kulimaliza hili kabla madhara hayajawa mengi
 
Msiba sialisema, huyo mzungu hana hajanahiyo kesi, mawakili watanzania wenzetu tu, ndio wanatia chumvi kwenye chai.

Hataivyo Tanzania tuna mawakili wasomi wazuritu wenye viwango, kinachotusumbua ni uzalendotu.
 
Umenena vyema mkuu Mshana Jr , tusibweteke tukajiona tumeshinda na kujisahau kuwa deni bado lipo palepale tunadaiwa na dawa ya deni ni kulipa vinginevyo kama ulivyosema hii sherehe itakuwa ya muda mfupi tu na mzungu atatuliza tena .
 
Washauliwe mara ngapi kuwa kunahitajika majasusi wa kiuchumi.. Hawa ndo wataweza kupambana vizuri na kwa uendelevu makini matukio mengine ya kiuchumi yatupasa kuyasikia tu na si mpk hiyo mijizungu itugalagaze mahakamani
 
Msiba sialisema, huyo mzungu hana hajanahiyo kesi, mawakili watanzania wenzetu tu, ndio wanatia chumvi kwenye chai.
Hataivyo Tanzania tuna mawakili wasomi wazuritu wenye viwango, kinachotusumbua ni uzalendotu.
Musiba alidanganya Taifa zima..
 
Huyo mzugu hana ubavu wa kupambana na sisi, wako wengi wanaotudai na mpaka wenyewe kwa wenyewe tunadaiana na hatulipani.Mzungu akawaulize wazee wa EAC wamedai mpaka wakaandamana na kulala barabarani lakini wakaambulia virungu na hakuna aliyethubutu kushitaki,sasa huyo mzungu wa Makuyuni aoneshwe ungangari wetu ili akome.
 
Yap neno lakini Usisahau hata mahakama Za hapa anaweza kuja na kutusulubu hapa hapa,ukizingatia ukumu Za awali alipata point tatu yeye
Ana P. I (prohibited Immigrant) hivyo hawezi kuingia hapa mpaka zuio litenguliwe
 
Msiba sialisema, huyo mzungu hana hajanahiyo kesi, mawakili watanzania wenzetu tu, ndio wanatia chumvi kwenye chai.

Hataivyo Tanzania tuna mawakili wasomi wazuritu wenye viwango, kinachotusumbua ni uzalendotu.
Liwagu..na wewe unamuamini Msiba kabisaa. Mzungu kaburu hajawahi samehe Deni kamwe. Na kwa taratibu za kisheria kesi inafutwa Mahakamani sio kwa kuambiwa Musiba sijui Msiba. Mawakili Ni wawakilishi tu wa mfungua madai wala sio wenye kesi Hivyo hawawezi kuzuia kesi isifutwe japo wanaweza kushauri. Hivyo kesi haijawahi kufutwa kabisa na tulishindwa kwenye Rufaa mwaka 2018. Tutafute namna kulimaliza hili jambo tusisingizie usaliti Wala mbwembwe zingine.
 
Mshana bwana! Kwamba sasa hivi wadeni wetu wanaweza kufungua kundi lao au umoja!
Nimecheka siku wakianzisha group la WhatsApp la Wadai wa TZ au chama Tanzania Debtors Association?
Au club ya kutia stories za machungu yao, Tanzania Wadai Club na hii hata wakandaras wa ndani, waalimu na waganga wote wanaruhusiwa kupata uanachama.
Kinaweza kuwa chama chenye nguvu kuliko CCM
 
Yap neno lakini Usisahau hata mahakama Za hapa anaweza kuja na kutusulubu hapa hapa,ukizingatia ukumu Za awali alipata point tatu yeye
Sijui kama wenye mamlaka watamwacha salama akija Tz kwa jinsi alivyowahenyesha
 
Ana P. I (prohibited Immigrant) hivyo hawezi kuingia hapa mpaka zuio litenguliwe

Hilo ndio atatusumbua nalo. Katika utetezi wetu SA tulisema kesi ilipaswa kufunguliwa TZ. Lakini hapa haturuhusu aingie ili aombe mahakama kuruhusu ashikilie vitu.

Kama mbinu yetu kutolipa deni ilikuwa ni kumfukuza tutakuwa tulikosea sana. Atazunguka na kuharibu taswira ya nchi. Hivi akienda kwa nchi kama US tutachomoka kweli??

Nashauri tumalizane na hili deni kwani itakuwa taabu hata ndege zetu kufanya safari za nje tena. Madeni yataharibu ufanisi wa ATCL.
 
Niwapongeze mawakili walioenda South Africa kupambana hadi kufanikiwa kuirudisha ndege aina ya airbus mali ya serikali ya Jamhuri? Ya Tanzania.. Nawapongeza sana kwakuwa ni nadra sana kutokea mawakili wetu kushinda kesi za nchi hasa nje ya nchi

Angalizo muhimu kwao:
Wasibweteke wakalewa sifa... Hii fungate ya ushindi isiwe ndefu... Wajipange... Hii ngoma bado mbichi sana... Ndege imerudi lakini deni bado liko pale pale na linazidi kuongezeka kutokana na riba
Bwana stein kadhamiria... Hata kama hatakata rufaa south Africa bado kuna mahakama ya Africa anaweza kukimbilia huko na bado kuna mahakama ya haki za binadamu anaweza kukimbilia huko na kusajili upya kesi yake
Ameshalipwa za kutosha na pengine ameshaona hakuna dalili za kulipwa tena hivyo atakachofanya sasa ni kusumbua na kuharibu taswira ya nchi kimataifa...
Hii inaitwa NIGUSE UNUKE.. unamwaga mboga namwaga ugali...
Kipindi hiki cha fungate zitafutwe mbinu za kumalizana na mzungu kiroho safi ILI maisha yaendelee bila hofu... Hapa Tanzania vinapokamatwa vitu kwenye misako ya polisi watu hutangaziwa kwenda kuvitambua vitu vyao
Akikamatwa jambazi sugu wananchi hutangaziwa kwenda kumtambua...

Nina hofu wadeni wetu wanatafutana na kutengeza group za mawasiliano ILI siku mali yetu ikikamatwa popote watoke kila kona.... Tuna nafasi bado ya kulimaliza hili kabla madhara hayajawa mengi
Mawakili wetu walikuwa wasikilizaji tu kazi imefanywa na yule sa. Sidhani kama wakili anaweza kufanya kazi za uwakili katika nchi nyingine bila kuwa registered kule. Pia bado hatujaambiwa ukweli halisi mazingira ya kuachiwa ndege yetu ndio maana tumesitisha safari za huko kwa kisingizio cha vurugu
 
Mshana bwana! Kwamba sasa hivi wadeni wetu wanaweza kufungua kundi lao au umoja!
Nimecheka siku wakianzisha group la WhatsApp la Wadai wa TZ au chama Tanzania Debtors Association?
Au club ya kutia stories za machungu yao, Tanzania Wadai Club na hii hata wakandaras wa ndani, waalimu na waganga wote wanaruhusiwa kupata uanachama.
Kinaweza kuwa chama chenye nguvu kuliko CCM
Group zitafurika wanachama...
 
Back
Top Bottom