Ishushe hiyo mizigo

mxsdk

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,585
2,049
1..Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.
2..Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.
3..Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!
4..Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna. Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.
5..Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii. Huna siri hata moja! Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema "umefulia"
6..Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.
7..Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia "hapa umekosea" kwa sababu ya ujuaji wako.
ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli unahitaji kusonga mbele!..
 
aiseee...! hayo yote yapo kwenye moyo wa mtu mmoja!

mbaya zaidi huyo mtu unakuta ni masikini halafu zaidi zaidi hajionei huruma kumbe ni mlemavu..!
 
Ujumbe murua
10809006_738681342886025_738023514_n.jpg
 
Mimi naishi maishayangu huwa sitaki kufananisha maisha yangu na mtu mwingine
 
1...................

7..Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia "hapa umekosea" kwa sababu ya ujuaji wako.
..........
Watu wa hivi wanaudhi sana.
 
Back
Top Bottom