Grevic Jos
Member
- Aug 29, 2013
- 57
- 2
Mdau hapa naona haiko sawa.
Watu tunahistoria ya kusomeshwa na wazazi wetu kupitia SACCOS kwa mikopo na marejesho ya fedha kidogo kidogo za mama zetu wakaanga vitumbua.
Tumesoma shule za private kwa kuwa ni serikali hii haikutaka kutupangia shule zake kwa kuwa ufaulu wetu ulikuwa ni wa kiwango cha chini.
Hali imeendelea hivyo hadi katika ngazi za diploma, na hii yote ni katika kutafuta sifa linganishi za kutuwezesha kufika huko kwenye vyuo vikuu, na Mungu amesaidia hili.
Sasa serikali ikifikiria sisi kupitia njia mbadala kuwa tuna uwezo inakosea kwani nayo pia ni sababu ya sisi kusomeshwa shule na vyuo hivyo, na si kwamba wazazi wana pesa la hasha; wamekopa sana ktk SACCOS hizi hadi wamepoteza sifa za kukopesheka tena kwa kuwa madeni walionayo ni makubwa mno.
Kwa wale waliopewa wakadisco, bado pia wana haki ya kupata tena siku wakimaliza masomo wakafaulu basi watarejesha madeni.
Ni ukiritimba wa serikari na watu wachache iliowakabidhi hatamu za kuvisimamia vyombo hivi vya fedha.
Kigezo chao ni
1. Kama umeweza kusoma private school secondary then wewe una uwezo wa kujisomesha.
2. Kama umesoma diploma ina maana uwezo wa kujiendeleza unao.
3. Kama walikupa mara ya kwanza uka disco then rejesha kwanza ndo wakupe tena!
Hakya ya MUNGU bodi hawana akili timamu!
Kwa mliopata.ni asilimia ngapi?Cha maana ni kuangalia jinsi gani unaweza songa mbele endapo utakosa mkopo kabisa!
Hiyo sentensi ya mwisho ndo umeongea vizuri, mengine yote ulikuwa unapiga siasa tu mkuu! Maana ukisema huyu kasoma private hivyo hastahili mkopo utakuwa umemwonea, wazazi wengi wanajinyima ili kusomesha watoto huko O na A levels wakitarajia kwamba mtoto akienda university angalau watapumua! Kwa upande wa Diplo pia hawa watu siyo kwamba kusoma kwao Dip ndo wanauwezo wa kujilipia, la hasha! Wengi wetu unakuta vimishahara ndo hivyo tena ni vya nyanya, sasa ukimwacha atakimbilia wapi? ubaya na DCs hazina mafungu ya kusomesha watumishi wake! Watoe mikopo bwanaaaa! Hata hivyo Mimi wa equivalent wamenipa 100% wandugu! ILA BODI HAWANA AKILI AU WAMEJAA UBINAFSI!! Ningekuwa mimi ndo Bodi ningetoa kidogo kidogo kwa kila mtu bila kujali priority courses! 100% ningetoa kwa yatima mwenye uthibitisho! Wengine wote wangelamba 70 au 80%!
Mbona kuna m2 kasoma shule zote za kishua kapigwa 100%