Watu wanasahau tu kuwa hata EL akiingia madarakani allegiance yake ya kwanza itakuwa kwa wale waliomsaidia kuingia madarakani na kusimama naye. Atakuwa na mtandao square. Kitakachokuwa ni marudio ya utawala wa Kikwete na CCM haitakuwa na amani bado. Wenyewe wanasema Lowassa is not a unifying figure but a polarizing one...
Swali lako la msingi lilikuwa is EL relevant? Ukajibu NO. Nilichelea kutoa maoni yangu ili nisije mhukumu EL bila ya hoja inayosimamia kile ninachokiamini, na yanayoendelea Dodoma sasa yananifungua vema.
Kwanza, nakubaliana nawe kuwa ni irrelevant na hata yeye anafahamu hilo.Tatizo la EL ni ile hali wanasaikolojia wanaiita 'state of denial'. Yeye anaamini kuwa amezaliwa kuwa rais hata kama ni wa Burkina Faso, Lesotho au Tonga na fiji ni lazima awe rais.
Nyerere alipomkataa alidhani ni mtu mmoja na hata watu milioni 30 wanapomkataa bado hatambui hilo! 'state of denial'.
Kwamba anaweza kuwa rais wa nchi hii hilo ni irrelevant, lakini kuna kitu relevant kuhusu EL ambacho hatukipi uzito. EL ame-determine kuwa rais, ni dtermination hiyo ndiyo iliyomfanya akatumia mapesa kuunda mtandao ili muda ukifika naye afike kileleni. Akawa PM na kujitahidi kununua watu wake kwa pesa alizozishuku Nyerere.
Akiwa PM akawa anafanya mambo kwa 'show off' kitu lkilichompatia sifa ya utendaji na ufuatiliaji. Ukweli unabaki pale pale kuwa hakuwa na utendaji wowote zaidi ya kuita wakuu wa wilaya , waganga wa vituo vya afya na walimu kujibu maswali hadharani.
Ni EL aliyekuwa kichaka cha akina RA na wenzake na hana historia ya kutetea masilahi ya umma.
Baada ya anguko kama PM kwa jaziba akijua linafungua njia ya kurudi magomeni na si Magogoni, EL hakukata tamaa. Ni mtu aliye determine na ghafla akajikita kwenye kupanga vijana UVCCM. Akarejea ngazi ya mkoa na kutaka kuwaweka akina Matilda ili kuendeleza mtandao.
Hilo nalo linaonekana kuwa gumu kama tunavyoshuhudia vugu vugu la Arusha hasa UVCCM.
Kashfa ya Richomnd ndiyo inamtia wazimu kufikia ndoto zake. Na kwa hilo anaona yeye ni loser and he has nothing to lose.
Akili yake inamtuma kuwa yeye kazaliwa kuwa Rais na ndiyo maana tunaona kageukia viongozi wa dini zote ili kutafuta pa kutokea. Tunamuona akijihusisha na shugHuli za kuzindua kwaya n.k.
Dodoma ndiko kunaonekana kungehitimisha safari yake na kwa vile ame-determine basi ameamua liwalo na liwe muhimu ni kuwa rais.
Tunaona alivyomuumbua mshirika wake kwa kumtaja katika sakata la Richomnd. Ni JK aliyewahi kusema hajui lolote kuhusu hao akina Richmond na Dowan( hata kutungiwa shairi, sijui mimi sijui'.)
Rekodi zinaonyesha aliwahi kusema hakuna mchezo mbaya Richmond.
Kama angeyasema ya leo ndani ya bunge akiwa PM tungemuelewa, kwa vile ameamua kufa na tai basi akae kimya.
Kitendo cha kumuumbua JK ni ushahidi kuwa EL ame-determine kutumia mbinu yoyote kuwa rais hata kama ni kuliangamiza taifa. Hapa ndipo ninasema bado ni relevant, kwani watu wanaweza kufyekana ili mradi tu yeye awe Rais.
Hata yeye kuungwa mkono na Sumaye ni ushirika wa kikabila kama alivyowahi kusema Ole Naiko kuwa wamasai wanaandamwa. Tunajua si mmasai lakini EL anaweza kuwa Mbondei au Msambaa endapo tu hilo litamhakikishia urais.
EL ana historia chafu sana isiyomruhusu kuwa hata mwenyekiti wa mtaa, bado anaamini kuwa anaweza kuwa rais.
Tatizo ninaloliona na linalonitisha ni jinsi EL anavyoweza kutumia mbinu chafu kuliangamiza taifa ili wae rais.
Kamnukuu JK akiwa Zbar kuwa' ...urais ni majaliwa ya mungu' akionyesha nia yake ya kuwa rais licha ya uchafu alionao .
Hii ni state of denial inayoweza kulivuruga taifa.
Na muhimu zaidi ni kuwa ameweza kuzuia NEC isimtie adabu, ushawishi wa nguvu aliyo nayo ndani ya chama.
Ukiongezea na determination yake huyu si mtu wa kupuuza. Anaweza asiwe rais wa halali lakini akawa rais kwa damu za wanadamu. Huyu ndiye ENL