IRINGA: Watatu wafariki katika ajali ya basi la Ngasamo Express

IRINGA: Watatu wafariki katika ajali ya basi la Ngasamo Express

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
HABARI MPASUKO:

Ajali nyingine Iringa, Basi la Ngasamo Express limepata ajali leo na kwa mujibu wa taarifa za awali watu watatu wafariki papo hapo.

Cy-YZQUWgAEJ7eQ.jpg


Cy-YZQVXUAEtDSe.jpg

======
UPDATE: 12:02 PM

BAADA ya ajali iliyotokea jana majira ya saa 11.45 jioni eneo la Tanangozi kwa lori kuligonga gari dogo aina ya Hiace iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya stendi kuu ya Iringa mjini na Ulete na kusababisha vifo vya watu 9 papo hapo na wengine 18 kujeruhiwa ,ajali nyingine imetokea majira ya saa 5 usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinyanambo C mjini Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani hapa kwa basi la kampuni ya Ngasamo Express kuacha njia na kupinduka na kupelekea abiria watatu kufa papo hapo na wengine 13 kujeruhiwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (RPC)Julius Mjengi amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo lililokuwa likitoka Mwanza kuelekea Mbeya kushindwa kulimudu gari hilo hivyo kupelekea gari hilo kuhama njia na kupinduka.

Alisema kuwa basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Amos Yoyo na kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi iliyopo mjini Mafinga na miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti Hospitalini hapo.

Chanzo: Clouds Media Live
 
Kama kawaida.mwisho wa mwaka huu.
Watu wanataka wafunge hesabu.mwakani waanze upya
 
Hilo bas ni la musukuma na wasukuma sio watu wazur wanatoa ndagu sana bado na super shem ndo wasukuma hao hao
 
Si ajabu huyo dreva katoka na hiyo gari Mwanza hadi eneo la ajali, hakuna kupokezana, dreva mmoja anatoa gari Mwanza hadi Mbeya halafu hawalali njiani anataka apusue afike siku hiyo hiyo
 
Hilo bas ni la musukuma na wasukuma sio watu wazur wanatoa ndagu sana bado na super shem ndo wasukuma hao hao
Ajali zote z mabasi zinazosababisha vimo wamiliki wa mabasi hayo yote ni wasukuma?
 
Eeh Mungu tuepushe na ajali hizi bila wewe hatuwezi vifaa vyote vimeumbwa kwa mikono dhaifu ya mwanadamu.
 
Back
Top Bottom