Iringa: RC Hapi, aibua madudu mazito tarafa ya Malangali

Iringa: RC Hapi, aibua madudu mazito tarafa ya Malangali

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
RC HAPI AIBUA MADUDU MAZITO TARAFA YA MALANGALI

Aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi kituo cha afya malangali

Ni baada ya gharama zake kutoendana na thamani ya majengo

Ikiwa leo ni siku ya pili tangu kuanza ziara yake mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ametembelea miradi mbalimbali katika tarafa ya Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi.

Katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa ameweza kuweka jiwe la msingi mradi wa maji Bumilayinga wenye thamani ya shilingi milioni 320 na unahudumia zaidi ya wanachi 1637.
i
RC Hapi ametembelea mradi wa vyoo na maji safi katika shule ya msingi Ihowanza, Ilangamoto na Ugenza ambapo visima 3 vimechimbwa na ujenzi wa matundu 23 ya vyoo pamoja na usambazaji wa mabomba ya maji ya mita 1,816 katika shule hizo na vijiji vya jirani.

Wakati wa ziara yake katika tarafa hiyo alifanya ukaguzi katika majengo ya kituo cha afya cha Malangali mbayo ni pamoja na jengo la maabara, nyumba moja ya mtumishi pamoja na maabara ya kisasa ambapo hakuridhishwa na gharama zilizotumika katika ujenzi huo uliotumia FORCE ACCOUNT. Ujenzi wa baadhi ya majengo na ukarabati wa majengo mengine unatajwa kutumia zaidi ya milioni 400 huku nguvu za wananchi zikiwa pia zimetumika kuchangia zaidi ya matofali 64,000, mchanga na mawe.
Mhandisi wa halmashauri ya Mufindi alishindwa kutoa ufafanuzi wa gharama kubwa zilizotumika kwa baadhi ya majengo zisizoendana na thamani ya fedha.
Baada ya kutoridhishwa na majibu ya muhandisi huyo, RC Hapi amemuamuru mkuu wa TAKUKURU Iringa, Aidan Ndomba kuchunguza suala hilo na kujiridhisha kama hakuna pesa ya serikali iliyotafunwa.

Pia mkuu huyo wa mkoa ametembelea na kukagua ukarabati wa majengo ya madarasa, maabara na mabweni katika shule ya sekondari ya wavulana ya Malangali ambayo yamekarabatiwa na wakala wa majengo wa serikali TBA na kupongeza juhudi hizo.

Ally Hapi amemalizia siku ya pili ya ziara yake katika kata hiyo kwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya sekondari ya Malangali kwa kusikiliza kero za wananchi.
IMG-20180910-WA0034.jpg
IMG-20180910-WA0032.jpg
 
Yote hayo ni ccm tu alafu .....wanakamatana wenyewe
 
Hongera sana mheshimiwa RC kwa kutembelea sehemu za ndani (vijijini) kabisa katika mkoa na kuibua madudu yanayofanyika huko ambako wapigaji wanahisi kutoonekana. Binafsi nampongeza kwa kufika kijijini Malangali maana nilisoma sekondari hiyo na kwa miaka yote minne niliyosoma pale sikuwahi kuona RC au DC akifika kijijini hapo hivyo naamini hata wananchi watakuwa wamefurahi mno kutembelewa na kiongozi wao wa mkoa, ni aina fulani ya historia ameiandika.
Hata hivyo hao TAKUKURU mkoa wa Iringa ni wazembe mno kuchukua hatua hata pale wanapopelekewa tuhuma zinazojitosheleza kabisa. Labda hili kwa kuwa ni agizo la RC huenda wakalifanyia kazi!
Kwa mara nyingine nampa hongera sana mheshimiwa Ally Hapi kwa kuwafikia wananchi hukohuko walipo!!
 
Ujinga wa kijinga...hajaridhishwa maana yake nini? Yeye ni mtaalam majengo mkaguzi?

Hizi siasa za kijinga mziache.
 
Back
Top Bottom