figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Hali ya Simanzi imetawala katika kijiji cha mibikimitali kilichopo katika tarafa ya kiponzelo kikiwa umbali wa kilomita zaidi ya sabini tokea Iringa mjini.
Radi hiyo imepiga katika shule ya msingi mibiki mitali na kuua mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la Goodlove Luhaga mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la 4 amefariki papo hapo baada ya radi kumpiga akiwa amekaa na wenzake 4 ambao ni majeruhi.
Mungine aliye fariki katika ajali hiyo ni binti amabaye ametambulika kwa jina moja tu la Kulwa ambaye ni mtumishi wa ndani wa Mwalimu Mkongwa aliye kuwa akichota maji na kufariki papo hapo.
Mpaka sasa majeruhi wanne ambao ni Noah Mdota miaka 12 aliyeungua paji la uso, Firida Kibiki miaka 13, Zela Chaula miaka 13 na Recho Mdemu miaka 10 ,Majerhi wote wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Iringa kwa matibabu na uangalizi wa karibu.
Akiongea kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richald Kasesela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo “ Majira ya saa tisa hivi leo nimepokea taarifa hizo na nimebahatika kufika eneo la tukio ni kweli radi hiyo imepiga na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo pamoja na majeruhi, nime waomba wakazi wa mibikimitali kuwa na moyo wa subira pamoja na kuwa watulivu hasa katika kipindi hiki kigumu”.
Radi hiyo ilipiga muda wa saa 9 mchana ambapo watoto walikuwa wakijiandaa kurudi nyumbani.