PreGE2025 Iringa: Issa Gavu azindua mradi wa maduka ya CCM Stendi Kuu ya zamani

PreGE2025 Iringa: Issa Gavu azindua mradi wa maduka ya CCM Stendi Kuu ya zamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
341
Reaction score
476
Katibu wa NEC organaizesheni na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Issa Gavu amezindua mradi wa Maduka ya chama Cha mapinduzi yaliopo stendi kuu ya Zamani huku akiwaasa wanachama pamoja na wafabiashara kuitunza milango (flemu) hizo.

Akizungumza wakati wa Kuzindua na kuweka jiwe la msingi flemu hizo Issa Gavu ambae ni Katibu wa NEC organaizesheni wa Kamati kuu ya CCM amesema mradi huo ni mkubwa hivyo ni wajibu wa Kila mwanachama kuitunza na kuilinda.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mradi huu ni mkubwa wote tunajua kuwa uchumi ni siasa na siasa ni uchumi hivyo ni vema chama Cha mapinduzi CCM kikawa na Miradi mizuri na yenye Tija Ili kusaidia chama na jamii. "Alisema Gavu"

Kwa upande wake Katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM tawi la stendi kuu Bi. Paulina Senyota amesema kamati ilikusanya jumla ya Shilingi milioni 178 kwa ajili ya ujenzi wa flemu 22 na ujenzi huo ulianza mwezi Mei 2023 na umekamilika mwezi machi 2025.

 
This is too much! Maeneo ya serikali mnayapora kinyemela na kujimilikisha kama ya kwenu mchana kweupe! Viwanja vya michezo navyo mnajifanya eti navyo ni vya kwenu! Majengo ya serikali mnageuza kuwa ofisi zenu!!

I wish ningekuwa Rais wa hii nchi! Hakika ningewafilisi na kuwanyang'anya mali zote mlizopora tangu mwaka 1977!
 
Back
Top Bottom