Iringa hongereni kwa Usafi

Hardlife

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2021
Posts
2,760
Reaction score
6,320
Habari.

Binafsi sijawahi kufika Iringa mjini zaidi ya kupita tu kule Ipogoro nikienda au kutoka Mbeya.

Sasa nimekuja kikazi hapa Iringa mjini. Kilicho nishangaza ni jinsi mji ulivyo msafi na pia nilijua ni mji wa hovyo kumbe sio kabisa

Kwangu mimi kipimo cha usafi kwenye mji huwa ni sokoni maana kuna shughuli nyingi ambazo husababisha kuchafuka kwa mazingira. Kwa hapa Iringa nimefika Sokoni sijaona hata chembe ya uchafu.

Hongereni sana wahusika wa utanzaji wa Mazingira IRINGA.
 
Asante, Karibu Iftari jioni kwa Mama Solemba.
 
Nimepata hapo kwa BABA NUSA
 
Kwangu mimi kipimo cha usafi kwenye mji huwa ni sokoni maana kuna shughuli nyingi ambazo husababisha kuchafuka kwa mazingira. Kwa hapa Iringa nimefika Sokoni sijaona hata chembe ya uchafu.

Hongereni sana wahusika wa utanzaji wa Mazingira IRINGA.
Nenda Mlandege makaburini ndiyo utajua hao unaowasifia wakoje
  • Wamegeuza makaburi ndiyo dampo ya kutupa taka
  • Wamegeuza makaburi ndiyo kwa kuweka matangazo ya waganga wa dawa za mapenzi
  • Wamegeuza makaburi ndiyo sehemu ya kujisaidia haja kubwa na ndogo
  • Wengine hufanya ndiyo sehemu za kumaliziana matamanio yao
  • Kuna mengi hayako sawa hapo
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…