Iringa: Bar na Grocery zimepoa, Migahawani Ugali umeshapikwa Saa mbili Asubuhi

Ha ha ha nakweli majuzi nlikua napita apo iringa nkitokea songea nlishangaa kuona satatu asubuhi ugali ukipikwa badala ya chai....
 
Wasalaam,

Katika Uchunguzi ambao nimeufanya hapa kwetu kuanzia mwezi wa Kwanza, Vijiwe vingi (Bar na Grocery pamoja na 'sebule' za starehe vimepoa na havina watu kabisa si kama zamani. Kwa mfano katika kijiwe changu cha C2C BAR na IN BOX nilikuwa nikifika tu mida ya 2:00 usiku hakuna mahali pakukaa wateja wamejaa mpaka wengine tunaishia nje. Lakini ni tofauti hawatujahi kama zamani mtu ananua zake moja anaondoka.

Na kwa Upande wa migahawani sasa ni tofauti Chai haipikwi sana kama zamani. Saa mbili asubuhi ukipita vibanda vya CCM Ugali umeshaiva na ikifika saa 4 Umeshaisha na kuanza kupikwa mwingine.

Vipi hali ya vijiwe huko mtaani kwenu.
tupo kwa cachella wambali mkuu,njoo utatukuta...jioni tumehamia kwa kibangali pale kwake kaleta watoto wa singida,tunapaita KIBANGA AMPIGA MKOLONI...karibu tujumuike.
 
Na bado hizo vitz na passo mtazipark na kuhamia kwenye bodaboda TVS HLX
Masela kibao wanauza hivyo visafirio. Utasikia jamaa anavunga oooh! Bi mkubwa kijijini anaumwa hivyo hakuna namna.
Mwingine ooh! Nilitaka kubadilisha ila ngoja niongeze pesa kidogo nipate model na aina mpya. Ukimfuata baada ya mwezi utasikia anasema aah? Subiri upepo wa magufuli ukae sawa.
 
Wasalaam,

Katika Uchunguzi ambao nimeufanya hapa kwetu kuanzia mwezi wa Kwanza, Vijiwe vingi (Bar na Grocery pamoja na 'sebule' za starehe vimepoa na havina watu kabisa si kama zamani. Kwa mfano katika kijiwe changu cha C2C BAR na IN BOX nilikuwa nikifika tu mida ya 2:00 usiku hakuna mahali pakukaa wateja wamejaa mpaka wengine tunaishia nje. Lakini ni tofauti hawatujahi kama zamani mtu ananua zake moja anaondoka.

Na kwa Upande wa migahawani sasa ni tofauti Chai haipikwi sana kama zamani. Saa mbili asubuhi ukipita vibanda vya CCM Ugali umeshaiva na ikifika saa 4 Umeshaisha na kuanza kupikwa mwingine.

Vipi hali ya vijiwe huko mtaani kwenu.
Ebu jaribu kufanya utafiti,nini kimesababisha khali hiyo.
 
Hujasema sababu ni nini??!!Vile vibanda vya CCM, kwa Joyce na wenzake pakoje sasa, maana nimefika siku nyingi pale...kulikuwa na supu safi ya kuku saa za jioni kuanzia saa 12.30 jioni...nilikaa hapo Iringa wiki moja hivi...
 
Sababu kubwa Mifuko ya wengi imetoboka...

Kwa dada joy bado panaendelea supu za kuku kama kawaida..
 
Aaaah, safi, nitafika Iringa miezi michache ijayo, Mungu akipenda...suala la mifuko 'kutoboka' siyo la Iringa tu, mahali pengi ndivyo hali ilivyo...Dar es salaam, wanaisoma namba pia, mbege inaanza kupata soko maeneo ya Kimara, Mbezi na kadhalika...ila nimesikia wanywa mbege wakilalamika kuwa kuna 'viroba' vinawekwa kwenye mbege, duh, kama ni kweli hii ni hatari sana...Nyie wa Iringa piganieni ULANZI upate soko kubwa kubwa...
 
Hah..hah..Ulanzi Umeshaisha...sasa ni msimu wa MACHICHA..
 
Tabia ya Iringa inapofunguliwa Bar mpya watu wanajaa sana baada ya muda wanaanza kurudi sebuleni kwao MIAMI, STEREO, +255 na VIP. Utakua ulienda kipindi zinafunguliwa hizo C2C na Inbox. Pale C2C sio pa kijanja sana sijui hua napaonaje
 
Back
Top Bottom