Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,776
Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kushiriki kwake katika kampeni za siasa wakati akifanya harakati za kutaka kuingia bungeni kumempatia ujasiri mkubwa katika maisha yake.
Katika uchaguzi wa mwaka 2015, muigizaji huyo alijitosa kwenye siasa na kuchukua fomu ya ubunge viti maalum Tabora lakini akakosa.
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Irene Uwoya amesema kwa sasa anajipanga tena kwa kipindi kijacho, kwani tayari ameshatambua njia zote.
“Sijajisikia vibaya, mimi sio mwanasiasa nilijaribu na natumaini wakati ujao nitayaribu tena,” alisema Irene.”Lakini kusema kweli kuna vitu ngingi nimejifunza, nimejifunza kuwa strong,”