Pole sana hii mitandao ya simu ni balaa
Mi kuna siku nilikuwa nampigia boy flan kwa namba ya tigo
Nikawa nijibiwa na wimbo
"Usilie dadaa ,nenda zako dada"
Nilikereka sana ila mpe muda Irene atakuelewa tu
Ha ha haaa!umemwandikia irene au sisi?...loading error...
"Uliapo sitokufuta chozi, bali nitalia nawe,
Sitokukataza uondokapo laaziz, nitaondoka nawe,
Sitokudaka uangukapo mpenzi, nitaanguka nawe,
Nitakutunuku hata yangu pumzi, nife mimi uishi wewe"
Haya ni maneno yako Irene. Uliniambia kwa kinywa chako mpenz wangu ni vipi leo umeyasahau? Mbona leo unanitelekeza Irene?
Natambua kuwa jana ulinihitaji sana. Ulihitaji angalau kupata ujumbe wa huba kutoka kwangu, ulihitaji faraja kutoka kwangu, ulinihitaji mimi, ila kati ya yote hayo hakuna nililolifanya, niliurarua moyo wako.
Irene barafu wa mtima wangu, sikukusudia kufanya hilo ila voda ndio tatizo. Muda wote simu yangu iliandika "emergency call". Nilishindwa kuwasiliana nawe mke wangu sababu ya voda. Message zote thelathini ulizonitumia zimefika leo asubuhi, message ya mwisho uliandika, "Asante mpenzi, umenitenda sana... endelea na maisha yako"
Aah Voda mmeniharibia ndoa tarajiwa na nasema hivi leo nawahama!!! nahamia Airtell! NAWAHAMA VODA MMENIKWAZA SANA.. NDOA TARAJIWA IPO SHAKANI!!! VODA! VODA! AARRGH
tena bora uwashukuru voda , wamekuepushia mwanamke mzigo hasiye na maamuzi changanuzi
huyo alikutafutia sababu mda mrefu sana, kwa yaliyokukuta mwanamke mwenye akili ya kujiongeza hasingefanya maamuzi ya kipuuzi kama hayo
shukuru Mungu kijana, kama umempa sababu ,ukaomba msamaha na akashindwa kukuelewa
mpe bye bye
Pole sana hii mitandao ya simu ni balaa
Mi kuna siku nilikuwa nampigia boy flan kwa namba ya tigo
Nikawa nijibiwa na wimbo
"Usilie dadaa ,nenda zako dada"
Nilikereka sana ila mpe muda Irene atakuelewa tu
Tigo? Upo bongo?
unajua waafrika ndivyo tulivyo angekuwa mwanamke wa ulaya au marekani angepata tabu leo hii angedamkia kwako kukujulia hali labda umezidiwa usiku ndio maana ukashindwa kujibu sms zake. usiku mrefu ila hawa dada wa afrika muda wote wanawaza kusalitiwa aaghh. WAAFRIKA TUBADILIKE
Kweli kabisa, yaani badala ya kuniuliza nimepatwa na tatizo gani yeye anasema niendelee na maisha yangu
so nami natakiwa nireplace?