Irene Mpenzi, Kosa si langu ni la Voda

Irene Mpenzi, Kosa si langu ni la Voda

dawa yenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
2,833
Reaction score
3,751
"Uliapo sitokufuta chozi, bali nitalia nawe,
Sitokukataza uondokapo laaziz, nitaondoka nawe,
Sitokudaka uangukapo mpenzi, nitaanguka nawe,
Nitakutunuku hata yangu pumzi, nife mimi uishi wewe"

Haya ni maneno yako Irene. Uliniambia kwa kinywa chako mpenz wangu ni vipi leo umeyasahau? Mbona leo unanitelekeza Irene?

Natambua kuwa jana ulinihitaji sana. Ulihitaji angalau kupata ujumbe wa huba kutoka kwangu, ulihitaji faraja kutoka kwangu, ulinihitaji mimi, ila kati ya yote hayo hakuna nililolifanya, niliurarua moyo wako.

Irene barafu wa mtima wangu, sikukusudia kufanya hilo ila voda ndio tatizo. Muda wote simu yangu iliandika "emergency call". Nilishindwa kuwasiliana nawe mke wangu sababu ya voda. Message zote thelathini ulizonitumia zimefika leo asubuhi, message ya mwisho uliandika, "Asante mpenzi, umenitenda sana... endelea na maisha yako"
Aah Voda mmeniharibia ndoa tarajiwa na nasema hivi leo nawahama!!! nahamia Airtell! NAWAHAMA VODA MMENIKWAZA SANA.. NDOA TARAJIWA IPO SHAKANI!!! VODA! VODA! AARRGH
 
ahahahah
yani u made my asubuhi..lol
 
tukushauri au unatupa taarifa?!
 
Pole sana hii mitandao ya simu ni balaa
Mi kuna siku nilikuwa nampigia boy flan kwa namba ya tigo

Nikawa nijibiwa na wimbo

"Usilie dadaa ,nenda zako dada"
Nilikereka sana ila mpe muda Irene atakuelewa tu
 
Mmmnh... Yaani hiyo ndio sababu ya kukuacha???? Mbona ni vitu vidogo saana..!!
 
Pole sana hii mitandao ya simu ni balaa
Mi kuna siku nilikuwa nampigia boy flan kwa namba ya tigo

Nikawa nijibiwa na wimbo

"Usilie dadaa ,nenda zako dada"
Nilikereka sana ila mpe muda Irene atakuelewa tu

Tigo? Upo bongo?
 
"Uliapo sitokufuta chozi, bali nitalia nawe,
Sitokukataza uondokapo laaziz, nitaondoka nawe,
Sitokudaka uangukapo mpenzi, nitaanguka nawe,
Nitakutunuku hata yangu pumzi, nife mimi uishi wewe"

Haya ni maneno yako Irene. Uliniambia kwa kinywa chako mpenz wangu ni vipi leo umeyasahau? Mbona leo unanitelekeza Irene?

Natambua kuwa jana ulinihitaji sana. Ulihitaji angalau kupata ujumbe wa huba kutoka kwangu, ulihitaji faraja kutoka kwangu, ulinihitaji mimi, ila kati ya yote hayo hakuna nililolifanya, niliurarua moyo wako.

Irene barafu wa mtima wangu, sikukusudia kufanya hilo ila voda ndio tatizo. Muda wote simu yangu iliandika "emergency call". Nilishindwa kuwasiliana nawe mke wangu sababu ya voda. Message zote thelathini ulizonitumia zimefika leo asubuhi, message ya mwisho uliandika, "Asante mpenzi, umenitenda sana... endelea na maisha yako"
Aah Voda mmeniharibia ndoa tarajiwa na nasema hivi leo nawahama!!! nahamia Airtell! NAWAHAMA VODA MMENIKWAZA SANA.. NDOA TARAJIWA IPO SHAKANI!!! VODA! VODA! AARRGH

"MAHABA niue Mnakazi"...Good luck...
 
pole sana mkuu na airtel wakikufanyia hivyo utahamia mtandao upi?
mfuate aliko irene mkayamalize yanazungumzika hayo.
 
Back
Top Bottom