Zurie
Platinum Member
- Jul 6, 2014
- 2,089
- 5,964
Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi ametangaza operesheni kubwa ya kijeshi ya kuukomboa mji wa Fallujah kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State lililouteka mji huo miaka miwili iliyopita.
Akiwa ameandamana na maafisa wakuu wa jeshi, Bw al-Abadi alitoa tangazo hilo moja kwa moja kupitia televisheni na kusema bendera ya Iraq karibuni itapepea katika mji wa Fallujah uliopo takribani maili 40 Magharibi mwa Baghdad.
Maafisa wa serikali awali walikuwa wamewatahadharisha maelfu ya raia ambao bado wamo katika mji huo, wengi wao jamaa za wapiganaji wa IS, kuuhama mji huo.
Licha ya kukabiliwa vikali, wapiganaji wa IS bado hudhibiti maeneo makubwa kaskazini na magharibi mwa Iraq, ukiwemo mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Mosul.