Hao Iran kila mwaka porojo zao ni hizo hizo. Ikija kwenye uhalisia, inatandikwa mpaka chumbani bila hata ya kujitambua, inarusharusha tu makombora, huku mengi yakipotelea porini bila habari. Mwakajana tu hapo, Iran imepata kipigo cha aibu kubwa: makamanda wake wakuu, wanasayansi mashuguli, karibia wote wakauawa. Vituo vyake vyote vya nuklia vikibondwa! Yaani vituo vya nuklia havina hata ulinzi wa kuaminika!
Fikiria unaingia vitani na hasimu wako, wewe unapoteza watu zaidi ya 1,000, tena wakiwemo makamanda wakuu, halafu wewe unaua raia 27 na askari aliyekuwa likizo 1 wa adui yako!! Hiyo inaonesha ninyi uwezo wenu umetofautiana sana, kama ingekuwa ni mpira, basi mwingine yupo kwenye mechi za mchangani, mwingine yupo ligi kuu.
Iran ikiingia tu vitani na USA, vifo vya askari wa Iran vs USA itakuwa ni 1,000 :
Ikiwa Iran itafanya kosa ikaishambulia Israel, itakuwa ndiyo mwisho wa Ayatollah. Mwakajana lilikiwa ni ombi la USA, wasimmalize Ayatollah. Lakini USA ikitoa go ahead kwa Israel kummaliza Ayatollah, atakuwa na nafasi ndogo sana ya ku-survive. Fikiria makamanda wa Iran, Hamas, Hezbollah waliv ulivyokuwa wakidonolewa mmoja baada ya mwingine.
Nafasi pekee ya Ayatollah ilikuwa ni kuwa na mshikamano na wananchi, lakini kwa sasa Ayatollah kwa Iran, mazingira dhidi ya wananchi wake, hayana tofauti na samuya. Wananchi hawamtaki.