Massenberg
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 1,173
- 1,373
Duniani kote kuna Watanzania wa aina mbili tu - wale wanaoamini CCM itashindwa katika uchaguzi mkuu wa 2015 na wale wanaoamini kuwa itashinda. Kila kundi lina orodha ya sababu zake, lakini ipo sababu moja yenye pande mbili ambayo haimo katika orodha za wengi walio katika kundi linaloamini CCM itashinda. Pande mbili za sababu yenyewe ni hizi:
MAREKANI NA MCC YAO:
Wote tunakumbuka Februari 2008 wakati rais wa wakati ule wa Marekani George Bush alipofanya ziara hapa nchini. Moja ya mambo aliyokuja kuyafanya ni kutia saini makubaliano baina ya nchi hizi mbili ambayo yalilenga kuipatia Tanzania mamilioni ya dola chini ya mpango ujulikanao kama Millennium Challenge Account (MCC). Kama ni mfuatiliaji wa masuala ya siasa za nje za Marekani utagundua kuwa mara zote huwa misaada yao inazingatia vigezo vingi ukiwemo utawala bora, vita dhidi ya rushwa, haki za binadamu, n.k.
Kwa vigezo hivyo ni vigumu kuamini kuwa Tanzania ilifaulu mtihani huo na hivyo kustahili fedha zile; sote tunajua namna ambavyo nchi yetu ilivyo kwenye maeneo haya.
MCC ilijumuisha makubaliano mengi tu yaliyohitaji kutiwa saini, na mpango huu haukuanzia wakati wa serikali ya awamu ya nne, ulianza tangu enzi za Mkapa. Tofauti ni kwamba Mkapa hakutia saini kirahisi makubaliano hayo, na Wamarekani hawakusumbua kichwa, wakasubiri rais atakayefuata. Huyu haikuwa kazi kubwa kumaliza naye mchezo na matokeo yake ni kwamba kama malipo ya mamilioni yale ni kama nchi wameuziwa Wamarekani.
Hitaji kubwa la Marekani ni nishati na hii inapatikana kiurahisi maeneo ya kusini mwa nchi hii. Kutokana na umuhimu na unyeti wa makubaliano haya, Wamarekani wanafanya kila juhudi kuhakikisha serikali inayoendelea kuwepo madarakani ni ya CCM ili ilinde matakwa yao. Wanafahamu kuwa ikija serikali tofauti itarudisha rasilimali hizi mikononi mwa nchi na hivyo kuharibu maslahi yao.
IRAN NA URANIUM YETU:
Tanzania si nchi ya kiislamu, lakini ni nchi yenye uhusiano mzuri na nchi za kiislamu. Iran ni mojawapo ya mihimili ya nchi hizi na ni rafiki wa siku nyingi wa Tanzania. Ulimwengu wote unafahamu kuwa Iran inaendesha program ya nyuklia ambayo wao wanadai ni kwa matumizi ya nishati wakati Wamarekani wanasema ni kwa ajili ya silaha za nyuklia.
Ili silaha hizi zitengenezwe yanahitajika madini ya uranium. Barani Afrika yanapatikana Niger, Tanzania, na pengine DRC (kama sikosei); uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Iran ni mwanya kwa Iran kupata madini haya kutoka hapa kama ambavyo tunafahamu maswahiba hugawana vitu vitamu.
Marekani inalijua hili na kwa haraka wamefanya juhudi kuhakikisha wanawahi kabla Iran haijaweka mikono yake.
Kama namna ambavyo Marekani ilipigana vita baridi na Urusi kwenye ardhi za nchi zingine kama Angola, Ulaya Mashariki na Amerika ya Kati, vita yao ya kimaslahi dhidi ya Iran pia inapiganwa kwenye ardhi zingine ingawa si kwa silaha. Marekani haitaki Iran iwe na silaha za nyuklia.
Hivyo basi, kwa maslahi yao binafsi, Wamarekani hawatakuwa tayari upinzani ushike nchi mwaka 2015.