Iran kuzindua mfumo mpya wa makombora wa 'Joshan' ni laser weapon pia

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,036
17,997
Jeshi la Iran kuzindua mfumo mpya wa makombora wa 'Joshan'

Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mfumo mpya wa makombora wa Joshan utaanza kufanya kazi kabla ya kumalizika mwaka huu wa Kiirani.

Brigedia Jenerali Ali Reza Elhami alisema hayo jana Jumamosi na kuongeza kuwa, mfumo huo erevu, wa kisasa na unaotumia mifumo ya kisasa ya sayansi kama 'quantum' na 'laser' utazinduliwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa Kiirani ulioanza Machi 21, 2021.

Amebainisha kuwa, uwezo mkubwa wa kiulinzi na kujihami wa Jamhuri ya Kiislamu unalipa taifa hili nguvu za kuonyesha irada yake ya kisiasa, na nguvu zake zinazoweza kutumika dhidi ya adui iwapo italazimu.

Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, mfumo huo wa makombora ya kujihami una uwezo wa kulenga shabaha maeneo ya mbali na karibu kwa usahihi mkubwa kwa kuwa umenakshiwa na teknolojia ya kisasa kabisa.

Katika miaka ya hivi karibuni Iran imepata mafanikio makubwa katika sekta ya ulinzi huku ikijitosheleza kwa kiasi kikubwa katika zana za kujihami. Jamhuri ya Kiislamu inasisitiza kuwa, uwezo wake wa kijeshi si tishio kwa nchi zingine bali sera yake ya ulinzi imejengeka katika msingi wa kujihami.

Mji wa chini ya ardhi wa makombora ya Iran

Aprili mwaka huu, mitambo mipya kabisa ya makombora ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilizinduliwa katika gwaride maalum lililofanyika kwa mnasaba wa "Siku ya Jeshi".

Aidha Novemba mwaka jana 2020, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC lilizindua mfumo erevu na wa kiotomatiki wa kuvurumisha makombora kadhaa ya balestiki ya masafa marefu kwa wakati mmoja.
 
Haya mambo wenzai kitambo wanayo wao.ndio hadi mwaka uishe ndio mtambo uanze kufanyakazi.
 
haitasaidia kuzuia mtambo wao wa nuklia usipigwe na kubomolowa. uwezo wao kijeshi ndio kwanza unafikia uwezo wa kijeshi wa nchi ya Somalia.
 
Jeshi la Iran kuzindua mfumo mpya wa makombora wa 'Joshan'

Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mfumo mpya wa makombora wa Joshan utaanza kufanya kazi kabla ya kumalizika mwaka huu wa Kiirani.

Brigedia Jenerali Ali Reza Elhami alisema hayo jana Jumamosi na kuongeza kuwa, mfumo huo erevu, wa kisasa na unaotumia mifumo ya kisasa ya sayansi kama 'quantum' na 'laser' utazinduliwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa Kiirani ulioanza Machi 21, 2021.

Amebainisha kuwa, uwezo mkubwa wa kiulinzi na kujihami wa Jamhuri ya Kiislamu unalipa taifa hili nguvu za kuonyesha irada yake ya kisiasa, na nguvu zake zinazoweza kutumika dhidi ya adui iwapo italazimu.

Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, mfumo huo wa makombora ya kujihami una uwezo wa kulenga shabaha maeneo ya mbali na karibu kwa usahihi mkubwa kwa kuwa umenakshiwa na teknolojia ya kisasa kabisa.

Katika miaka ya hivi karibuni Iran imepata mafanikio makubwa katika sekta ya ulinzi huku ikijitosheleza kwa kiasi kikubwa katika zana za kujihami. Jamhuri ya Kiislamu inasisitiza kuwa, uwezo wake wa kijeshi si tishio kwa nchi zingine bali sera yake ya ulinzi imejengeka katika msingi wa kujihami.

Mji wa chini ya ardhi wa makombora ya Iran

Aprili mwaka huu, mitambo mipya kabisa ya makombora ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilizinduliwa katika gwaride maalum lililofanyika kwa mnasaba wa "Siku ya Jeshi".

Aidha Novemba mwaka jana 2020, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC lilizindua mfumo erevu na wa kiotomatiki wa kuvurumisha makombora kadhaa ya balestiki ya masafa marefu kwa wakati mmoja.
Kwahiyo hayo makombora yatakusaidia nini ww na familia yako! Bichwa empty kama mzee Mpili wa kisemvule
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom