Iran inawezaje kufanya haya

Tangu vita ianze February Iran anadai kushambulia na kuangamiza hizo kambi kila siku mpaka unajiuliza Marekani ana maelfu ya makambi mangapi kwenye hizo nchi.
Tangu vita vianze, Trump ameshasema ameshinda vita zaidi ya mara moja.
Ameshasema ameimaliza Iran kijeshi zaidi ya mara moja.
Ameshasema Iran haina jeshi la anga wala jeshi la maji zaidi ya mara moja.
Ameshasema Strait of Hormuz ipo wazi, meli zinaweza kupita kwa kujinafasi AKA kujidai zaidi ya mara moja.
Vipi unakubaliana nae!?
 
Jibu jepesi, hawana CCM..
watu wapo kwa ajili ya taifa, watu wanapambania taifa lisonge mbele, unadhani wangekuwa na viongozi wa kama kwetu huku, saa hizi taifa lile halipo ni aidha ishakuwa koloni la israel/america ama nchi ya waisrael kabisa.
Pongezi kubwa kwa viongozi wao..
Wameonesha uzalendo wa hali ya juu mnooo
 
UZALENDO
 
Kama Ukraine na Russia tu. Na hapo maamuzi ni nchi za Ulaya. Kwanini ? Nitaeleza;

Russia ameshindwa kumpiga Ukraine kwasababu
Ukraine inapata misaada mikubwa ya kitaalam, kiufundi, kifedha, silaha na personnel kutoka Ulaya kuhakikisha Russia HASHINDI vita na Ukraine.
Vilevile, Marekani ameshindwa kumpiga Iran kwasababu nchi za Ulaya zimegomba kuchangia chochote kwenye vita vya Marekani na Iran. Na kwa msingi huo, Marekani hata afanyeje HAWEZI kuipiga na kuishinda Iran.
 
Una hoja!
 
Ungemalizia hapo chini wakutajie nchi moja tu iliyowahi kupigana na muajemi ikashinda??
 
Wewe unashangaa kambi haziishi, mimi mwenzio nashangaa na kujiuliza hawa Wairan haya mabomu wanayatoa wapi?
Missile launchers wanaziokota wapi!?

Maana Trump alishalipua kambi zao zote na jeshi lote alishalimaliza.
HAo qatar saudi china pakistan wanasaidia ila kwa siri sana nao wanamzunguka usa kimya kimya yaani nakusaidia ila staki watu wajue
 
Dunia inaendeshwa na mifumo ya kinafki. Cha ajabu watanzania wanawategemea wamarekani kwamba watawaokoa kwenye mdomo wa mamba called CCM
 
Ipende Israel kwa moyo wako YESU atakubaliki achana na mafundisho ya majini
 
Kwenye hiyo namba wanayotaja, unaongeza sifuri.

Hawa Waajemi wanamsumbua sana USA!!!


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…