Japo siwezi kuzitaja IQ zao kwa Tarakimu, kama ningewapanga kulingana na IQ zao, basi ningefanya kama ifuatavyo, nikianzia mwenye Iq ndogo kabisa kwenda juu:
NYERERE : IQ ndogo kabisa kuliko wote. Aliingiza nchi katika matatizo ambayo yameigharimu na yataendelea kuigharimu nchi kwa muda mrefu, kutokana na IQ yake ndogo.
MKAPA: Baaada ya MWINYI kurekebisha kwa kiasi kikubwa matatizo aliyoyaacha Nyerere, huyu bwana alikuja kuharibu kila kitu, ikiwa ni pamoja na kufanya ufisadi wa hali ya juu, yeye na baadhi ya mawaziri wake, ambao umeleta hasara kubwa sana kwa Taifa letu.Sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na kuwa na IQ ndogo, ambayo haikumwezesha kumudu madaraka ya Urais
MWINYI: Kutokana na IQ yake kubwa, aliweza kufufua uchumi na kuleta mageuzi makubwa ya kuichumi, na kuwatoa wananchi katika janga la umasikini alilotuachia Myerere. Siwezi sahahu alivyotuondolea adha ya kununa sukari kwa kaya, kilo moja mara moja kwa mwezi, tena kwa foleni, na lazima uwe na kibali toka kwa mkuu wa wilaya au wa mkoa.nafahamu wengi wenu mlikuwa wadogo sana, au hamjazaliwa.
Mifano ya mageuzi aliyoleta ipo mingi sana, na yote hayo yaliwezekana kwa sababu ya IQ kubwa.
KIKWETE.Aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya, yanaashiria kwamba IQ yake iko juu kuliko wote waliomtangulia.
Sina haja ya kutaja aliyoyafanya, kwa sababu hata huku kuwa ndani ya JF tukiwajadili maraisi wetu mawzo kwa uhuru kabisa bila kukamatwa na kuwekwa kizuizini, ni mfano tosha kwamba ameleta mageuzi makubwa ndani ya Tanzania.
Naomba kuwasilisha.