IPTL liquidators move to sue Harbinder Sethi

IPTL liquidators move to sue Harbinder Sethi

Ilishasemwa tangu mwanzo...fedha za IPTL zimeibwa laivu...yule singa singa ni tapeli ameshirikiana na matapeli wa ccm
hizi fedha zilichotwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao na kuandaa makazi ya wakubwa ugaibuni, kwani wana uhakika mwakani CCM watapigwa chini.
 
MODS: Nimepandwa na hasira sana kwa uamuzi wako wa kuibadilisha headline ya uzi wangu huu na kuuweka katika KJiingereza. Mimi nilikuwa nimeuweka Kiswahili chini ya heading "IPTL Kumekucha; Wafilisi wa IPTL wamfikisha Kalasinga mahakamani kwa udanganyifu". Ninahisi una ajenda zako za siri (ulterior motive) kuibadilisha heading hii kuwa kwa Kiingereza ili wengi wanaoingia JF wakiiona tu waipite tu kwa kutoelewa kwao Kiingerza.

MODS kwa nini umefanya hivyo? Kalasinga kushitakiwa kwa udanganyifu kuhusu ununuzi wa hisa za IPTL ni ishu kubwa kwani suala hili lilitikisa Bunge, viongozi wakuu walituhumiwa kupewa milungula na hadi Balozi wa Uingereza aliingizwa bila sababu. Unataka Watanzania wengi wasiojua Kiingereza wasijue habari hii, angalau kutokana na heading niliyoweka ambayo sikuona kosa lake? Kwa nini umefanya hivyo?

Tafadhali rudisha heading yangu ya Kiswahili.


Nakuunga mkono hawa moderators wa Kenya ambao hata shule hawakwenda ndio wanajifanya vinara wa kubadili heading nk. Tulipoanza JF hakukuwa ma maluelue kama haya na serikali ilikuwa inapita hapa kwa njia ya vibaraka wao kuja kuchota habari siku hizi hakuna chake kutokana na tabia mbaya ambayo huwezi hata kuieleza. Unapoweka heading unakuwa na insight ambayo umeiona, heading inapobadilika na upepo unabadilika vile vile. Mod badili heading na omba MSAMAHA NAFAHAMU NI AIBU NA NGUMU LAKINI UUNGWANA NI VITENDO.


Back to the topic ... ... ... ...

Hili sakata bado linatafuna pesa za walipa kodi tangu lianze in the 1990's na ajabu kubwa (sio ajabu tena) washiriki wakubwa BW nkapa, Mzee rukhsa aliyetuletea jinamizi la rais dhoofu, wote watatu bado wapo na ni wafaidikaji wakubwa wa miradi bandia kama hii. Njia kuu za uchumi zinashikwa na majangili nchi haiwezi kuendelea.
 
hii ni aibu kwa chama changu na serikali yangu nimemjibu mtu hapa cjui kama amenielewa kuwa mwisho wa mkataba IPTL ilitakiwa kuwa mali ya tanesco pia pesa alizopewa singa singa c za kwake cjui kama alinielewa
 
Sisi tunachotaka umeme,kama wameingizana chaka wao kwa wao,watajiju,madamu generator zipo na zinagenerate umeme na watu wanatumia,na serikali inalipa kwa mjibu wa makubaliano,who care kama singasinga kaitapeli kampuni huko malaysia.
ama ndo tunataka kurudia ujuaji wa dowans..,ooh kampuni ni ya kwenye briskef.
''sawa,lakini generator zipo na zinatoa umeme?''.
''zipo sawa,lakini tumeenda marekani hatukuona ofisi zao''.
''kwani wewe shidako ni ofisi za richmond marekani au unataka umeme?''.
ujuaji kibao matokeo tukalimwa bonge la faini.
HATULIPI.
MTALIPA.
HATULIPI NG'O.
NAKWAMBIA MTALIPA.
 
hii ni aibu kwa chama changu na serikali yangu nimemjibu mtu hapa cjui kama amenielewa kuwa mwisho wa mkataba IPTL ilitakiwa kuwa mali ya tanesco pia pesa alizopewa singa singa c za kwake cjui kama alinielewa
Sio za kwake kivipi?zimefikaje kwenye account ya escrow?.

sio zake kivipi wakati mshatumia umeme?.
au sikuhizi benkikuu wanagawa hela kama sandakalawe kwa wageni?
 
Sisi tunachotaka umeme,kama wameingizana chaka wao kwa wao,watajiju,madamu generator zipo na zinagenerate umeme na watu wanatumia,na serikali inalipa kwa mjibu wa makubaliano,who care kama singasinga kaitapeli kampuni huko malaysia.
ama ndo tunataka kurudia ujuaji wa dowans..,ooh kampuni ni ya kwenye briskef.
''sawa,lakini generator zipo na zinatoa umeme?''.
''zipo sawa,lakini tumeenda marekani hatukuona ofisi zao''.
''kwani wewe shidako ni ofisi za richmond marekani au unataka umeme?''.
ujuaji kibao matokeo tukalimwa bonge la faini.
HATULIPI.
MTALIPA.
HATULIPI NG'O.
NAKWAMBIA MTALIPA.

fikiria vizuri mkuu

ukikamatwa na mali ya wizi inakuwaje kwa sasa? .... jibu rahisi ni kuwa utaenda isaidia polisi pamoja na polisi kuchukua hiyo mali ya wizi

nimeanza hivyo maana inakuwaje serikali inalipa mtu aliyeiba kampuni toka kwa wengine (mtu wasiye na mkataba naye) .... sishangai maana kwa serikali hii ni kawaida hasa pale inapokua sehemu ya malipo hayo hurudi kwa wakubwa serikalini

hili sakata lina sura nyingi tu .... ila sehemu ambayo watanzania wanahusika ni malipo ya TANESCO kwa IPTL yaliyochukuliwa wakati kesi ya msingi ya ukokotoaji malipo hayo haijamalizika vizuri.

Pia wananchi wanataka kuona wote waliohusika na huu ufisadi toka awamu ya pili ya rais mwinyi wanachukuliwa hatua .... hii kampuni ilikua ni kwa ajili ya umeme wa dharura kipindi kile 1994/1995 lakini bado ina mkataba mrefu na si ajabu unaongezwa tu muda 20 years later

Swala la hao wawekezaji walivyoibiana humo ndani sisi halituhusu ila tunaweza saidia mahakama zetu au za kimataifa kuenforce maamuzi yao kama kukamata mali za wahusika, etc
 
huyo singa ni mtafutaji kama walivyo wafanyabiashara wote.yaweza kuwa kipindi ananunua hisa za kampuni ya malaysia hisa zao zilikua zimeshuka.kwenye soko la hisa waweza kuta hisa leo dola 100 kesho imeporomoka mpaka dola 1.sasa wale maspeculator wao hapo ndo wanakulaga timing.
unaweza leo ukawa ndo mwenyehisa nyingi kesho kwenye bodi unakuta jamaa limeshakupiga bao.
mambo hayo mbona hata kwenye isidingo yapo.
rugemaila yeye alikua smart na hakutaka kuziachia hisa zake na kaja kuziuza kwa bei kubwa na akapiga bao.
 
Naamini kuwa RAIS MAGUFULI ni member wa JAMIIFORUMS
 
Back
Top Bottom