Ipoje kisheria, wanakijiji walioshinda kesi ya hifadhi kukamatwa tena na polisi nje ya mahakama na kutozwa fedha kila mmoja

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Wanakijiji walishinda kesi hiyo baada ya mahakama kujilizisha pasi na shaka kuwa walikuwa wanalima maeneo ambayo hayana katazo la kutolima. Jumuiya hiyo ya HIFADHI ilikuwa imewashitaki wanakijiji waliokuwa wanalima MAENEO ndani ya HIFADHI yake.
Baada ya ushahidi kutimia ni kweli wanakijiji hawajavamia maeneo ya HIFADHI bali HIFADHI inataka kuvamia maeneo yasiyo ya hifadhi.

Mbali na ulalamikaji huo wa hifadhi wanakijiji walieleza namna walivyohalibiwa mazao yao na kupigwa kwenye unyao huku wakiwa uchi na kuning'inizwa juu.

Baada ya mahakama kuwaambia wameshinda kesi kwa kuwa hayo MAENEO waliyokuwa wanalima sio hifadhi ya wanyama, wanakijiji hao walijawa na furaha huku wakitoka nje.

Walipofika tu nje ya mahakama, wote wakakamatwa na kupelekwa tena polisi. Walipofika polisi waliambiwa "Nyie si mnakimbuka mliingia humu na mlitoka bila kutoa chochote kitu?" Wakiwa na maana polisi kuingia bure na kutoka kwa hela.

Walichangishwa elfu 50 kila mmoja ili waweze kuachiwa na asie nae anabaki. Najiuliza tu Asikali wa hifadhi(maliasiri) waliowakamata na kuwapeleka polisi kabla ya mahakamani, na kwa tafsiri ya mahakama walikamatwa kimakosa, Sasa je kilipishwa faini ni halali?

Pili nataka kujua sheria gani inayotumiwa na POLISI kuingia bure kutoka na hela?


MAENEO:
Hifadhi : Mbarang'andu
Wilaya ; Namtumbo
Mashamba; Namayani
 
Hako ni kautaratibu kao ka Dhulma tu hata kama kapo ndani ya sheria au hakapo, mimi wangenilipa mimi.
 
Back
Top Bottom