Ipo wapi thamani ya JOHO la kuhitimu kama zamani?

Ipo wapi thamani ya JOHO la kuhitimu kama zamani?

MIDFIELD

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2013
Posts
1,944
Reaction score
703
Habari za kutwa wapendwa. Kuna hili suala la kuvaa majoho kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kama ilivyoshamiri siku hizi. Kusema kweli, joho katika siku za nyuma lilikuwa ni vazi maalum lenye hadhi kubwa na lenye kuonesha heshima fulani anayopewa mtu kutokana na kazi au hatua kubwa aliyofikisha katika elimu yake. Hili lilidhihirishwa zamani pale ilipowekwa picha ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) katika fedha halali ya Tanzani, kama sikosei ilikuwa noti ya 1000. Hii ilionesha uthamani wa Joho kutoa taswira ya utaalamu aliofikia mtu na kuwa tayari kulitumikia Taifa kwa utaalamu aliokwisha upata. Kipindi hiki Joho lilivaliwa na mhitimu wa Chuo Kikuu pekee. Hii ilitufanya sisi tuliokuwa tunasoma kuwa na shauku ya kufikia hatua hiyo, ili nasi tuje tuweke historia ya kuvaa joho ktk maisha yetu.
Hata hivyo siku za hivi karibuni mambo yamekuwa tofauti kabisa. Joho limekosa thamani kwani linavaliwa na hata anayemaliza sekondari, shule ya msingi, diploma au mbaya zaidi hata chekechea!!! Jamani, hivi Joho limekosa thamani kiasi hicho! Au ndiyo mambo ya utandawazi?
Wenzangu mnalionaje hili, Karibuni tubadilishane mawazo:
 
Waliovaa majoho enzo hizo unazoziita kuea koho lilikuwa na thamani ndiyo ambao wametuibia pesa kupitia ESCROW, EPA & RICHMOND...

Thamani ya elimu ishapotezwa sana na mawaziri madebe + serikali kiziwi!

Ntafurahiaje joho wakati najua wazi kuna foleni ya 10,000+ people unemployed?

Graduate at your own risk, no one will fight for your living...
 
Mbona hata huko majuu kwenye elimu za ukweli hayo majoho huvaliwa kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Kama tumeiga mifumo ya elimu zao sioni ubaya tukiiga hayo mavazi kwenye ngazi tofauti za elimu.

After all ni majoho tu. Cha muhimu zaidi ni elimu aipatayo mtu.
 
Ni kweli kabisa mkuu
 
Binti yangu ka graduate chekechea juzi kavaa joho na cheti juuu, ni shidaa hata hawaelewi maana ya hilo joho na cheti.

hahahaaaaaa, hata mimi ni hivyo hivyo. kagraduate juzi na januari anaanza std one
 
Hivi huko majuu ambako wanavaa majoho kuanzia kindergarten ina maana huko nako hilo joho halina thamani?

Na hivi haya mambo ya kuvaa majoho tuliyatoa wapi?
 
Joho ni alama tu kuwa umehitimu ngazi fulani.

Jambo moja ambalo litamtofautisha aliyehitimu darasa la saba, sekondari au chuo ni utendaji wa kazi, na ufahamu wa kuchanganua mambo.

Kama umemaliza Chuo kikuu na akili yako haitofautiani na standard seven hata uvae majoho ya dhahabu haina maana.

Tunapenda sana kuona JOHO HALISI LA GRADUATE KICHWANI JINSI ANAVYOPAMBANUA MAMBO NA SIYO KWENYE KITAMBAA CHA NGUO.
 
Siku hizi joho ni biashara lazima litavaliwa kwa wahitimu ili tu watu waingize pesa.

Hapo umenena mkubwa. Mfano leo nimeenda kuchukua Joho kwa ajili ya graduation jmosi, kuna mkataba unajaza kwa sh 5,000/= kwa ajili ya kuazima hilo joho, halafu kuchukua joho lenyewe sh 40,000/=. Jumla 45,000. Halafu unavaa siku moja tu, then unalirudisha. Hii ni biashara ya watu nakubaliana na wewe
 
Hivi huko majuu ambako wanavaa majoho kuanzia kindergarten ina maana huko nako hilo joho halina thamani?

Na hivi haya mambo ya kuvaa majoho tuliyatoa wapi?

Tupe data mkubwa inawezekana concept yangu ni wrong ndo maana nataka tuelimishane
 
Muache ufinyu wa mawazo,
Embu thamani ya digrii yenyewe iko wapi, wengi wamekwenda kujifunza "extra culiculum"" badala ya utaalam.
Mfano wanachuo kucheza picha za ngono .
Leo hii wanvyuo wote wameshusha thamani ya elimu kuliko ilivyotarajiwa kabisaaa .
Kujiuza mpaka thamani ya chips , leo unaniambia niheshim joho na wakati mvaaji mwenyewe ni kilaza wa stadi za maisha/?
Kingine leo unavaa joho mwakani unanigongea sigara mimi mgonga debe ntaliheshimu vipi joho na wakati ulie livaaa huna uhakika wa maisha?
 
Mbona hata huko majuu kwenye elimu za ukweli hayo majoho huvaliwa kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Kama tumeiga mifumo ya elimu zao sioni ubaya tukiiga hayo mavazi kwenye ngazi tofauti za elimu.

After all ni majoho tu. Cha muhimu zaidi ni elimu aipatayo mtu.

Weka picha
 
Weka picha

Hosford-Kindergarten-Grad.jpg
 
Mwanangu alivaa majoho alipohitimu preschool, kindergarten, elementary, na junior high school.

Mpaka afikie Phd hatokumbuka idadi ya majoho ktk maisha yake alokwishakuvaa
 
Ata binti juzi kahitimu kindergarten kavaa joho na kofia na cheti katunukiwa
 
Back
Top Bottom