Ipo wapi nchi ya Tanganyika?

Ipo wapi nchi ya Tanganyika?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,079
Reaction score
4,892
Wadau Tarehe 26 April 1964 Nchi mbili za TANGANYIKA na ZANZIBAR Ziliungana na kupatikana NCHI ya TANZANIA.

Kitu cha AJABU Nchi ya ZANZIBAR ipo Nchi ya TANZANIA IPO lakini NCHI ya TANGANYIKA haipo.

Je, ni MUUNGANO wa Aina gani unaoua NCHI MOJA?

Je, nchi ya TANGANYIKA IPO wapi?

Siku hizi Wakati wa kuadhimisha Uhuru utasikia wanasema UHURU wa TANZANIA BARA NCHI ambayo hakuwepo Mwaka 1961.

TUNAOMBA tuelezwe TANGANYIKA IPO WAPI?
 
Kati ya upuuzi kifimbo alichemka ni huu muungano yani wazanzibari kuna mambo matatu wametupiga.

1: Tunawapa Ulinzi
2: Tunawapa Vyeo Bara
3: Tunawapa ardhi Bara

Kupitia muungano huu wazanzibari wanapata ulinzi wa kijeshi kupitia jeshi la Jwtz ambalo ki budget ni 100% jmt na dsm ndiyo 80% ya pato la jmt. Wao wana jeshi lao la kmkm halitoi ulinzi bara.

Wazanzibari tunawapa vyeo bara kuanzia uraisi hadi serikali za mitaa hadi udiwani na taasisi za umma za bara, ila mbara zenji hapati cheo chochote zenji hata ujumbe wa nyumba 10, hata umesenja kwenye taasisi za umma za zenji hapati sahau kuhusu serikali kuu na top position za umma.

Wazenji bara tunawapa ardhi sehemu yoyote hadi vijijini wamejazana hata asilimia kubwa ya viongozi wa zenji wako dar na mijengo yao ila mbara zenji marufuku kumiliki ardhi.

Ajabu jana nimeskia pesa zimekopwa eti baadhi zitaenda kutekeleza miradi ya pemba sasa huko si kuna serikali ya zenji kama siyo kuingilia majukumu ya smz na kumbypass rais wao ni nini?.
 
Bunge la 1990-1995 lilikuwa moto sana

Kuna miamba 55 wakiongozwa na Njelu kasaka walikiamsha kisawa sawa kutaka kurudisha Serikali pendwa ya Tanganyika

Mzee Malecela akiwa PM akaelewa somo na akamshawishi Amiri Jeshi wa wakati huo aende bungeni akaridhie suala hilo …mipango ya kumkaribisha Rais ikakamilika na kwa 'bahati mbaya' sana Habari zikamfikia Mzee mmoja kule Butiama

Akaomba appoitment na Rais kabla hajaenda Dodoma…akamuomba Rais Wabunge wakakutane nae kwny Close door meeting na wajumbe wa NEC…akaenda kuwaangamiza huko wakatoka wamelegea wote

Hoja yake ilikuwa moja…nyie ni wawakilishi wa wananchi kupitia dhamana ya CCM na sera ya CCM ni serikali mbili…mkitaka kuikana dhamana ya CCM mnapaswa kutoka nje ya ccm mkaombe dhamana ya vyama vya serikali 3 na tayari vipo

Akawatisha kidogo kuwa Chama kinaweza kujivua kuwadhamini mkiendelea na usaliti dhidi ya sera

Hadithi ikaishia hapo

Nikitazama bunge la sasa hivi siwaoni kina Tuntemeke, njelu…Halid Kimbau, Sebastian Kinyondo n.k

Nje ya Bunge akawepo Mwamba mwingine kiboko ya Magabacholi…mzee wa 'kanakwamba' saa ya Ukombozi ni sasa Hayati Mchungaji Christopher Mtikila …9 december alikuwa akiingia uwanja wa Taifa na bendera ya Tanganyika huku akiwashangaa wanaoingia na bendera za Tanzania akisema Tanzania haijawahi kutawaliwa hivyo haijawahi kupata uhuru kwa kuwa haikuwahi kuwa koloni


Sasa hivi unamchomoa Spika kama diwani tu wa kule majohe na kila kitu kinaendelea kama kawa

Kadri vyuo vinavyozidi kumwaga wasomi mitaani idadi ya waoga inaongezeka sijui kwanini?
 
Umenikumbusha Mzee kinyondo na mustachi wake kweli dunia inaenda mbio
 
Back
Top Bottom