Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,348
- 23,757
Ndugu zangu Watanzania,
Siku yaja Siku za Mbeleni ambapo Wanaomtukana Matusi Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu. Watalia na Kububujikwa na machozi ya Damu huku wakiwa wamepiga magoti ardhini na kumuomba Msamaha Rais wetu wakiwa huko huko waliko.
Najua Baadhi wanaongozwa na chuki tu Binafsi na wengine wanasombwa na kufuata tu mkumbo na wengine wanatumiwa na kutumika tu na baadhi ya watu maadui Wa RAIS wetu na Taifa letu kwa ujumla wake.
Wengine wanaongozwa tu na chuki binafsi zinazochangiwa na ubaguzi kwa misingi ya ukabila ,Udini ,ukanda na jinsia tu. Wengine ni kujikatia tu tamaa ya maisha wanajikuta wanakuwa na mahasira kana kwamba Rais Samia ndiye kuwasababishia umaskini wao. Wakati unakuta mwingine alichezea maisha na muda wake halafu leo anataka kuleta na kutolea hasira zake kwa Rais wetu Mpendwa.
Embu fikiria ndugu yangu unakuta mtu leo hii ana miaka 45 au 40 anaanza kumlaumu Rais Samia eti kuwa ndiye kusababisha yeye hana nyumba ya kuishi kwa sababu ya bei ya vifaa vya ujenzi . Unajiuliza miaka yake yote 45 aliyoishi hapa Duniani Rais Alikuwa Ni Mama Samia? Je Mama Samia ndiye angekuja kumjengea nyumba yeye ikiwa yeye ameshindwa kujenga kwa mikono yake katika uumri wake huo wa zaidi ya Miongo 4?
Unakuta mtu mwingine hana ajira na yupo mitaani Tangia 2015 halafu leo anaanza kumlaumu Rais Samia. Unajiuliza Je Rais Samia ndiye Alikuwa Rais wa Tanzania Tangia 2015? Je Amekuta wangapi hawana ajira ? Je nani asiyejua kuwa Rais Samia katoa Maelfu kwa maelfu ya ajira kwa vijana ?
Mwingine anaweza kusema Alikuwa ni Makamu wa Rais. swali linakuja je Anayajua majukumu ya Makamu wa Rais kikatiba ? Je unayajua majukumu ya Rais kikatiba? Je unafikiri Makamu wa RAIS anaweza kutoa Amri kwa Rais kuwa atoe ajira kwa vijana ikiwa Rais yeye ajira siyo kipaumbele chake kwa wakati huo?
Ni mingapi mazuri na makubwa amefanya Rais wetu Mpendwa yaliyokuwa kiu ya watanzania na kila mmoja alitamani kuona ya kifanyika? Hivi mmesahau ya kuwa Mama yetu alikuta Taifa lina mgawanyiko mkubwa kwa misingi ya itikadi za kisiasa? Mmesahauu ilifika wakati watu wanazikana kwa kuangalia aliyekufa ni wa chama kipi?
Mmesahauu kuwa alikuta hakuna habari za mikutano ya hadhara? Mnakumbuka kuwa alikuta kuna watanzania wamekimbia nchi? Mnakumbuka kuwa alikuta vijana wametapakaa mitaani na vyeti vyao vya shahada? Mnakumbuka kuwa alikuta vyombo mbalimbali vya habari ikiwepo magazeti yamefungiwa kufanya kazi zake?
Mnakumbuka alikuta kuna wafanyabiashara wengine wanaendelea kuhamisha biashara zao na kuzikimbizia nje ya Nchi? Mnakumbuka kuna wafanyabiashara walikuwa wanachotewa pesa zao kwenye akaunti zao? Mnakumbuka mangapi ambayo mlikuwa mnalialia na kutaka yafanyiwe marekebisho?
Ni nani aliyelileta Taifa pamoja mpaka watanzania kuanza kuzikana bila kujali itikadi za kisiasa wala Dini ya mtu? Si ni Mama yetu ndiye aliyekuja kuliunganisha Taifa letu? Si ni Mama yetu mpendwa ndiye aliyekuja kuwapa matumaini wafanyabishara? Si ni Mama yetu Mpendwa ndiye aliyefanya akina lissu, Godbless Lema na wengine wengi kurejea Nchini? Si ni Mama yetu Mpendwa aliyepiga marufuku mfanyabiashara kuchotewa pesa zake Bank? Si ni Mama aliyeanza kutoa maelfu kwa maelfu ya ajira kwa vijana?
Si ni Rais Samia aliyeanza kuvifungulia vyombo vyote vya habari vilivyo fungiwa na kupokonywa leseni zao? Mnataka RAIS wetu awafanyie nini wenye Watanzania mpate kuridhika wenye mliokosa shukurani?
Nini na kipi hajafanya na Kugusa RAIS wetu Mpendwa? Kwanini tunataka kumvunja moyo Rais wetu Mpendwa? Kwanini tunakosa shukurani kiasi hicho? Tumesahau mara hii tulikotoka?
Mnaweza kusema ni chama gani kilikuwa madarakani? Jibu ni kuwa CCM ni chama kinachojisahihisha na kufanya marekebisho panapostahili na kuendana na mahitaji ya wakati na muda. Ni chama kinachosikiliza Sauti za watu. Ndio maana ya kuwa chama kiongozi Barani Afrika.
Kwa hakika ipo Siku wenye kumtukana Rais wetu Mpendwa watakuja kujutia na kuomba Rais wetu na mama yetu mpendwa aendelee kuliongoza Taifa letu hata baada ya kumaliza muda wake wa kukaa kitini 2030.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.