Ipo siku JamiiForums itaandikwa kwenye historia ya Tanzania

karatta

Senior Member
Apr 2, 2012
109
46
Wakuu poleni kwa maisha magumu kwa kila mtanzania,poleni madaktari kwa kiongozi wenu kufanyiwa unyama.

Naamini kabisa JF one day itaandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu vya ukombozi wa taifa letu.

JF nimekuwa nikiifatilia kwa muda mrefu sana, na nimegundua kuwa ni moja ya chachu ya MAPINDUZI ya taifa letu, ikumbukwe mapinduzi ya Misri yalichochewa na mitandao ya kijamii, so WITO WANGU naomba tunavyo kuwa tunapashana habari na kujuzana mambo muhimu kuhusu taifa letu, naomba kila mwenye ndungu vijijini ajaribu kuwa ANAWAELIMISHA, coz watu wa vijijini walio na elimu ndogo, hawapati habari kwa muda NDIO WATUMWA WA CCM,THEY DON'T KNOW WHAT TO DO, zaidi ya kuendelea kuwa mtaji wa MAGAMBA.

Kwa upande wangu nimejaribu sana kuelimisha nugu zangu wengi sana wa vijijini and i hope wamenielewa and they will participate for changes.

vipi kuhusu ndugu zenu wa vijijini?

Bibilia inasema msiogope bwana atasimama mbele yenu!

TOGETHER WE CAN MAKE CHANGES,we beleave in God n he will stand for us!
 
Huu ndio mtandao pekee Tanzania wenye kusimamia ukweli na uwazi, na unatekeleza 100% uhuru wa mwananchi kujieleza na kushiriki ktk mijadala, ombi langu ni kuwa JF idumu na misimamo yake mpk Tz yetu itakapopata ukombozi wa kweli! Mungu ibariki JF, Mungu ibariki Tanzania!
 
Ni kweli imeulizwa hata Bungeni Serikali inaiona ni CHADEMA nyingine, Taabu ya Serikali Dhaifu mtu yeyote anae ongea ukweli ina mwona ni CDM, Haitaki sasa kusikia ukweli, inataka isifiwe hata ktk Ujinga, na Imeishiwa mbinu za kuleta Ustawi kwa watanzania, na imeamua sasa kukomoa wananchi kwa kutafuna mafedha na malasilimali kwa kasi ya ajabu. ndo maana kila siku ni fedha zimeliwa mara twiga kapandishwa ndege, mara wamewekewa mapesa huko Uswis, si tunadanganywa ooh Gas kumbe watu wamesha uza na kula cha juu, CCm sasa ina Komoa 2
nahisi serikali inaiogopa jamii forum.
 
mama Lwakatare aliuliza bungeni "nani ni mmiliki wa jamii forum"?

ccm walisema matokeo mabaya waliyopata ya uchaguzi mkuu wa 2010 yalisababishwa na jamii forum pia.
 
Kwangu mimi JF ni kila kitu.

Kwanza imenifanya niwe jasiri, niwe mwenye kujenga hoja kwa evidence (source) vilevile kuyafahamu mambo mengi, ya uhakika na kwa haraka.

Mungu ambariki mwanzilishi.
 
Kwa nini inaonekana kwamba JF ni wanasiasa? ina maana kule MMU na jukwaa la wakubwa wadau wake nani sasa? ni upuuzi mtupu JF ina jukwaa moja tu siasa, na majukwaa mengine yanawanufaisha watu mbalimbali, ila kwakuwa kuna mijitu wao inawaza siasa tu, wanadhani JF ni Chadema na CCM, huu ni uvivu wa kufikiri
 
Kweli kabisa ndio Media iliyo huru haiegemei CDM wala CCM wala CUF na ni chombo kisichochuja habari hivyo naomba MUNGU akijalie kidumu hata Dahari na Vyama vyote vife na JF idumu
 
Karatta.

Acha kujidanganya JF sio mali ya Chadema kwanza fahamu hivyo...JF ni Jukwaa huru kuna watu wa kila aina kuna wana CCM, Chadema, NCCR Mageuzi, CUF, TLP, na vyama vingine na wasiokuwa na vyama...vile vile JF ni shule kwa watu wengine kwenye majukwaa yao JF...hakuna ubaguzi ni Jukwaa huru.
 
Karatta.

Acha kujidanganya JF sio mali ya Chadema kwanza fahamu hivyo...JF ni Jukwaa huru kuna watu wa kila aina kuna wana CCM, Chadema, NCCR Mageuzi, CUF, TLP, na vyama vingine na wasiokuwa na vyama...vile vile JF ni shule kwa watu wengine kwenye majukwaa yao JF...hakuna ubaguzi ni Jukwaa huru.

Kalale dogo ukue, nyinyiemu maumivu matupu kwani vifo vya wasio na hatia mwaona fahari,ole wenu pana siku yaja ya kulia na kusaga meno,
Endeleeni kujidanganya kwamba mtatawala milele.
 
Back
Top Bottom