Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,542
- 3,451
IPO NAFASI NAFASI YAKO, FANYA YANAYOKUHUSU.
Maisha siyo vita wala kupambana sana ili kuwazidi wengine, maisha pia siyo kusubiri wakati tunaouita mzuri na majaliwa tu halikadhalika maisha siyo kile unachoambiwa au kukiona kwa wengine ila ni vile unavyoishi wewe.
Tafsiri sahihi ya maisha yako ipo kwako na siyo kwa mwingine yeyote. Maisha ya mwingine hayawezi kuwa tafsiri sahihi ya maisha yako.Maana ya maisha yako ni wewe unavyoishi na kuuelewa ulimwengu wako.
Suala la msingi zaidi ni kujielewa wewe mwenyewe kabla ya kutaka kuwaelewa wengine na kushindana nao. Kumbuka kila mtu anacho kitu chake anachoweza kukifanya kwa wepesi zaidi katika maisha yake.
Tambua kitu chako cha kufanya kuliko kukazana kutambua wanachofanya wengine na kujishidanisha nao. Kumbuka wao pia wana uwezo ambao wewe huna. Ipo nafasi ya kwanza kwa kila mtu inaitwa "upekee".
Tumia nafasi yako ya kwanza kufanya vitu vyako kwa sababu kila mtu ana nafasi yake ya kwanza katika kufanya mambo yake. Hivyo jitahidi sana kufanya yale yanayokuhusu zaidi kuliko kuumia na namna wengine wanavyotumia nafasi yao ya kwanza.
Kumbuka kuna vitu unaweza kuvifanya wewe na wengine wasiweze kabisa ila haimaanishi wao hawana vya kwao ambavyo wewe huwezi hata ukijilazimisha. Nadhani kufanya mambo yako ndiyo jambo la msingi zaidi.
"Live your life".