ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Ukiwa na mpenzio/ mume/mkeo mwatembea mmeambatana, mara inapotokea jozi (pea) nyingine ya wapendanao mkapishana nayo, jaribu kuchunguza kwa makini...
Wengi ya wapendanao huwa wanapoteza kabisa kwa muda hisia zao juu ya wenzi wao...
Kwa kawaida baadhi ya wanaume huwa na jicho la kasi la tathimini, waweza hata kugeuza shingo kwa staili kumtizama mwanamke wa wenzie..huku akifikiri moyoni labda kuna vitu anavikosa.... Pengine kama utabahatika, unaweza kukuta kumbe na mwanaume mwenzio nae huko nyuma alikuwa akimkata jicho wa kwako akiwa na fikra zinazofanana na wewe!!.
Kwa wanawake, wao si rahisi sana kukuta anageuka, ila baadhi yao anaweza kuanza kuwaza moyoni mambo mengi ikiwemo tofauti iliyopo katika yake na mwanamke mwenzie au kati ya mwanaume alie nae na yule wa mwenzie.. tofauti ya mavazi,ulembo na harufu ya manukato yake na yale ya mwenzie..atatamani au kukereka nafsini, kwa nini ipo vile kwa wengine na sio kwake...
Ukiwa makini sana unaweza kuyabaini haya kwa vitendo, ..wengi ya wanawake, anaweza kuguna,kuanza kujifuta uso, kulamba midomo, kurekebisha nywele, kuweka vizuri pochi, mavazi yake nk au pia kuanzisha maongezi yeyote tu juu ya wale mliopishana nao.. kama si kuwaponda basi kuwasifia.
....kama hakuwa amekushika mkono, bega au kiuno, na akiona hizo pea nyingine wameshikana, atafanya kila jitihada ya kuhakikisha nae anakukaribia, au pengine ikiwa ni mwanaume unamkwepa kwa kuwa ndae mbali, atazungumza tu "ona wenzetu/wenzio wanaojua mapenzi"...
Kwa asili, wengi wetu huwa twapenda kutamani au kuchukia kitu kikiwa kwa mwenzio..mengine yanatufundisha na mengine yanatuharibia kabisa...