Ipo haja Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya wa Pwani wawe wanajeshi

moma2k

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
1,091
1,405
Hali halisi ya matukio haya ya kihalifu yanaleta wito wa kuwa na mkuu wa mkoa wa Pwani kuwa mwanajeshi.Sisi raia ni siasa tu. Mkuu wa mkoa akiwa mjeshi uozo wote utafutika mara moja. Tumeshuhudia Major General S.Kijuu alivyo safisha wavamizi ktk mapori tengevu ya Mkoa wa Kagera.Pwani needs a strong person with military background to address th existing problem.

---
ibesa mau said,
Kwa hali jinsi ilivyo ipo haja ya viongozi wakuu wa ulinzi na usalama wa mkoa wa pwani na wilaya zake wawe wanajeshi wa vyeo vya juu.

Mkoa wa Pwani unaonekana kama kichaka cha kujificha majambazi na kufanyia uhalifu, vilevile watu wengi wanao uliwa maeneo mengine hutupwa katika mkoa huo.

Ipo haja kwa Rais Magufuli kuweka viongozi wanajeshi mkoa huo. Nadhani hiyo itasaidia kupunguza uhalifu. Tena kwa nyongeza Rc awe mwanajeshi,ma dc wawe wawe wawe makanari, maafisa tarafa wawe maluteni , watendaji wa kata wawe wanajeshi, watendaji wa kijiji, mtaa wawe wanajeshi pia. watumishi wote wanao ongoza taasisi kama shule wawe kutoka usalama usalama wa taifa.

Kama ilivyo kwa mikoa ya mipakani au pembezoni yote kuwa na wakuu wa mikoa wanajeshi na huu mkoa uangaliwe kwa jicho la pekee kama mikoa yote yenye viashiria vya vurugu.
 
Wakuu wa mikoa ni jau tu pengine ndio wanafanya hata vyombo vyetu vya ulinzi kuacha weledi na kufuata matakwa ya wakuu hao ambao ni makada wasiojua lolote kuhusu usalama wala ulinzi zaidi ya kuhakikisha nyumbu wa kijani wanabakia madarakani
 
Hali halisi ya matukio haya ya kihalifu yanaleta wito wa kuwa na mkuu wa mkoa wa Pwani kuwa mwanajeshi.Sisi raia ni siasa tu. Mkuu wa mkoa akiwa mjeshi uozo wote utafutika mara moja. Tumeshuhudia Major General S.Kijuu alivyo safisha wavamizi ktk mapori tengevu ya Mkoa wa Kagera.Pwani needs a strong person with military background to address th existing problem.
Wanajeshi huwa hawashindwi, hawavamiwi? hawafi ? Think again!
 
Sasa Akiwa mwanajeshi ndio majambazi yatakimbia? Nikutafuta mbinu mbadala kuweza kumaliza hili jambo kwa kuimarisha intelejensia katika ulinzi na usalama wa RAIA..na kuweka mahusiano mazuri kati ya RAIA na Askari ili kupata taarifa muhimu za kipelelezi.
 
Hali halisi ya matukio haya ya kihalifu yanaleta wito wa kuwa na mkuu wa mkoa wa Pwani kuwa mwanajeshi.Sisi raia ni siasa tu. Mkuu wa mkoa akiwa mjeshi uozo wote utafutika mara moja. Tumeshuhudia Major General S.Kijuu alivyo safisha wavamizi ktk mapori tengevu ya Mkoa wa Kagera.Pwani needs a strong person with military background to address th existing problem.
Kweli kalamu ya mjinga huandika popote. Kwani nani kakwambia hili ni tatizo la kijeshi?
 
Mimi nadhani issue ni uhusiano mbaya uliopo kati ya Jeshi la Polisi na Jamii na kati ya serikali za Mitaa na Jamii. Hebu Polisi na Viongozi wa Mitaa wajitathmini na kujichungiza kama kweli wanatenda kazi zao kwa haki bila uonevu wa hali yoyote !
 
Hali halisi ya matukio haya ya kihalifu yanaleta wito wa kuwa na mkuu wa mkoa wa Pwani kuwa mwanajeshi.Sisi raia ni siasa tu. Mkuu wa mkoa akiwa mjeshi uozo wote utafutika mara moja. Tumeshuhudia Major General S.Kijuu alivyo safisha wavamizi ktk mapori tengevu ya Mkoa wa Kagera.Pwani needs a strong person with military background to address th existing problem.
Nakuunga mkono
 
Pwani igeuzwe kuwa Kanda Maalum ya Kipolisi Kama Dsm na Tarime

Serikali iongeze Informers wa kutosha katika Jamii husika kwani hao Magaidi wanapigana vita pia ya kisaikolojia Ndio sababu hawauwi Raia wa kawaida ili Raia wasiwaone ni sehemu ya Tatizo, naskia hao Magaidi wametokomeza hata vitendo vya ujambazi uliokuwa awali

Askari wakiwa kwny operation wapunguze kutumia Magari rasmi ya Polisi yenye plate no. za PT

Polisi Jamii iliyaonzishwa na Jk chini ya IGP Mangu ambayo Magufuli aliibeza irejeshwe ili kushirikisha zaid Raia ambao itakuwa wanajua ABC za hao Wauaji
 
Hali halisi ya matukio haya ya kihalifu yanaleta wito wa kuwa na mkuu wa mkoa wa Pwani kuwa mwanajeshi.Sisi raia ni siasa tu. Mkuu wa mkoa akiwa mjeshi uozo wote utafutika mara moja. Tumeshuhudia Major General S.Kijuu alivyo safisha wavamizi ktk mapori tengevu ya Mkoa wa Kagera.Pwani needs a strong person with military background to address th existing problem.
I don't think kwamba kuwa na RC mwanajeshi ndio suluhu, cha muhimu hapo inatakiwa a holistic approach, majeshi yote yashikiri kuondoa hilo tatizo kwa kushikiriana na wananchi. RC ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ana polisi, uhamiaji, magereza, TISS, JWTZ ambao wanaweza kumshauri cha kufanya, ila hata akiwa ni mjeshi sidhani yeye ndio atashika bunduki na kupigana.

Lakini umesahau kuwa katibu mkuu wa mambo ya ndani ni JWTZ na katibu mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT ni raia.

hapa ni suala vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kujipanga tu.
tanzania siasa ndo imeshika namba moja mengine yatafata nyuma
Yes Tanzania siasa ndio mwendo mzima, walipoteuliwa ma RC wanajeshi huko Geita, Kigoma, Katavi, Rukwa, na Kagera plus maDC wa kasulu, Kibondo etc, kelele zilipigwa sana ooooh nchi imekuwa ya wanajeshi, oooh serikali ya kijeshi, sasa naona hapa anatakiwa RC mwanajeshi, kweli hii ni siasa.

Wakuu wa mikoa ni jau tu pengine ndio wanafanya hata vyombo vyetu vya ulinzi kuacha weledi na kufuata matakwa ya wakuu hao ambao ni makada wasiojua lolote kuhusu usalama wala ulinzi zaidi ya kuhakikisha nyumbu wa kijani wanabakia madarakani
Atakuwa mkuu wa mkoa wa ajabu sana atakayeendekeza njaa na kuacha watu wauwawe hivyo. Labda sijakuelewa unataka tuamini kuwa RC wa Pwani ndio kaelekeza hao vijana wauwawe?
 
Hali halisi ya matukio haya ya kihalifu yanaleta wito wa kuwa na mkuu wa mkoa wa Pwani kuwa mwanajeshi.Sisi raia ni siasa tu. Mkuu wa mkoa akiwa mjeshi uozo wote utafutika mara moja. Tumeshuhudia Major General S.Kijuu alivyo safisha wavamizi ktk mapori tengevu ya Mkoa wa Kagera.Pwani needs a strong person with military background to address th existing problem.
RC akiwa mjeshi ndo atakuwa analala kwenye lindo au ataliondoa jeshi la polisi kulinda raia na mali zao na aweke wanajeshi?
 
Hali halisi ya matukio haya ya kihalifu yanaleta wito wa kuwa na mkuu wa mkoa wa Pwani kuwa mwanajeshi.Sisi raia ni siasa tu. Mkuu wa mkoa akiwa mjeshi uozo wote utafutika mara moja. Tumeshuhudia Major General S.Kijuu alivyo safisha wavamizi ktk mapori tengevu ya Mkoa wa Kagera.Pwani needs a strong person with military background to address th existing problem.

Kuongozwa na mwanajeshi si kigezo cha kuufanya Mkoa wa Pwani uondokane na matukio haya ya uhalifu,mbona nchi inarndeshwa na Amiri jeshi mkuu,Rais anayejiamini tena aliyeenda peke yake kuchukua fomu na bado matukio hayo yanafanyika nchini mwake?

Dola lililoparaganyika ndiyo chanzo cha matatizo yote,kama vikosi vya ulinzi na usalama vinaweza kutoka kambini na kuhamia barabarani nchi nzima ili kuudhibiti UKUTA,kwa nini vikosi hivyo visijipange kukabiliana na magenge hayo ya kihalifu?

Kile tulichozoea kuambiwa kuwa intelijensia ya polisi imebaini kutakuwa na uvunjifu wa amani mahali ambapo wapinzani huomba kufanya shughuli zao za kisiasa,kwa nini intelijensia hiyo isitumike kufahamu uvamizi wa wahalifu waliojipanga kulidhuru jeshi?Au nlintelijensia yao ni kwa mambo ya siasa tu?

Tunavuna tulichopanda,tuliwekeza nguvu nyingi sana katika mkakati wa kusomeshana namba,tukasahau masuala nyeti yahusuyo ulinzi na usalama wa Taifa letu,ngoja tuisome namba,wakati sisi tunasomeshwa namba kwa amri na matamko,huku tukiadhibiwa na ugumu wa maisha,wanaotusomesha namba nao wanapewa tuition ya namba kwa mtutu wa bunduki!

Chuki na visasi vya utawala ndiyo vilivyotufikisha hapa tulipo,hakuna anayejali.Kama watu wanauwawa na wengine wanapotea kwa takribani nusu mwaka sasa na serikali na vyombo vyake imekaa kimya,ni nani wa kujishughulisha na matukio haya dhidi ya polisi?Naanzaje kwa mfano kulionea huruma jeshi ambalo halinitendei haki pale ninapohitaji haki?

Tulipofikia ni matokeo ya kiburi na dharau za watawala wetu,hadi pale watawala wetu watakapojitambua,ndipo ushirikiano wa kijamii utarejea na kuliponya Taifa letu.
 
Mwanajeshi ndiyo atakaa porini muda wote kusubiri hao magaidi?
Hiyo habari ya magaidi inatoka wapi??? MTU MWENYE MAMLAKA YA KUTANGAZA TISHIO AU JANGA LOLOTE HAPA TANZANIA NI RAISI TU, HAKUNA UGAIDI HAPA NCHI, tuache kutumia maneno mazito ya kutisha watu. waliofanya mauaji ya Askari ni MAJAMBAZI yasiyopenda amani tuombe amani katika nchi yetu
 
Nadhani ufanyike uchunguz wa kina, kuna nn nyuma ya pazia, kwasababu matukio yote yanatokea wakati raia wanashuhudia, lakini ikihitajika msaada, watu wanakaa kimya
 
Hali halisi ya matukio haya ya kihalifu yanaleta wito wa kuwa na mkuu wa mkoa wa Pwani kuwa mwanajeshi.Sisi raia ni siasa tu. Mkuu wa mkoa akiwa mjeshi uozo wote utafutika mara moja. Tumeshuhudia Major General S.Kijuu alivyo safisha wavamizi ktk mapori tengevu ya Mkoa wa Kagera.Pwani needs a strong person with military background to address th existing problem.
Takwimu zinaonyesha asilimia kubwa ya wanafanya matukio ya Bunduki ni Askari..
 
Back
Top Bottom