Ipi Zaidi: Samsung Galaxy au Pebble

ManiTek TV

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
410
159
Saa ya Pebble ilikuwa miongoni mwa smart watch za mwanzo kabisa kuingia sokoni, Nike walifuatia na Nike Fuelband na kampuni nyingine kadhaa ikiwemo Sony. Makala hii itafananisha Saa ya Pebble dhidi ya Samsung Galaxy Gear ili tuone kama Samsung wamerudi nyuma, wamefanya ugunduzi wowote tofauti na Pebble, pia ni ipi kati ya hizi mbili ni bora zaidi kwa mujibu wa pointi za Gajetek. Katika mpambano huu pia Gajetek tutatoa pointi kwa kila jambo ambalo limeninganishwa na hivyo kutangaza mshindi mwishoni.

Skrini na Display

Skrini ya Pebble ni ndogo ukilinganisha na Galaxy Gea, ambapo Pebble ina ukubwa wa 1.26” wakati skrini ya Gear ina ukubwa wa 1.63”, ukubwa wa skrini katika smart watch ni kitu muhimu sana ukizingatia saa hizi zina kazi nyingi mno.

Pebble na Samsung wamefanya mkakati tofauti, wakti Pebble wametumia display aina ya e-Paper, Samsung wametumia Super Amoled, hivyo basi Pebble inatumia chaji kiasi kidogo mno ingawa ubora wa skrini ni wa hali ya chini mno, na Samsung ina skrini yenye ubora wa hali ya juu lakini inakula betri mno. Vile vile skrini ya Gear ni skrini mguso (touch screen). Wakati skrini ya Pebble ina ppi 176 Samsung Galaxy Gear ina ppi 278. [Hapa Gear imepata pointi 5 na Pebble pointi 2]

Betri

Hivyo kwa upande wa chaja Pebble inadumu siku 5 hadi 7 wakati Galaxy Gear inadumu masaa 24 tu. Zote zinatumia chaja za USB. Hivyo ukisahau kuichaji samsung, huna saa siku nzima kama ni mtu uliye na mishwari mingi ya kimaisha. (Pebble point 5 na Samsung point 2)

Muonekano

Pebble inaonekana ndogo na kufit mkononi vizuri na saa yenyewe pamoja na mkanda ni raba au silicone, mtumiaji anaweza kubadili mikanda ya rangi mbali mbali na hivyo kupata mabadiliko siku hadi siku, zote Samsung na Pebble unaweza kubadili muonekano wa sura ya saa kwa kutumia app. Pebble ina rangi tano tofauti ukiwemo nyeupe, nyeusi, nyekundu na grey.

Samsung kwa upande wake inaonekana saa ambayo ni “solid” ikiwa ni ya stainless steel na mkanda wa sylicone. Hivyo Samsung ni saa ambayo inaonekana ya kiume kutokana na ukubwa. Pia Samsung Galaxy Gear inapatikana katika rangi sita tofauti ikiwemo nyeupe, nyeusi, manjano, kijani na bluu [Gear pointi 5 na Pebble point 4]

Kamera

Samsung ina kamera yenye 1.9 mp na ina uwezo wa kurekodi video za HD, Kamera hii inachukua video fupi za muda usiozidi sekunde kumi kwa sasa. Pebble haina kamera. [Gear point 5 - Pebble point 0]

Prosesa

Pebble inatumia prosesa yenye kasi ndogo sana aina ya ARM Cortex M3 ambapo ina kasi ya 80MHz, hii ina maana kwamba apps na PEbble lazima ziwe hazihitaji nguvu kubwa ya prosesa katika utendaji kazi hivyo itawafanya watengeneza Apps wawe na mambo machahce ya kufanya.

Samsung Galaxy Gear kwa upande wake inatumia prosesa yenye kasi ya 800MHz, hii ni mara kumi ya kasi ya prosesa ya saa ya Pebble. [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble point 2]

OS na Apps

Pepple imetoka na OS yao binafsi ambayo inaitwa Pebble OS wakati huu ni ugunduzi mzuri lakini haitavutia watengenezaji wa apps (developers), Samsung Galaxy Gear inatumia Android ambapo developers wengi watavutika kirahisi kutengeneza apps. Gear imetoka ikiwa na Apps 70 [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble pointi 1]

Sensa na kuunganisha (connectivity)

Pebble ina akselerometa, e-compass na sensa ya mwangaza (ambient light sensor) ambayo inasaidia kudumisha betri ya Pebble. Pia Pebble ina bluetooth 4.0. Samsung ina akselelrometa na sensa ya gyro. Samsung haihitaji sensa ya mwangaza kwa vile inapokuwa haitumiwi saa hivyo inazima skrini mithili ya simu.[Samsung Galaxy Gear pointi 4 - Pebble pointi 5]

Bei

Pebble inauza nusu ya bei ya Gear kwa $150 huku Gear ikiuzwa jumla ya $300. Huu ni udhaifu mkubwa wa saa ya Samsung wengi wakiwa na mtazamo kuwa ni ghali mno. Nike Fuelband ni $150 na Sony Smartwatch 2 ni $150, zote hizi ni bei za Marekani. [Samsung Galaxy Gear pointi 1 - Pebble pointi 5]

Audio na Video

Wakati Pebble haina uwezo wa kutoa sauti au kucheza video Samsung Galaxy Gear ina Video Codec H.264 na inacheza MP4 inarekodi video za HD 720p@30fpsna sauti aina ya AAC na M4A. Pebble inafanya notification tu. [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble pointi 1]

Memory

Samsung ina 4GB disk ambayo ina uwezo wa kuhifadhi mafaili ya sauti, video na picha. Pebble haina disk ya kutumiwa na mtumiaji kwa mafaili yake binafsi. [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble pointi 0]

Maji

Pebble inatumia teknolojia ya IP55 kuzuia maji ambapo unaweza hata kuogelea nayo bila ya shaka yoyote. Samsung inatumia teknolojia ya 5ATM kuzuia maji, yaani unaweza tu laba kuoga nayo au kutembea nayo kwenye mvua lakini huwezi kuogelea nayo. [Samsung Galaxy Gear pointi 2 - Pebble pointi 5]

Utangamano (Compatibility)

Pebble inaweza kuunganishwa kwa teknolojia ya bluetooth na simu yoyote ya Google au iPhone. Galaxy Gear kwa sasa inafanya kazi na Samsung Galaxy Note 3 na Samsung Galaxy Note 10.1 (2014 Edition itakapotoka) tu. Pia Samsung wametangaza baada ya kufanyiwa uboreshwaji wa OS kwenda android 4.3 simu za Galaxy S3, Galaxy S4 na Galaxy Note 2 nazo zitakweza kufanya kazi na saa hii. [Samsung Galaxy Gear pointi 1 - Pebble pointi 5]

Mambo Mengine Muhimu

Samsung Galaxy Gear ina-features nyingi muhimu kama vile uwezo wa kupokea simu na kuongea kwa kutumia saa ambapo mtumiaji ananyanyua mkono na kuuweka karibu na sikio, vile vile ina feature ya smart Relay ambapo unapofungua app fulani kwenye saa na simu pia hufunguka app hiyo hiyo kwenye simu hivyo huna haja ya kufungua app unapotaka kuhamia kwenye simu. Pia Gear ina S Voice, Memographer (Picha) na Voice Memo, vitu hivi havipatikani kwenye Pebble.

Pebble inajitangaza kuwa na uwezo wa notification, alarms, kubadili muonekano wa saa, app za mazoezi na ku-control muziki kwenye simu. Hizi zote zinapatikana kwenye Gear tena kwa ubora zaidi. Mathalani Samsung ina face ambazo zinaonyesha pia na hali ya hewa mbali na saa, Pebble haina uwezo huo, Wakati Pebble ina-control muziki Gear inacheza muziki, video na kurekodi pia. [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble pointi 2]

AQ1

Chati ya Vielelezo

Matokeo
Samsung Galaxy Gear pointi 50/65 = 77%

Pebble Watch pointi 32/65 = 49%

Hivyo Samsung Galaxy Gear ni Saa bora kuliko Pebble.

Ubora wa Gear dhidi ya Pebble: Pebble imeangushwa na Gear kwa sababu 5 kuu: Ina kamera, kasi ya CPU, Microphone inayoruhusu kuongea bila kutumia simu na ubora wa display, ina memory inayoruhusu kuhifadhi picha, video na mafaili ya sauti na inafanya mambo mengi zaidi kama vile smart relay, voice memo, memographer na S Voice.

Ubora wa Pebble dhidi ya Gear: Pebble walikuwa ni wa mwanzo kufanya ugunduzi, inafanya kazi na simu za Android zote pamoja na iPhone kadhaa, unaweza kubadili mkanda na bei kidogo inaridhisha.

Hata hivyo tukizingatia kuwa Pebble ni saa ambayo haikuwa hata na kampuni (imechangiwa kwa mtindo wa crowdsourcing kama kickstart project, hawana budi kupewa pongezi kwa kazi nzuri

Pointi za Gajetek ni maoni yetu binafsi ambapo wengi wanaweza kutofautiana na maoni hayo. Tungependa kujua mtazamo wako na sababu za mtazamo huo ikiwa umetofautiana nasi.

Source: gajetek habari

Saa ya Pebble ilikuwa miongoni mwa smart watch za mwanzo kabisa kuingia sokoni, Nike walifuatia na Nike Fuelband na kampuni nyingine kadhaa ikiwemo Sony. Makala hii itafananisha Saa ya Pebble dhidi ya Samsung Galaxy Gear ili tuone kama Samsung wamerudi nyuma, wamefanya ugunduzi wowote tofauti na Pebble, pia ni ipi kati ya hizi mbili ni bora zaidi kwa mujibu wa pointi za Gajetek. Katika mpambano huu pia Gajetek tutatoa pointi kwa kila jambo ambalo limeninganishwa na hivyo kutangaza mshindi mwishoni.

Skrini na Display

Skrini ya Pebble ni ndogo ukilinganisha na Galaxy Gea, ambapo Pebble ina ukubwa wa 1.26 wakati skrini ya Gear ina ukubwa wa 1.63, ukubwa wa skrini katika smart watch ni kitu muhimu sana ukizingatia saa hizi zina kazi nyingi mno.

Pebble na Samsung wamefanya mkakati tofauti, wakti Pebble wametumia display aina ya e-Paper, Samsung wametumia Super Amoled, hivyo basi Pebble inatumia chaji kiasi kidogo mno ingawa ubora wa skrini ni wa hali ya chini mno, na Samsung ina skrini yenye ubora wa hali ya juu lakini inakula betri mno. Vile vile skrini ya Gear ni skrini mguso (touch screen). Wakati skrini ya Pebble ina ppi 176 Samsung Galaxy Gear ina ppi 278. [Hapa Gear imepata pointi 5 na Pebble pointi 2]

Betri

Hivyo kwa upande wa chaja Pebble inadumu siku 5 hadi 7 wakati Galaxy Gear inadumu masaa 24 tu. Zote zinatumia chaja za USB. Hivyo ukisahau kuichaji samsung, huna saa siku nzima kama ni mtu uliye na mishwari mingi ya kimaisha. (Pebble point 5 na Samsung point 2)

Muonekano

Pebble inaonekana ndogo na kufit mkononi vizuri na saa yenyewe pamoja na mkanda ni raba au silicone, mtumiaji anaweza kubadili mikanda ya rangi mbali mbali na hivyo kupata mabadiliko siku hadi siku, zote Samsung na Pebble unaweza kubadili muonekano wa sura ya saa kwa kutumia app. Pebble ina rangi tano tofauti ukiwemo nyeupe, nyeusi, nyekundu na grey.

Samsung kwa upande wake inaonekana saa ambayo ni solid ikiwa ni ya stainless steel na mkanda wa sylicone. Hivyo Samsung ni saa ambayo inaonekana ya kiume kutokana na ukubwa. Pia Samsung Galaxy Gear inapatikana katika rangi sita tofauti ikiwemo nyeupe, nyeusi, manjano, kijani na bluu [Gear pointi 5 na Pebble point 4]

Kamera

Samsung ina kamera yenye 1.9 mp na ina uwezo wa kurekodi video za HD, Kamera hii inachukua video fupi za muda usiozidi sekunde kumi kwa sasa. Pebble haina kamera. [Gear point 5 - Pebble point 0]

Prosesa

Pebble inatumia prosesa yenye kasi ndogo sana aina ya ARM Cortex M3 ambapo ina kasi ya 80MHz, hii ina maana kwamba apps na PEbble lazima ziwe hazihitaji nguvu kubwa ya prosesa katika utendaji kazi hivyo itawafanya watengeneza Apps wawe na mambo machahce ya kufanya.

Samsung Galaxy Gear kwa upande wake inatumia prosesa yenye kasi ya 800MHz, hii ni mara kumi ya kasi ya prosesa ya saa ya Pebble. [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble point 2]

OS na Apps

Pepple imetoka na OS yao binafsi ambayo inaitwa Pebble OS wakati huu ni ugunduzi mzuri lakini haitavutia watengenezaji wa apps (developers), Samsung Galaxy Gear inatumia Android ambapo developers wengi watavutika kirahisi kutengeneza apps. Gear imetoka ikiwa na Apps 70 [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble pointi 1]

Sensa na kuunganisha (connectivity)

Pebble ina akselerometa, e-compass na sensa ya mwangaza (ambient light sensor) ambayo inasaidia kudumisha betri ya Pebble. Pia Pebble ina bluetooth 4.0. Samsung ina akselelrometa na sensa ya gyro. Samsung haihitaji sensa ya mwangaza kwa vile inapokuwa haitumiwi saa hivyo inazima skrini mithili ya simu.[Samsung Galaxy Gear pointi 4 - Pebble pointi 5]

Bei

Pebble inauza nusu ya bei ya Gear kwa $150 huku Gear ikiuzwa jumla ya $300. Huu ni udhaifu mkubwa wa saa ya Samsung wengi wakiwa na mtazamo kuwa ni ghali mno. Nike Fuelband ni $150 na Sony Smartwatch 2 ni $150, zote hizi ni bei za Marekani. [Samsung Galaxy Gear pointi 1 - Pebble pointi 5]

Audio na Video

Wakati Pebble haina uwezo wa kutoa sauti au kucheza video Samsung Galaxy Gear ina Video Codec H.264 na inacheza MP4 inarekodi video za HD 720p@30fpsna sauti aina ya AAC na M4A. Pebble inafanya notification tu. [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble pointi 1]

Memory

Samsung ina 4GB disk ambayo ina uwezo wa kuhifadhi mafaili ya sauti, video na picha. Pebble haina disk ya kutumiwa na mtumiaji kwa mafaili yake binafsi. [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble pointi 0]

Maji

Pebble inatumia teknolojia ya IP55 kuzuia maji ambapo unaweza hata kuogelea nayo bila ya shaka yoyote. Samsung inatumia teknolojia ya 5ATM kuzuia maji, yaani unaweza tu laba kuoga nayo au kutembea nayo kwenye mvua lakini huwezi kuogelea nayo. [Samsung Galaxy Gear pointi 2 - Pebble pointi 5]

Utangamano (Compatibility)

Pebble inaweza kuunganishwa kwa teknolojia ya bluetooth na simu yoyote ya Google au iPhone. Galaxy Gear kwa sasa inafanya kazi na Samsung Galaxy Note 3 na Samsung Galaxy Note 10.1 (2014 Edition itakapotoka) tu. Pia Samsung wametangaza baada ya kufanyiwa uboreshwaji wa OS kwenda android 4.3 simu za Galaxy S3, Galaxy S4 na Galaxy Note 2 nazo zitakweza kufanya kazi na saa hii. [Samsung Galaxy Gear pointi 1 - Pebble pointi 5]

Mambo Mengine Muhimu

Samsung Galaxy Gear ina-features nyingi muhimu kama vile uwezo wa kupokea simu na kuongea kwa kutumia saa ambapo mtumiaji ananyanyua mkono na kuuweka karibu na sikio, vile vile ina feature ya smart Relay ambapo unapofungua app fulani kwenye saa na simu pia hufunguka app hiyo hiyo kwenye simu hivyo huna haja ya kufungua app unapotaka kuhamia kwenye simu. Pia Gear ina S Voice, Memographer (Picha) na Voice Memo, vitu hivi havipatikani kwenye Pebble.

Pebble inajitangaza kuwa na uwezo wa notification, alarms, kubadili muonekano wa saa, app za mazoezi na ku-control muziki kwenye simu. Hizi zote zinapatikana kwenye Gear tena kwa ubora zaidi. Mathalani Samsung ina face ambazo zinaonyesha pia na hali ya hewa mbali na saa, Pebble haina uwezo huo, Wakati Pebble ina-control muziki Gear inacheza muziki, video na kurekodi pia. [Samsung Galaxy Gear pointi 5 - Pebble pointi 2]

AQ1

Chati ya Vielelezo

Matokeo
Samsung Galaxy Gear pointi 50/65 = 77%

Pebble Watch pointi 32/65 = 49%

Hivyo Samsung Galaxy Gear ni Saa bora kuliko Pebble.

Ubora wa Gear dhidi ya Pebble: Pebble imeangushwa na Gear kwa sababu 5 kuu: Ina kamera, kasi ya CPU, Microphone inayoruhusu kuongea bila kutumia simu na ubora wa display, ina memory inayoruhusu kuhifadhi picha, video na mafaili ya sauti na inafanya mambo mengi zaidi kama vile smart relay, voice memo, memographer na S Voice.

Ubora wa Pebble dhidi ya Gear: Pebble walikuwa ni wa mwanzo kufanya ugunduzi, inafanya kazi na simu za Android zote pamoja na iPhone kadhaa, unaweza kubadili mkanda na bei kidogo inaridhisha.

Hata hivyo tukizingatia kuwa Pebble ni saa ambayo haikuwa hata na kampuni (imechangiwa kwa mtindo wa crowdsourcing kama kickstart project, hawana budi kupewa pongezi kwa kazi nzuri

Pointi za Gajetek ni maoni yetu binafsi ambapo wengi wanaweza kutofautiana na maoni hayo. Tungependa kujua mtazamo wako na sababu za mtazamo huo ikiwa umetofautiana nasi.

Source: gajetek habari

Huu uzi ulikua mzuri heartbroken haujapata reply mpaka leo ni 2019.

Sent using Samsung Galaxy
 
Back
Top Bottom