Ipi mipaka ya Mkuu wa Wilaya huyu kwanini ana vitisho?

Michael mbano

JF-Expert Member
Apr 4, 2022
820
567
Nimepita mahala ktk wilaya fulani nimeisahau jina ila katika mkoa wa njombe mkuu wa wilaya anahutubia,na mkutano huo umeitishwa ghafla tu ktk siku ya leo ambayo inasemekana ya mazingira duniani.

Wamepita wagambo kuwambia wafanyabiashara kuanzia wakubwa hadi wadogo wafunge waje kumsikiliza.

Haikutosha kaita viongozi wavijiji na vitongoji waongozane na wagambo wakakamate watu wawapige faini au kuwaweka lockup. Halafu kwenye mkutano huo kuna wazee lakini mkuu wa wilaya anatamka kauli si nzuri et mi naita mkutano hamji ninyi wajinga nini? Au niwaweke wote lockup.

Sasa nauliza wanajamvi huyu mtu uwezo wake wa kutenda na mipaka yake ipoje? Mh mkuu wa nchi anateuwaje watu waliyokosa busara mbele ya watu?
 
ungeandika jina la mkuu wa wilaya na jina la hiyo wilaya yake ungesaidia zaidi......Unachoogopa kitu gani? au unatidanganya?
 
Wakuu wa wilaya wengine hawana busara na akili. Kumbuka "the crown does not change the mind"
 
Serikali hii ya majizi ya kura haina uhalali wa umma, ndio maana unaona watu wanatishiwa ili wahudhurie mikutano ya hayo majizi.

Haya ndio madhara ya kuingia madarakani bila ridhaa ya umma. Na huko tuendako kwenda kwenye mikutano ya viongozi itakuwa shuruti kuhudhuria.
 
Na imekuwa shuruti mana alituma wenye viti wa vijiji na migambo nendeni mkakamate weka lockup wasodika.Au faini.
 
Back
Top Bottom