Ipi mashine nzuri yakufulia nguo kwa bajeti ya laki 6?

Gentleman 446

Senior Member
Mar 26, 2021
112
399
Habari zenu, habari zenu tena....

Wakuu wenye uzoefu nisaidieni ushauri ni kampuni gani nzuri au ni mashine gani nzuri yakufulia nguo kwa matumizi ya nyumbani?
 
Usinunue mashine ya kufulia kwa kigezo cha jina, utaumia. Mashine karibia zote zinafanya vizuri mno upande wa ufuaji na huwa zinakufa mapema kwenye upande wa kukamua nguo kwa mashine ambazo ni semi automatic. Ukitaka mashine nzuri nunua semi automatic ya angalau kg 15 kwa bei hiyo utapata Hisense, Zec, SPJ, nk.


Niulize hapa hapa kama kuna pahala hujaelewa.
 
unapoenda duka lolote kununua kitu chochote usijaribu kumuuliza muuzajia au wafanyakazi wake eti ipi nzuri nichukue hii au hiyo, ni kosa na utajuta, wao wauzaji wanalenga vitu visivyotoka sana vinunuliwe au visivyokuwa na ubora ndio vitoke kwanza visiwe mizigo kwao, chakufanya chukunguza kwanza ipi ni bora na ukipata uhakika ndio unaenda dukani kuchukua
 
Mkuu hapa utauziwa kwa hadhi ya majina ya makampuni.
Nenda mpaka kwa wauzaji wa hizo mashine....ingia dukani,declare your interest lakini omba upewe elimu kuhusu brand zilizopo. Usiende kwenye kigezo cha original na brand utapigwa.
duuh jina lako limenifanya niwaze mengi🤣🤣
 
Back
Top Bottom