Ipi Bima bora ya Afya kati ya NSSF na NHIF?

Ipi Bima bora ya Afya kati ya NSSF na NHIF?

Kama upo serikalin ingia NHIF. Nssf unachagua hospital ya kutibiwa bt nhif unaenda hospital yeyote inayopokea bima ya nhif. Tofaut yao ni kuwa nssf ukichagua hospital unaenda hapo hapo hubadirishi bt nhif popote kambi mradi tu wawe wamejisajil huko
 
Kwa mtu binafsi aidha mfanya biashara,mkulima na hata asie na kazi hulipa direct kwa nssf hiyo sh 20000 kwa mwezi.unaweza kujipa kwa mpigo kwa miezi kadhaa.motisha ya mpango huu ni kama pesa yako umeiweka bank.wakati ukihitaji pesa hizo unarudishiwa kama zilivyo mbali na matibabu uliyoyapata.sina hakika kwa walioajiriwa inakuaje.

Are you serious?
Sasa wanafaidikaje wao? Au Sijaelewa maelezo yako?
 
Hivi ukikatwa hiyo elfu 20 kwa mwezi itakuwa na wategemezi wako wangapi?.. Au ni kwa mtu mmoja tuu anaye katwa?
 
Nssf wanayo bima ya afya!mpango wao huo unawafaa sana watu wa kipato cha kawaida.ukiingia nao mkataba unachagua hospital moja kati ya hospital zao teule.malipo yao ni sh 20000 kwa mwezi.fika kwenye ofisi zao mtaa wa jamhuri kwa maelezo zaidi.

Mkuu, kama makato inakuwa ni 20000 kwa mwezi, kwa mtu ambaye kwa mfano mwezi huu alipata huduma yenye thamani zaidi ya kiasi hicho inakuwaje hapo?
 
Mkuu NSSF siyo Mfuko wa Bima ya Afya ni National Social Security Fund Kazi yake ni Mambo ya Pension (Kiinua mgongo)/ Malipo baada ya kustaafu au mambo yoyote ya kijamii kutokana na Faida wanayoipata hizi ziko nyingi kuna PPF,LPF na zimepewa sheria kuwa makato yao katika mshahara yasizidi 10% na NSSF wanakata 10% ambayo ni kubwa mifuko mingine hadi 6% na kumbuka unavyokatwa % kubwa ndipo pesa zinakua nyingi kama uki staafu au Kuacha kazi

NHIF ni National Heath insurance Fund ambayo hukatwa Kusaidia Mwajiriwa kama akiungua au kupata matatizo yoyote ya Kiafya awapo kazini au nje ya kazi na hii huwa ni 4% ya mshahara wako hope utakua umeelewa na hii nayo imegawanyika kutokana na Mshahara kuna wengine wana Kadi za bima za Kijani hawa huchangia pesa nyingi zaidi na Wakiugua wanaweza kutibiwa hadi nje ya nchi.

NHIF ni 3% of basic salary
 
Wana bima ya afya pia ndio.
 
kwa upande wa NSSF huduma ya matibabu wanayoitoa inaitwa social health insurance benefit (SHIB), ni moja katika mafao wanayotoa ya muda mfupi kwa wanachama wao. ili uweze kufaidika na fao hili lazima uwe mwachama wa nssf kwa muda usiopungua miez mitatu. utatibiwa wewe na mwenza wako mke au mume na watoto wanne. mwananchi yoyote anaruhisiwa kujiunga na mfuko ukiwa ktk sekta isio rasmi (informal sector)au sekta rasmi ( formal sector ). kiwango cha chini kuchangia ktk kwa mfuko kwa informal sector ni sh 20,000 kwa mwezi ambapo mbali ya kupata matibabu pia utapata mafao yote yanayotolewa na shirika kama mafao ya uzaz kwa wanachama wanawake, mafao ya kuumia kazini, mazishi , mafao ya kujitoa ,pension ya uzeen na penshen ya warithi. kumbuka kuwa ukichangia kiwango kikubwa zaidi nipo utakapokuja kupata mafao ya uzeen (pension) kubwa zaidi. tembelea ofisi yoyote ya nssf ilio karibu nawe kwa ajili ya kujiandikisha uanachama na kama tayar ni mwanachama nenda kajaze fomu za kujiunga huduma hii ya matibabu na kuchagua hospital unayotaka kutibiwa wewe na familia yako.
 
pia hakuna makato yoyote utakayokatwa kwa kupata huduma hii kutoka ktk michango yako , hii huduma ni katika mafao ya muda mfupi wanayotoa shirika kwa wanachama wao.
 
Are you serious?
Sasa wanafaidikaje wao? Au Sijaelewa maelezo yako?

Im very serious!kwanza mimi ni mwanachama mmoja wapo.lkn tokea nitoe mchango karibu mwaka sasa nimeugua mara moja tu tena malaria.kwahiyo pesa za namna hii na makato mengine huelekezwa kuwekeza kwenye vitega uchumi vingine.faida inayopatikana ndiyo hiyo ambayo unarudishwa pesa yako ukiitaka wakati wowote.ni vigumu kuamini lkn fika kwenye ofisi zao watakueleza.
 
Mkuu, kama makato inakuwa ni 20000 kwa mwezi, kwa mtu ambaye kwa mfano mwezi huu alipata huduma yenye thamani zaidi ya kiasi hicho inakuwaje hapo?

Hata ukitibiwa kwa laki mbili .mchango wako ni 20000 tu kwa mwezi.ni mfano tu wa insurance.unaweza kulipia comprensive sh 200000.lkn gari lako likipata ajali unalipwa pesa ya kununua gari jiya.siri ya wazi ni kwamba wanachama wanaochangia hiyo pesa ni wengi na sio wote wanaougua.
 
Mkuu, nashukuru sana kwa maelezo yako!
 
Naulizia rates za malipo ya NHIF kwa mwaka ni kiasi gani?

Muajiriwa 3% ya basic salary

Asiye muajiriwa 1.5M package ya familia max watu 6

Wanafunzi wa vyuo 50400 kwa mwaka

Watoto under 18 50400 kwa mwaka(Toto Kadi)

Mashirika ya dini nimesahau kidogo

Vikundi vya ujasiriamali 78000 kwa mwaka
 
Hapa kwenye vikundi minimum watu wangapi??
 
Back
Top Bottom