Ipi Bima bora ya Afya kati ya NSSF na NHIF?

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,147
2,630
Wakuu natumai wote wazima,

kama ilivyo kichwa hapo juu, uzoefu wenu unasemaje katika hilo?

Natanguliza shukrani.
 
Mkuu NSSF siyo Mfuko wa Bima ya Afya ni National Social Security Fund Kazi yake ni Mambo ya Pension (Kiinua mgongo)/ Malipo baada ya kustaafu au mambo yoyote ya kijamii kutokana na Faida wanayoipata hizi ziko nyingi kuna PPF,LPF na zimepewa sheria kuwa makato yao katika mshahara yasizidi 10% na NSSF wanakata 10% ambayo ni kubwa mifuko mingine hadi 6% na kumbuka unavyokatwa % kubwa ndipo pesa zinakua nyingi kama uki staafu au Kuacha kazi

NHIF ni National Heath insurance Fund ambayo hukatwa Kusaidia Mwajiriwa kama akiungua au kupata matatizo yoyote ya Kiafya awapo kazini au nje ya kazi na hii huwa ni 4% ya mshahara wako hope utakua umeelewa na hii nayo imegawanyika kutokana na Mshahara kuna wengine wana Kadi za bima za Kijani hawa huchangia pesa nyingi zaidi na Wakiugua wanaweza kutibiwa hadi nje ya nchi.
 
NSSF wana bima zao za afya,,,ukijiunga utapewa mwongozo wa kuipata hiyo bima ya matibabu
ila NHIF bado iko juu kwa kuwa karibia vituo vyote vya afya wamejiunga na mfuko hu
 
Kama vile Ma benki yalivyo na bima zao za afya
NMB. Wanatumia. strategis
CRDB. Wanatumia JUBILEE
Kuna AAR
tanesco nao pia wana bima zao za afya
 
NSSF wana bima ya Afya inaitwa SHIB (Social Health Insurance Benefit).
Unaweza unaweza kwenda tawi lolote la NSSF kuulza makato yake ni jinsi wanavyotoa benefit watakuelekeza ukalinganisha na NHIF!
Au ingia kwny mtandao utapata maelekezo!
 
Nhif iko v izuri mana WaPo hosptal nyingi sana .vipimo vinavyolipiwa na nhif ni vingi sana..vifaa watoavyo mfano magongo m iwani nk..vpmo Mri. .ctscan..nk na dawa watoazo ni nyingi pia maduka yanayopokea nhif ni mengi tofauti na nssf...na hutakiw kuwa nazo zote mbili unatakiwa uwe na Moja tu..
 
Pole sana, hawa ni jamaa wasio na mahusiano hata kidogo.

Mkuu NSSF siyo Mfuko wa Bima ya Afya ni National Social Security Fund Kazi yake ni Mambo ya Pension (Kiinua mgongo)/ Malipo baada ya kustaafu au mambo yoyote ya kijamii kutokana na Faida wanayoipata hizi ziko nyingi kuna PPF,LPF na zimepewa sheria kuwa makato yao katika mshahara yasizidi 10% na NSSF wanakata 10% ambayo ni kubwa mifuko mingine hadi 6% na kumbuka unavyokatwa % kubwa ndipo pesa zinakua nyingi kama uki staafu au Kuacha kazi

NHIF ni National Heath insurance Fund ambayo hukatwa Kusaidia Mwajiriwa kama akiungua au kupata matatizo yoyote ya Kiafya awapo kazini au nje ya kazi na hii huwa ni 4% ya mshahara wako hope utakua umeelewa na hii nayo imegawanyika kutokana na Mshahara kuna wengine wana Kadi za bima za Kijani hawa huchangia pesa nyingi zaidi na Wakiugua wanaweza kutibiwa hadi nje ya nchi.

Nadhani bado mko nyuma kidogo, Serikali imeyaamrisha mashirika yote ya penshen kutoa huduma za afya kwa wanachama wao, ikiwemo NSSF, sijajua kwa mingine kama wameshaanza ila NSSF wao wameshaanza ambao unaitwa
SHIB (Social Health Insurance Benefit).

tukirudi kwenye swali la mleta mada.
kila mmoja ana faida yake na hasara yake.
kwa mfano NHIF wapo kila mahali (nchini) na ukiwa na kadi yako unaweza kutibiwa kwenye hospitali zozote Tanzania
ambayo imejiunga nayo (ambazo ziko nyingi sana)

Bei ya matibabu wameshapa wao kwa hiyo mtoa huduma (hospital) lazima akubaliane na hiyo bei.

NSSF (SHIB) wao unachagua hospitali ya kupata huduma na unafungua faili lako huko, (wao hawana vitambulisho) so kwenye lile faili lako kunakuwa na majina na picha zako pamoja na wategemezi wako. kwa hiyo huwezi kwenda kutibiwa kwenye hospital nyingine zaidi ya ile uliyoichagua, mfano kama umesafiri nje ya mji hutaweza kutibiwa ukiwa huko ulipo, na kama unataka kubadilisha hospital ni mpaka mwaka uishe.

Faida ninayoina kenye NSSF ni wanamwekea mwanachama wake fedha nyingi zaidi ya huduma, kwa hiyo unakuwa na uwezo wa kupata tiba nzuri zaidi.. mf. kwa mgonjwa wa OPD unaweza kutumia sh. 40,000/= kwa mara moja hapo ni mje ya vipimo kama x-rays, ultrasound nk. kwa hiyo unaweza kupata dawa nzuri na huduma bora zaidi.

ukilinganisha na NHIF ambayo kwa mfano dawa ya malaria wanayoruhusu ni ALU ambayo bei yao elekezi ni sh. 1000/= kama sikosei, sasa kama unatumia dawa kama artequine, na zile za bei ya juu kidogo hutapewa.
 
Lakini cha moto.wanna NSSF ukipata wakati WA kustaafu gharama zote hizo hukatwa ktk mafao yako..
 
Ahsante kwa kunijulisha, lkn nina kaswali kadogo, ina maana kama haujatibiwa ukistaafu unakatwaa?
 
Nadhani bado mko nyuma kidogo, Serikali imeyaamrisha mashirika yote ya penshen kutoa huduma za afya kwa wanachama wao, ikiwemo NSSF, sijajua kwa mingine kama wameshaanza ila NSSF wao wameshaanza ambao unaitwa
SHIB (Social Health Insurance Benefit).

tukirudi kwenye swali la mleta mada.
kila mmoja ana faida yake na hasara yake.
kwa mfano NHIF wapo kila mahali (nchini) na ukiwa na kadi yako unaweza kutibiwa kwenye hospitali zozote Tanzania
ambayo imejiunga nayo (ambazo ziko nyingi sana)

Bei ya matibabu wameshapa wao kwa hiyo mtoa huduma (hospital) lazima akubaliane na hiyo bei.

NSSF (SHIB) wao unachagua hospitali ya kupata huduma na unafungua faili lako huko, (wao hawana vitambulisho) so kwenye lile faili lako kunakuwa na majina na picha zako pamoja na wategemezi wako. kwa hiyo huwezi kwenda kutibiwa kwenye hospital nyingine zaidi ya ile uliyoichagua, mfano kama umesafiri nje ya mji hutaweza kutibiwa ukiwa huko ulipo, na kama unataka kubadilisha hospital ni mpaka mwaka uishe.

Faida ninayoina kenye NSSF ni wanamwekea mwanachama wake fedha nyingi zaidi ya huduma, kwa hiyo unakuwa na uwezo wa kupata tiba nzuri zaidi.. mf. kwa mgonjwa wa OPD unaweza kutumia sh. 40,000/= kwa mara moja hapo ni mje ya vipimo kama x-rays, ultrasound nk. kwa hiyo unaweza kupata dawa nzuri na huduma bora zaidi.

ukilinganisha na NHIF ambayo kwa mfano dawa ya malaria wanayoruhusu ni ALU ambayo bei yao elekezi ni sh. 1000/= kama sikosei, sasa kama unatumia dawa kama artequine, na zile za bei ya juu kidogo hutapewa.

Duh Mkuu, nashukuru sana kwa kuipa nyama ya kutosha katika kutofautisha faida na hasara. Kifupi nimejifunza mengi.
 
Nhif iko v izuri mana WaPo hosptal nyingi sana .vipimo vinavyolipiwa na nhif ni vingi sana..vifaa watoavyo mfano magongo m iwani nk..vpmo Mri. .ctscan..nk na dawa watoazo ni nyingi pia maduka yanayopokea nhif ni mengi tofauti na nssf...na hutakiw kuwa nazo zote mbili unatakiwa uwe na Moja tu..

Ukijiunga zote mbili inakuwaje?
 
NSSF wana bima ya Afya inaitwa SHIB (Social Health Insurance Benefit).
Unaweza unaweza kwenda tawi lolote la NSSF kuulza makato yake ni jinsi wanavyotoa benefit watakuelekeza ukalinganisha na NHIF!
Au ingia kwny mtandao utapata maelekezo!

Nashukuru sana kwa maelezo yako...nitalifanyia kazi
 
Mkuu NSSF siyo Mfuko wa Bima ya Afya ni National Social Security Fund Kazi yake ni Mambo ya Pension (Kiinua mgongo)/ Malipo baada ya kustaafu au mambo yoyote ya kijamii kutokana na Faida wanayoipata hizi ziko nyingi kuna PPF,LPF na zimepewa sheria kuwa makato yao katika mshahara yasizidi 10% na NSSF wanakata 10% ambayo ni kubwa mifuko mingine hadi 6% na kumbuka unavyokatwa % kubwa ndipo pesa zinakua nyingi kama uki staafu au Kuacha kazi

NHIF ni National Heath insurance Fund ambayo hukatwa Kusaidia Mwajiriwa kama akiungua au kupata matatizo yoyote ya Kiafya awapo kazini au nje ya kazi na hii huwa ni 4% ya mshahara wako hope utakua umeelewa na hii nayo imegawanyika kutokana na Mshahara kuna wengine wana Kadi za bima za Kijani hawa huchangia pesa nyingi zaidi na Wakiugua wanaweza kutibiwa hadi nje ya nchi.

Nssf wanayo bima ya afya!mpango wao huo unawafaa sana watu wa kipato cha kawaida.ukiingia nao mkataba unachagua hospital moja kati ya hospital zao teule.malipo yao ni sh 20000 kwa mwezi.fika kwenye ofisi zao mtaa wa jamhuri kwa maelezo zaidi.
 
Mkuu unamaanisha unakatwa 20000 kila mwezi au maana navyoelewa hakuna makoto ya ziada kwa huduma hii kwakuwa hiki ni kivutio tu.
 
Kwa mtu binafsi aidha mfanya biashara,mkulima na hata asie na kazi hulipa direct kwa nssf hiyo sh 20000 kwa mwezi.unaweza kujipa kwa mpigo kwa miezi kadhaa.motisha ya mpango huu ni kama pesa yako umeiweka bank.wakati ukihitaji pesa hizo unarudishiwa kama zilivyo mbali na matibabu uliyoyapata.sina hakika kwa walioajiriwa inakuaje.
 
Back
Top Bottom