Nadhani bado mko nyuma kidogo, Serikali imeyaamrisha mashirika yote ya penshen kutoa huduma za afya kwa wanachama wao, ikiwemo NSSF, sijajua kwa mingine kama wameshaanza ila NSSF wao wameshaanza ambao unaitwa
SHIB (Social Health Insurance Benefit).
tukirudi kwenye swali la mleta mada.
kila mmoja ana faida yake na hasara yake.
kwa mfano NHIF wapo kila mahali (nchini) na ukiwa na kadi yako unaweza kutibiwa kwenye hospitali zozote Tanzania
ambayo imejiunga nayo (ambazo ziko nyingi sana)
Bei ya matibabu wameshapa wao kwa hiyo mtoa huduma (hospital) lazima akubaliane na hiyo bei.
NSSF (SHIB) wao unachagua hospitali ya kupata huduma na unafungua faili lako huko, (wao hawana vitambulisho) so kwenye lile faili lako kunakuwa na majina na picha zako pamoja na wategemezi wako. kwa hiyo huwezi kwenda kutibiwa kwenye hospital nyingine zaidi ya ile uliyoichagua, mfano kama umesafiri nje ya mji hutaweza kutibiwa ukiwa huko ulipo, na kama unataka kubadilisha hospital ni mpaka mwaka uishe.
Faida ninayoina kenye NSSF ni wanamwekea mwanachama wake fedha nyingi zaidi ya huduma, kwa hiyo unakuwa na uwezo wa kupata tiba nzuri zaidi.. mf. kwa mgonjwa wa OPD unaweza kutumia sh. 40,000/= kwa mara moja hapo ni mje ya vipimo kama x-rays, ultrasound nk. kwa hiyo unaweza kupata dawa nzuri na huduma bora zaidi.
ukilinganisha na NHIF ambayo kwa mfano dawa ya malaria wanayoruhusu ni ALU ambayo bei yao elekezi ni sh. 1000/= kama sikosei, sasa kama unatumia dawa kama artequine, na zile za bei ya juu kidogo hutapewa.