mzenjiboy
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 907
- 387
Ikiwa kuna mtu au watu wanakusumbua kwa kukutumia msgs au kukupigia simu za kukukera basi watu wa aina hiyo unaweza kuwazuia, yaani unawa-BLOCK.
Unaanza na Settings kisha Phone, ukibinya hiyo Phone itafungua page nyengine utaona Add New.
Ukibinya Add New itajitokeza contact list yako yote, hapo utachagua ni nani na nani unataka kumzuia (BLOCK) kisha unabinya jina lake na inakuwa tayari mtu huyo umeshamzuia, yaani BLOCKED.
Ama ikiwa unataka kumfungulia unaanza Settings kisha Phone. Ukibinya Phone na page inayofatia utaona Blocked, ukibinya Blocked kutajitokeza jina au majina ambayo umezuia.
Cha kufanya hapo unabinya Edit kisha itajitokeza alama nyekundu kwenye jina na hapo unabinya hiyo alama nyekundu, kisha panakuja neno UNBLOCK.
Ukibinya hiyo UNBLOCK itakuwa umeshamfungulia yule ambae ulikuwa umemfungia.
Enjoy your iPhone.