IPHONE:nini faida na hasara

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Posts
3,824
Reaction score
2,079
Wadau napenda kuuliza kuna faida gani au hasara gani kama nita-Jailbreack iphone yangu??????
 
Bado unatumia dah tushakukosa.husikii tim cook kishajitangaza.

Kama ni Ushoga hapa TZ upo mwingi sana Zanzibar na Tanga ndo usiombe mpaka madaktari sijui utakataa wasikutibu mpaka waalimu sijui mtoto wako utamzuia asisome.
 
Wadau napenda kuuliza kuna faida gani au hasara gani kama nita-Jailbreack iphone yangu??????

Kwani ukiiacha hivyo hivyo kuna tatizo gani? Kwa kiwa hujui hata sababu za kujailbreak si uendelee kuitumia hivyohivyo?
 
Ndiyo maana nikauliza kama kuna hasara au faida ku-Jailbreak,kama una ufahamu nijulishe tu.
 
Wadau napenda kuuliza kuna faida gani au hasara gani kama nita-Jailbreack iphone yangu??????

Sidhani kama ina hasara...sana sana utakua umeongeza wigo wa kufanya tweaking nk

Ila ikiharibika within the procesa warranty haitafanya kazi...lakini kwa Africa especially TZ hakuna agent wa Apple atakae weza kukurudishia mpya,therefore ni heri uharibu kikweli kweli tu anyway

Infact hakuna tatizo ili mradi uwe very knowledgeable usiiharibu
 
Ndiyo maana nikauliza kama kuna hasara au faida ku-Jailbreak,kama una ufahamu nijulishe tu.

Faida ni kudownload apps ambazo zinauzwa hasara wakati wa kuupgrade os ukikosea kidogo unaweza ukaitupa simu
 
Kwani ukiiacha hivyo hivyo kuna tatizo gani? Kwa kiwa hujui hata sababu za kujailbreak si uendelee kuitumia hivyohivyo?

Ku-Jailbreak ni deal sana mwana...as utapata wigo mkubwa sana wa tweaking na kufanya mambo makubwa zaidi ya yale allowable na Apple

Apple wanatumia closed system ,uki jailbreak unakua free kuifanyia manjonjo way above imagination
 
Bado unatumia dah tushakukosa.husikii tim cook kishajitangaza.

Mkuu Tim Cook ni mtu binafsi na ushoga ni mambo yake binafsi...siwezi acha kutumia Apple products sababu tu anaijenga ni gay au straight

Huwezi kusema kwenye viwanda vya Samsung au Nokia au Sony hakuna mafundi gays...huenda wapo pia
 
Ila Tim Cook katuzengua sana...inakuaje mtu anatangaza mambo yake binafsi hadharani?
It dont make any sense.

Ni kama straight person atoke public kwenye national television aseme im proud to be straight person,halafu tukusaidie nini sasa?

Mijitu mingine bwana...kuyaelewa ni very hard
 
Mimi nawashangaa watu wengine sana,Mada iliyoko ni faida au hasara ya ku-jailbreack sasa watu wanaanzisha mambo ambayo si MADA yangu sijui niwaeleweje mimi sijui wamemwonea wivu jamaa kwa sababu yeye amewawahi kujitangaza kwa kweli hii haipendezi.Bora kama hujui au huelewi kaa kimya,mimi hapa nimeomba kusaidiwa ili nijue.
 

Mkuu Echolima,hii post yako quoted hapa sijakusoma kabisa?

Kumuonea wivu kivipi?

Unajua huwezi kutaka Apple products bila kuwataja Tim Cook au Steve Jobs,right?Na huwezi kumtaja Tim Cook bila kua attach gayism kwake.Ni kitu natural kabisa.

Sasa unapoanza kujibu watu kwa kibri namna hiyo na kusema eti "wanamuonea wivu coz ka-come out" ni disrepect na insult kwa wachangiaji hapa.

Mchangiaji ni mchangiaji tu,atoe point au uchafu...huna haki ya kuwa label eti ni gays.

Watu wametoka nje ya mada warudishe vizuri,sio kuwaita gays.

Maafaka hujui Jailbreaking na bado walewale unaonataka wakueleweshe unawaita gays?

Have respect to people,sio una-run around like the biggest mofo than Tim Cook himself
 
Mleta mada kuomba msaada wa faida na hasara za jailbreak, kama unajua msaidie kama hujui kaa kimya, kuna mada humu kibao za kumhusu Tim Cook ni bora ukaenda huko kujadili au ni bora ukaanzisha mada inayomhusu Tim Cook
 
Mleta mada kuomba msaada wa faida na hasara za jailbreak, kama unajua msaidie kama hujui kaa kimya, kuna mada humu kibao za kumhusu Tim Cook ni bora ukaenda huko kujadili au ni bora ukaanzisha mada inayomhusu Tim Cook

Waheed,unachosema ni sawa ila jamaa katoa sentensi mbaya sana ya ku-group everyone kwenye group eti gay..

Kuna shida gani yeye kurun thread vizuri bila kutukana watu?

Na hii mtu kujifanya kufungua thread nakuona ana mandate ya kutukana watu wanaotoka nje ya mada kwasababu moja au nyingine sio sawa
 
Samahani kwa wote niliowakwaza nimetengua kauli yangu turudi kwenye MADA husika.
 
Narudia tena SORRY kwa yeyote aliyekwazika kutokana na kauli yangu na mimi siku-group watu,mimi nia yangu ki kujulishwa tu faida na hasara ya ku-jailbreack iphone tu mambo ya Gay i have nothing to do with them.
 
Huyo mbufi Cook ni just a CEO infact siamin sana kama ana mchango technical sana kwenye Product za Apple. Vitu vyote Steve Jobs alishaviset ,so huyu mbufi hanizuii kutumia product ambazo genius S.Jobs alitumia muda wake mwingi kuinvent
 

Mkuu punguza ukali wa maneno, kama hivyo kusingekua na mjadala hapa jf maana wote wangekua wanachangia kwa muono wa mleta mada.
 
Leo watu hawajatenda haki maana wameshaharibu MADA yangu kwa kuingiza mambo ambayo si ya maana,mimi nina kifaa cha Apple yananihusu nini mambo hayo???na kwa nini wengine wanachangia tofauti???? Yaani wanatoka nje ya MADA nilitarajia utawakemea hao waliochafua UZI wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…