Habari za leo wanajamvi,ninayo furaha sana kuwajulisha kuwa hatimaye simu yangu iliyoibiwa nimeipata Iphone yangu hiyo iliibiwa kwenye tukio la kutumia nguvu huko Mleba tarehe 11 june 2015 baada ya jamaa kuvamia nyumba ya kulala wageni na kuanzisha sanya-sanya kila chumba baadaye kutokomea kusikojulikana niliumia sana kwa Iphone yangu kuchukuliwa,Bahati nzuri nilikuwa nimei-lock kwa icloud,na baada ya kuibiwa nilitoa taarifa humu jamvini na nikapata watu wa kunielekeza namna ya kuifuatilia kwa sababu nilikuwa njiani kuelekea DRC nilienda safari hiyo na niliporudi nilipata pc nika login
www.icloud.com nikaenda FIND MY IPHONE nikakuta vifaa vyangu vyote yaani IPAD NA IPHONE iliyoibiwa na pia nikakuta option tatu za kufanya kwa iphoe iliyoibiwa 1.PLAY SOUND 2.LOST MODE 3.ERASE IPHONE na kuna rangi ya green kuonyesha siphone iko wasi na wapi iliko simu hiyo ilionyesha iko Nzega,nje kidogo ya nzega jana asubuhi nilisafiri kwenda nzega asubuhi nilifika nikafanya mipangilio yote na baadaye tukaelekea kufuata ramani inakotuelekeza tukafika maeneo ya Kitangili nilipowasha pc yangu kuangalia kama tupo karibu na huyo aliye na hiyo simu hiyo rangi ya green ikaonyesha tumepishana kumbe mwenye hiyo simu alikuwa ameamua kwenda mjini tulikaa hapa kitangili kama saa moja hivi nilipowasha pc yangu ilionekana wazi kuwa yuko mjini tukaamua kurudi mjini na sokoni ramani ilionyesha vizuri kabisa mpaka tukafika kwenye ile nyumba iliyokuwa inaonyesha ile green kuonyesha ilipo ilibidi kuongeza watu ili tuweze kuibaibi kwa urahisi baada ya kuwa watu 7 kwenye pc yangu nilibonyeza kwenye option namba moja ya PLAY SOUND ile iphone ilianza kutoa mlio ambao ulisababisha sisi tujue iko wapi na jamaa huyo alipatikana maana hakuweza kuizima hiyo sauti alikuwa anajribu kuizima lakini mlio uliendelea tu mpaka tukamtia mbaroni,na mpaka sasa hivi jamaa yuko ndani na kuna uwezekano wa kupelekwa Muleba,kwa ujumla nimependa sana kuiona simu yangu ingawaje polisi tena hawakuniruhusu niichukue hapa sasa sijui itakuwaje ngoja kesho nitajua zaidi nikienda kituoni.Nawashukuru sana
Paul S.S stephot Jerrymsigwa