Mkuu nawezaje tambua FAKE s2 galaxy?
mkuu unachotakiwa wewe ujue ni operating system ya galaxy s2 ambayo ni ANDROID.
Ukishajua hii ni android hutapata shida sio galaxy s2 tu utaweza kujua samsung, htc, lg, huawei, zte na sony fake na original.
utajuaje kama simu inatumia android au haitumii?
1.muonekano.
Muonekano wa android unajulikana na hili utalijua kwa kutumia experience kama umeshatumia simu nyingi za android then ukiona simu fake ya android hapo hapo utajua hii ni fake kutokana na muonekano ni tofauti. Njia hii si nzuri kwa mtu wa mara ya kwanza android.
2. Built in apps.
Android ikija na simu kuna application ambazo zinakuja na hio android. Mfano wa application hizo ni google play. Kwa hio ukishika simu ya android mfano hio galaxy s2 we tafuta app inaitwa google play then click utapelekwa store sehemu ya kudownloadia apps. Kama hamna google play au ipo lakini ukiclick hupelekwi store then hio fake
3.google acount
simu ya android inakua na google acount ambayo ni lazima uweke ili kutumia ecosystem ya google kwenye android. Google acount hutumika kwenye vitu vingi kama kusync contact, huwezi kudownload playstore bila google acount na vitu vyengine. Kama huoni option yoyote ya kueka acount possibility ni fake.
4.about phone.
Kwenye android ni rahisi kujua details za simu ukienda setting then about phone utaona details za simu. Mfano kama ni galaxy s2 utaona na version yake 2.3 na kama kuna update pia utazipata huku. Ni vigumu hivi kuekwa kwenye s2 fake.
Kitu vyengine vya kugundua simu fake ni
build quality mara nyingi simu fake zinakua na kioo cha resistive na sio capative. Resisitive screen inagusika na kitu chochote na ipo kama kapeti.