iPhone 11... kuvunja rekodi?

Mkuu umetumia galaxy S10? Jee kwa alicholeta jana apple na kwa maoni yako Galaxy S10 plus vs iPhone 11 pro max yupi yupo better?

Kwa maoni yangu samsung ana well made phones nyingi tu in the market.
Ni ngumu kuja na sensible conclusion kati ya simu yenye miezi minne sokoni na nyingine ambayo haijafika mikononi kwa watu.

On paper, Galaxy S10 is the best ila kwenye user experience i think Inategemea na preference ya mtu kwenye hardware na software.

Binafsi sipendelei Android kabisa. So there is no way nikaipa nafasi S10.
 
Walipenda waweke kwenye simu zao sema waliitilafiana na qualcomn kwenye masuala ya modem qualcomn akagoma kumuuzia hzo modem ambazo ndo zina support 5G ikabid wanunue modem kwa intel ambazo hazina support ya 5G bado.hayo mengine ni maneno tu.
Huyo jamaa anajitetea hajui kua watu wanajua alitamani kuweka ila mgogoro na quacomm ndio umesababisha washindwe, eti roll out haijawa kubwa.

Apple sasa atapitwa hata na tecno. Huko marekani watu wanatrade iphone kwenda android.

Imetoka cnet wakala wa apple anakiri mauzo ya simu ya Iphone yanadondoka kila siku sababu ya ukosefu wa ubunifu na bei ghali. Wewe ununue simu 3m alafu video ya 1080 huwezi kuangalia karne hii ya 21, si maajabu?
 
But rumors zilikua hivyo na inawezekana kabisa walikua na mpango huo wakaacha! Hii shape tuloiona jana akina techradar waliileta tangu March na imekuja kweli.
Mara nyingi hata wao wanazileak hizi shape kuangalia maoni ya watu wanasemaje.

Hata google pixel 4XL wameshaleak itafananaje, na uzuri zaidi inakuna na 90 HZ refresh rate.

Hii ndo simu ya Android nai admire sana. Inakuja na stock android sio hizi nyingine wanajaza skins juu ya custom android.
 
Na apple wameshajua wana wateja wa aina gani ,so wanafanya vile wanajiskia coz wanajua wateja wao watapenda tu
 
Mkuu tuache utani... ktk design Samsung hana mpinzani!! Napenda sana apple ila hii design ya mwaka huu naungana na reviewers wengine kwamba haijanibariki. Better nibaki kwa XS max.

Wengine ktk simu ukiacha yote tunapenda designs.
Apple sahivi wapo slow sana kubadili designs.

Nakubali bila shaka, kwenye design hakuna kama Samsung.

Ila tatizo langu ni Android tu. Basi.
 
Mkuu hili la perfomance nimeprove kwenye iphone 8 plus!! Kwa kadiri nilivyokua na update ndipo performance inashuka hata kwa battery life!!
 
sasa kufananisha techno na iphone unakosea sana. Tecno hatengenezi flagship
Tecno huuzia watu simu zao mbovu za mediatek kwa bei ghali sana, kwa ujumla huwapiga wateja wao, ndicho anachokifanya Apple, kuuzia watu simu ambazo ziko 3 years technologically backward kwa bei ghali wana tofauti gani?

Leo unazindua simu zenye 4k camera, teknolojia iko sokoni miaka 4 wana tofauti gani na tekno
 
Mkuu hili la perfomance nimeprove kwenye iphone 8 plus!! Kwa kadiri nilivyokua na update ndipo performance inashuka hata kwa battery life!!
Sijakataa kama perfomance inashuka, it is just me sijanotice na huenda ikawa kwa sababu nimeacha kuwa heavy user, ndani ya iphone sijaeka hata game moja. All i know is battery life ni mbovu na kwa sababu tayari nimebadilisha betri. Kwaio, kama wamepunguza perfomance, siamini kuwa ni kwa sababu ununue new phone, but wamejua kuwa OS yao, itaathiri vibaya previous devices zikiachwa zirun full capacity. You never, know, unaweza kuta simu inapata moto sana n.k
 
Kuna maana gani kupata new update huku perfomance ikishuka? Si heri anaetoa 2 years then ukafanya manually na mzigo ukawa poa?

Mkuu kuna samsung S2 imewekewa Oreo inapiga kazi vizuri tuu...

Sasa why leo apple atudanganye kwa updates zake huku matoleo ya nyuma yakielekea kuwa toys?

 
Angalia hizi comments mkuu....

Mwakani wanaweza wasilete vyote.

Nina uhakika watabadili aina ya kuchaji, apple hawataki kucopy, itakuwa wana design aina mpya ya charging na wanaifanyia majaribio ndio maana hujaiona wanaileta.
 
Tofauti ni Quality
 
So
Africa hakuna carrier ambaye amesha launch 5G.

Huko ulaya na marekani ni sehemu chache sana wameshalaunch na still haioneshi mafanikio.

Hata kwenye spot moja kuna upande unaweza pata 5G na mwingine ukakosa kabisa.
Soko kubwa la iPhone liko Africa siyo? Nijuze mkuu sababu huko mwingine kuna 5G kwani hawatengenezee hao kama wengine walivyofanya
 
Sio kila updates inahitaji kuongeza perfomance, updates huwa zinaleta new features au zina fix bugs. Sijui kama mnaelewa umuhimu wa simu kuendelea kuwa supported.

Tujaalie kuwa una iphone 7 yako ina IOS 10, huku na kule kuna ishu with IOS 10, Apple wanatoa IOS 10.1 kufix ile ishu, na wewe moyoni unapiga ofyeee.

Halafu tujaalie una S2, ambayo Samsung wameacha kuipa updates. umeweka Android 6 tuseme. ilikuja ikagundulika kuwa ile Android 6 kuna ishu inazingua na ishu yenyewe sababu ni Samsung walivomodify codes. Sasa Samsung kashaipotezea zamani, unaanza kuhangaika na third party sources halafu unakuja kujisifu kuwa nina S2 ina run latest software, kwa kutumia 3rd Party source kitu ambacho una risk saftey ya privacy yako?


mmekariri kuwa kila update lazima perfomance izidi, for me nafikiri update ya ios 13 ni mzigo kwa iphone 6
 
Maana ya update ni nini mkuu? Kama si kila update iboreshe zaidi software kazi nyingine ni nini?

Haha, kwahiyo tusikariri kuwa lengo la update huwa ni maboresho?
 
Maana ya update ni nini mkuu? Kama si kila update iboreshe zaidi software kazi nyingine ni nini?

Haha, kwahiyo tusikariri kuwa lengo la update huwa ni maboresho?
Usikariri kuwa maboresho ni spidi tu. Maboresho yanaweza kuwa UI, maboresho yanaweza kuwa Security tu, Maboresho yanaweza kuwa perfomance...

Wewe kama mtumiaji wa smartphone, utaona kwenye kufanya updates, utakuta nini wana update. Vile vile hio hio update inaweza ikawa source ya new vulnerabilities kujitokeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…