Habari wana jf, Kama thread inavyojieleza ni kwamba nataka kununua ipad 4 au samsung galaxy note 10.1, naomba wa ambae ameishatumia hizi gadgets au anayezifahamu vizuri anielezee ipi ni nzuri interms of quality of picture and video, speed, free apps from store, battery life, camera, etc, nitashukuru sana kwa msaada wenu kwani utaniwezesha kununua kitu sahihi, hasa napenda nijue ni ipi kati ya hizo ambayo ina apps nyingi za bure.
1. kitu kikubwa kinachoboa kwenye iPad ni kwamba huwezi kupiga wala kupokea simu au sms kama kwenye simu za kawaida. Hii inaleta shida sana wakati wa kuongeza vocha inabidi utoe line kwenye simu alafu urecharge kupitia simu ingine ndo urudishe kwenye iPad. Applications zingine kama whatsapp na viber zinazohitaji uwezo wa simu zinakuwa hazisupport kwenye iPad. Otherwise itakulazimu uJailbreak!
2. Kingine ni kwamba iPad haziingizi memory card hivyo inakuwa shida kufanya expansion ya storage.
3. iPad haina USB Host support ambayo ni muhimu kuwezesha kuchomeka (flash disk, mouse, keyboard, powered external hard disk etc) kwenye device yako.
4. Applications nyingi za Note 10.1 ni bure na unapata a full version 'photoshop touch' kwenye tablet yako.
5. bei ya iPad 4 ni kubwa sana almost twice bei ya note 10.1 ( 1.1mil for Note 10.1 'samsung store' wakati iPad 4 inafika mpaka 1.8mil)
6. Uwezekano wa kushare data na device zingine kupitia Bluetooth ya Note 10.1 (iPad ni kwa Apple devices otherwise through Jailbreak), na pia Note 10.1 inakuja na ir port inayokuwezesha kutumia remote ktk devices kama Tv, Radio, etc..
7. Android 4.2.2 Jelly Bean ni nzuri sana ina features nyingi ukilinganisha na IOS, na inaruhusu customization kibao kwakuwa ni open source.
8. Camera zote ni 5MP although zinatofautiana features.
9. Battery ya Note 10.1 ina nguvu sana (1500hrs of standby time ukilinganisha na 720hrs of iPad's) pia ina talk time kubwa of about 33hrs compared to 9hrs za iPad.
10. Note 10.1 ni nyembamba na nyepesi zaidi ukilinganisha na iPad 4.
11. Kioo cha iPad kina resolution kubwa kulinganisha na Note 10.1.
12. Browser ya Note 10.1 inaSupport Adobe Flash hivyo inasaidia kuplay flash contents papo kwa hapo unavyoBrowse internet.
13. Note 10.1 inakuja na S Pen stylus stick (nzuri kuchorea, signature, navigation na kwa mambo ya Artistic).
14. Note 10.1 ni rahisi kutransfer data from computer to tablet na kuzipangilia kama unavyofanya kwenye computer ofisini au nyumbani kupitia file manager (iPad ni lazima uJailbreak ili kupata iFile). iPad syncronisation ni ngumu na maranyingine unaweza ukadelete data zako accidentally kwasababu syncronisation inahitaji utumie computer moja tu otherwise ufanye transfer backup kwanza ndo usync!
15. Note 10.1 inaruhusu kuExplore root directory inayosaidia kuUpload chochote kutoka kwenye simu na kuDownload chochote kwenda kwenye simu (eg. Torrent files, files with various extensions wakati iPad inadownload compatible extensions tu (.ipa,.pdf,,),
All in all zote ni nzuri lakini nadhani Samsung Galaxy Note 10.1 ina Specification za kisasa zaidi na hutoboreka kuitumia. Its loaded!