acha ujinga, wapigie simu waambie uko kagera na hauwezi kufika waangalie uwezekano wa kuhamishia interview tarehe ingine (uitaje) au kama wanaweza wakakufanyia kwa njia ya simu. we vipi wewe.
Mkuu hilo linawezekana likafanyika kwa ivo ikiwa watafuta kazi ni wengi? Minimeona acha niaje ivo kwa kushindwa kwangu ambayo inaweza ikawaongezea nafasi ya kupata kaz kwa watakao fika.
Huyu jamaa anawazingua,kuna mambo nilikua nayafuatilia UTT,wakaniambia ndo kwanza deadline ya kupokea maombi ilikua tarehe 23/feb,kwa kifupi bado hata hawajaanza kupitia application zenu.
Mkuu tu wengi lakini tunatofauti, binafsi siwezi danganya adhara kwani sinafaida yoyote ikiwa wameita au hawajaita zaidi nami nimuanga wa ajira na niliomba pia. Nimepgiwa simu kwa 0222136974, wakaniambia usaili utafanyika ukumbi wa UCC Udsm kuanzia saa 2 kamili ya tar 14 means jumamosi ya kesho. Ivo tusiwe tunapenda kukanusha vitu tusivyojua na hata huyo uliemuulza akakujbu hilo pengne alikujbu kuondoa usumbufu.
Nimefika UCC kwa interview! Do MTU nyomi kama 100 sijui wanawafanyiaje interview wrote hawa so tutakesha hapa
akanana mugazaa..iwee...shiulienda kulaa senene.Wana JF, polen kwa majukumu, mwenzenu nilipigiwa simu jana saa 12 jion yaan saa 1 kasoro hivi ya kunitaka kufika katika interview ila bahati mbaya iliyoje nimekwama nauli kwani nipo mbali sana Kagera na nimekuja kumsalimia ndugu yangu najuta hata sijui kwanini nilikuja huku ila ni mipango ya Mungu tu na niliomba nafasi mbili tofauti na nimebahatika kupigiwa simu kwa nafasi zote. Nichukue nafasi kuwatakia kila la kheri wale wote walioitwa na watakaobahatika kufika.
akanana mugazaa..iwee...shiulienda kulaa senene.
Wana JF, polen kwa majukumu, mwenzenu nilipigiwa simu jana saa 12 jion yaan saa 1 kasoro hivi ya kunitaka kufika katika interview ila bahati mbaya iliyoje nimekwama nauli kwani nipo mbali sana Kagera na nimekuja kumsalimia ndugu yangu najuta hata sijui kwanini nilikuja huku ila ni mipango ya Mungu tu na niliomba nafasi mbili tofauti na nimebahatika kupigiwa simu kwa nafasi zote. Nichukue nafasi kuwatakia kila la kheri wale wote walioitwa na watakaobahatika kufika.
Kwa waliofika, zilizofanyika ni written or oral Interview ?? Nahisi kuna nafasi nyeti ambazo wagombea wake ni wachache wao hawanaga written, hazijaitwaaa