Interview na kupata kazi

Interview na kupata kazi

MICHOH

Member
Joined
Dec 3, 2014
Posts
15
Reaction score
5
Habari za asubuhi jaman. Kuna kitu kinaniboa Sana nchi hii, yaan mtu unaitwa interview una uhakika umefanya vizuri halafu mwisho wa siku kimya halafu unasikia mbona watu wapo kazini
Jaman hii nchi watu tusio na watu kwenye system Tunatoka lin?
Lingine nafasi 5 mnaitwa watu elfu 1000 halafu mnatumia nauli mwisho wa siku mnasikia zile nafasi zilikuwa na watu mlikuwa mnafanya usahili kama ushahidi tu.
Jaman tunahitaj mabadiliko system mbovu yani kama hii Hali itaendelea maana yake walionacho watazidi kuwa nacho na wasio nacho watazidi kukandamizwa..
Fanya maamuz sahihi chagua mtu atakayeweza kuondoa system hii iyooza
Naomba kuwasilisha.
 
ukifanya interview sio lazima upate..kuna kupata na kukosa
 
Tafuta kadi ya kura October tuwatoe hao wezi
 
Be strong mdau, never lose hope watu wana mafolder ya applications walizo tuma yet hawajapata kazi bado so be strong again kumbuka unazidi kupata experience za interview tofauti about Nauli n other cost zinazopotea usijali utakuja kusahau yote hayo once ukifanikiwa. Nakutakia kila la kheri Mhanga mwenzangu!!
 
Unajuaje umefanya vizuri? Unajipa mwenyewe?!! walokuita ndiyo wanakupima mkuu,yawezekana ww ukafanya vizuri wenzako wakafanya vizuri zaidi
 
Ukiitwa kwenye interview na ukakosa kazi kuna mambo mengi
1. Hujakizi vigezo vyao
2. Riziki haikuwa yako
3. Na wao ndio wapangaji sio wewe kusema tu sijapata sijapata, je kama walikuwako wazuri zaidi yako?
(lazima utambue tunatofautiana kiuwezo mkuu)

Pili unapoitwa ukakosa
1. Unaongeza uzoefu wa interview
2. Unaongeza uhusioano na watu mbali mbali hasa hao wanaoendesha interview...
(akikuona mahali pengine ni rahisi kukukumbuka na kushirikiana nawe mambo kadhaa)
3. Shukuru kwa kila jambo
4. Mlango mmoja ukifunga mwingine utafunguka tu.
Nitakuwa nimekusaidia kwa njia moja ama nyingine.
 
Back
Top Bottom