International passport


Bila kutoa chochote kama jadi yetu hiyo time limit itakufikia kabla hujaitia mkononi hiyo pasipoti.
 
Mkuu Chimunguru, pole sana! Nafikiri usikate tamaa maadam ushavulia maji nguo!
 

Hiyo pesa umeliwa tu. Muda utakaopotea na nguvu ulizotumia ni bora mambo yote ungefanya kihalali tu.
Mimi kwenye ofisi ya serikali sitoi rushwa. Sioni kwanini nitoe rushwa iwapo kila nyaraka halali ninazo. Mmoja akinisumbua, naenda kwa mwingine, au hata naulizia kwa bosi wake. Mtu analipwa mshahara kwa kodi yangu, halafu bado nimpe rushwa zaidi? Labda kama hicho kitu ninachokitaka au hiyo huduma sio halali yangu ndio nitatoa hela ya chai.
 
if u have all the supporting documents inawezekana kabisa.....
 

lizzy hapo kwenye nyekundu ndio ugomvi wangu kila siku:nono:
 

Ni aibu kwa kelwi kwako na kwa nchi yako kueleza haya. Rushwa huwa hairahisishi mambo ungefuata utaratibu wa kawaida ungekuwa umepata passport. Kuna fundisho katika post yako. Mie nadhani uhamiajia wame improve sasa hivi kuliko huko nyuma kabla hawajaanza kutioa passport mpya. Yaani inawezekanaje wewe kazi inayotakiwa kufanyika katika ofisi ya serikali ukafantie dukani. Jamani Watanzania ujinga wetu utatumaliza. Ni aibu saana nadhani hata wewe mwenyewe ukisoma haya maandiko yako unayaonea haya. Eti ukampe mtu rushwa. hebu tuache huu ujinga. Nenda kaulize wanata vielelezo gani. Kamilisha vielelzo kisha peleka halafu uone kama utaombwa rushwa. Yaani umeniharibia siku yangu kwa kweli.
 
Infaal, kimjini mjini mambo yanaenda.
Passport hata siku moja ni nyingi. Kama unashida utafanyaje? Ni swala la kujua unayempa hiyo kazi.
100K unakamata siku hiyohiyo. Unampa hiyo hela, atajua kama atalipia formu au hatalipia, wewe unaingia unajaza form unaweka docs na unapiga alama za vidole, then unatafuta bar ya karibu unakamata kitu ya baridii, ikiwa tayari anakupigia cmu, unaenda kukolect na unaenda straight ubalozi kwa visa!
 
<br />
kuna taratibu pale kwa ajili ya emergency passport. Kuna watu kwao kutoa rushwa ni mwiko. Hivi inawezekana vipi kama leo hii zimejaa kelele za ufisadi halafu kisha mtu ukatoe rushwa? Jamani. Tuseme hapana na wale wenye tabia hizo waache. Ni tabia mbaya saana kuzoea kuishi bila kufuata utaratibu na kuita kimjini mjini au kuamini mambo ndio yanatakiwa yawe hivyo. Kwa mwendo huu, hata tuhamishie Tanzania serikali toka popote kusonga mbele ni ndoto!
 

vitafunwa
 
muda uliotumika kuandika hapa ungekuwa umeshapiga hatua katika ufuatiliaji. wiki moja inatosha(may be kwa sasa)mimi nilipata kwa siku tatu mwaka 2006 bila kutoa chochote wala bila kufahamiana na afisa yeyote
 

nakuunga mkono asilimia 100. watu wapuuzi sana kiherehere kutanguliza rushwa. anyway inawezekana nao ni wapokeaji wa rushwa kwenye ofisi zao ndio maana wako mbele kupokea rushwa. katika vitu ambavyo huwa haviko akilini mwangu ni kutoa rushwa.rushwa ni adui wa haki.
 

nakuunga mkono asilimia 100. watu wapuuzi sana kiherehere kutanguliza rushwa. anyway inawezekana nao ni wapokeaji wa rushwa kwenye ofisi zao ndio maana wako mbele kupokea rushwa. katika vitu ambavyo huwa haviko akilini mwangu ni kutoa rushwa.rushwa ni adui wa haki.
 
 
Aisee
mimi ninashukuru ila ilikuwa siku kuu kwangu
nilienda uhamiaji nikajaza fomu na vitambulisho kamili uwe na vitu kamili, niliipata kwa siku moja yaani kama masaa 6 tu niliipata, kama wewe una shida na vitu vipo kamili wanakupa kwa ni na wao ni watu pia, wala sikutoa kitu yaani jama analeta pass yangu hata kuuliza chai hakutaka aliita jina na kunipa,
kwa kweli ninashukuru sana, na nilikuwa ninaharakisha sana inafanana na yako

Omba mungu unaweza kupata bila ya shida yoyote ile
 
Nenda immigration office ukiwa na mahitaji yako yote kamili pamoja na hizo karatasi za masomo zinazo-onyesha ni lini unatakiwa uanze chuo, ambatanisha na ticket yako, viambatanishi vyote peleka orijino wazione na kopi zitakazobaki pale. Asikutishe mtu. It took me three days only kubadili passport ya zamani kuja mpya, nadhani wale pale wote wanaelewa dharura ni nini. Asikudanganye mtu kuhonga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…